Ushauri wangu Kwa wale wanaotaka kuagiza magari kipindi hiki

Sijui nini kinaendelea. Lakini huwa naagiza mzigo Germany. UK,Denmark na huwa napeleka bank invoice tu wanakata kwenye akaunti yangu ya Tz, Hizo hapo ni nchi tatu zenye currency tofauti. Same magari UK huwa naagizia watu procedure ni hio hio. Ukiniambia USD kuna uhaba kila mtu anajua. Anyway mara ya mwisho ni,menunua gari BeFoward nililipia kwa Tzs kulingana na Dollar raye ya wakai huo(kulikuwa hakuna huu uhaba wa dollar).
 
Btw mdogo wangu kaagiza gari Japan wiki mbili zilizopita nimemuuliza kalipaje,kasema kaenda bank yake katuma direct Jp bila shida,
 
byakunu umeeleza vizuri Sana kwasababu umekutana na hii changamoto Kwa kifupi ni Hali ngumu Sana kama unataka kuagiza gari.
Kila njia ya malipo hawataki Hadi ulipe Kwa dollar Tu na hii ni Kwa agents wote yaani mpaka ufanye mipango ya kupata dollar vinginevyo hakuna njia nyingine. Sipati picha baada ya mwezi July Hali itakuaje baada ya serikali kutangaza manununuzi Kwa Tsh
 
2020 niliagiza gari bila shida yeyote nilienda bank na invoice ya SBT nikajaza fomu zote na pesa ikafika Japan. Mimi nimefanya malipo tar 16/05 na pesa imefika kwenye account ya SBT Japan tar 25/05 yaani ni usumbufu juu ya usumbufu
 
Hongera mwamba…..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…