Ushauri wangu kwa Wanasiasa wa kweli walio ACT Wazalendo na CHADEMA

Ushauri wangu kwa Wanasiasa wa kweli walio ACT Wazalendo na CHADEMA

Ndugu, lazima tuelewe kuwa kufanya siasa za upinzani nchi hii ni ngumu sana sababu ya mifumo ya kiutawala na kisiasa iliyopo. Nimesema hivi baada ya kusoma hiyo suggestion kuwa waandike proposal ya kupata funds EU au US kwa zamani labda yes, ila kwa sasa hizo pesa zitapita wapi ndugu?

Hata hivyo tuendelee kuwa kuwapongeza wapinzani aina ya Lissu, if you know what i mean.
Zitapita kwenye mfumo huu huu wa kawaida wa kifedha. Kama Ccm ni wababe basi wataifishe izo hela na watapata matokeo sasa!!
 
Huu ushauri wangu hauhusishi wanasiasa njaa/ Wanasiasa Maslahi, bali wanasiasa kweli wenye uchungu na nchi yao. Waliopo kwenye siasa kwa dhumuni la kuleta itikadi mbadala inayoenda kuleta mabadiliko ya kweli nchini katika maendeleo ya wananchi yanayoongozwa na demokrasia ya kweli na sio wanasiasa maslahi, wanaochukulia siasa kama ajira au sehemu ya kujijenga kimaisha na kikipato.

NAJUA CCM wamejipanga kuondoa credibility ya vyama vyenu kwa wananchi. Na hili ni kwenye mitego hii waliyowawekea ya nafasi za uwakilishi/ ubunge na kwenye serikali.

Tayari kuna wanasiasa Chadema wameingia kwenye mtego huu na wameenda kuapa leo Bungeni. Najua kuna wanasiasa wa ACT WAZALENDO nao watafanya hivyo Tanzania bara na kule visiwani. Hili litahusisha wanasiasa wakubwa na wadogo mpaka wale ambao hawakutegemewa.

Najua hili litaleta mpasuko mkubwa sana, najua hili litashusha morali ya wananchi kwa kiwango kikubwa katika kupata Tanzania njema yenye maendeleo na demokrasia ya kweli. Ila naomba msikate tamaa

Kwenye hali hii ndo mtajua nani yupo kwenye vyama kwa maslahi yake na familia yake na nani yupo kwa maslahi ya Watanzania walio wengi na Taifa hili. Mtajua nani anamini itikadi zenu na nani a naamini siasa ni fursa ya kujijenga kimaisha.

Hatua hii mnayopitia ni muhimu sana kwa sababu ndo mnaenda kupata ile cream ambayo ipo kweli katika kuangalia itikadi na wala sio maslahi. Katika hili kumbukeni pia ni lazima mpitie hili ili mjue kuwa njia ya kwenda Kupata mabadiliko ya kweli wala sio rahisi. Ni lazima mjue kweli rangi halisi za kila mmoja wenu ili kweli Taifa hili likapate ukombozi wa kweli wa kifikra na kimaendeleo. Kumbukeni ukombozi wa kweli upo kwa watu wenye nia na akili ya dhati ya kuleta ukombozi huo.

Naomba msikatishwe tamaa. Kama vyama vyenu vimekuwa corrupted jiondoeni kwenye hivyo vyama. Kama mkiweza waondoeni hao wote walio kimaslahi na mjenge kweli taasisi zenu imara ambazo zimekaa katika kuamini itikadi zenu kwa maendeleo ya kitaifa ya wananchi wote na wala sio taasisi zilizojaa watu wanaoangalia niendeshe gari gani au niwe na maisha gani binafsi .

Kama mkichagua kuwaondoa hao watu corrupt kwenye vyama vyenu sasa anzeni rasmi kuvijenga vyama vyenu katika kuamini itikadi zaidi. Andikeni proposals ziende EU na hata USA, wawape funds na mzitumie kweli kuvijenga vyama vyenu na kujenga taasisi imara zilizo na watu imara na waaminifu ambao wako ndani ya hizo taasisi kwa sababu ya itikadi na wala si vinginevyo. Nilisikiliza majadiliano ya Kamati ya Bunge la Umoja wa Ulaya. Walijadili hili suala la kutoa hela moja kwa moja kwa watu wanao advocate democracy na human rights. Sasa jiandaenii katika kuitumia hii nafasi. Mkipata hizi hela ambazo ni nyingi kuliko hata hizo ruzuku, jengeni ofisi za maana katika kila kanda zenu, zitumieni hizo hela kujiimarisha kivifaa na kiteknolojia Kama kuanzisha television, radio au hata magazeti ambayo yataelimisha umma juu ya itikadi zenu kwa ajili ya maendeleo ya watu. Vilevile mzitumie hizo hela katika kuwajenga wanachama wenu kwenye mafunzo hasa sehemu mbalimbali duniani wakasome na kupata exposure ili waweze kuzielewa na kuziishi itikadi zenu

Kama mkichagua kujiondoa, naomba sasa mtengeneze taasisi imara zaidi ambayo iko nje ya ivyo vyama. Na muitumie iyo taasisi kufanya hayo niliyosema hapo juu.

Kuleta Mabadiliko ya kweli katika nchi yeyote si jambo jepesi. Kuleta mabadiliko ya kweli katika nchi zilizokulia mfumo wa kisocialist wala si jambo jepesi zaidi. Naomba mjijenge upya kwenye hayo na wala msiangalie waliowasaliti wala matumbo yenu, bali angalieni mustakabali mpana wa Taifa letu katika kuijenga Tanzania Nzuri yenye demokrasia ya kweli na maendeleo ya kweli yanayomnufaisha kila mwananchi na wala sio kikundi cha watu wachache.

Tanzania ya kweli itapatikana tu, Tanzania yenye watu genuine, wasioangalia matumbo yao bali wanaoiangalia Tanzania yote na wananchi wao na ustawi wao wa kweli.

Mungu awabariki!
Kwa nini wewe usianzishe hicbo chama unachodai cha kutetea maslahi ya watanzania unataka wengine ndio waanzishe? Usione mtu analima ukadhani ni kwa sababu udongo ni mlaini ukishika jembe ndio utajua.

Siasa ni watu na ufuasi, siasa ni kutumia kila fursa halali sio kupambana na dola kila wakati.

Hao wabunge wa CDM watapata fursa nzuri ya kupigania maslahi ya watu wao na nchi bungeni kuliko kama wangegoma.

Kupambana kwa kutumia key board kama unavyofanya ni rahisi kuliko kupambana katika real world.

Hizo pesa za EU hazitolewi kama njugu, kwanza kuna masharti na activities zinazoruhusiwa sio kila activity unaweza kutumia hizo pesa. Pili kuna sheria za ndani ya nchi ambazo nazo haziruhusu uingizwaji wa fedha holela toka nje kwa ajili ya kuchochea vurugu hivyo zinaweza zisiruhusiwe kuingizwa.

Katika siasa hakuna adui wala rafiki wa kudumu kama kweli uko interested na siasa utakuwa unalijua hilo.

Fanya kazi ujiletee maendeleo usidanganywe na wanasiasa.
 
Mwanasiasa gani wa kweli na kila mmoja anampinga ccm ili apate yeye nafasi ya kula!
Maccm yana akili za ajabu sana kilichowafanya ccm kuiba kura , kupora ushindi , kufunga , kuteka , kubambika kesi , kupiga , kujeruhi , kuua na kumwaga damu za watu wasio na hatia sio kula we Pimbi ? .
 
Kila mtu ana wajibu wake ndugu. Hata ulaya, China na Marekani kulikuwa na watu kama Mimi. Sio kila mtu alienda mbele kupambana. Wengine waliandika vitabu na articles ambazo ziliwapa morali na maarifa wapiganaji na frontlinies.
 
Kwa nini wewe usianzishe hicbo chama unachodai cha kutetea maslahi ya watanzania unataka wengine ndio waanzishe? Usione mtu analima ukadhani ni kwa sababu udongo ni mlaini ukishika jembe ndio utajua.

Siasa ni watu na ufuasi, siasa ni kutumia kila fursa halali sio kupambana na dola kila wakati.

Hao wabunge wa CDM watapata fursa nzuri ya kupigania maslahi ya watu wao na nchi bungeni kuliko kama wangegoma.

Kupambana kwa kutumia key board kama unavyofanya ni rahisi kuliko kupambana katika real world.

Hizo pesa za EU hazitolewi kama njugu, kwanza kuna masharti na activities zinazoruhusiwa sio kila activity unaweza kutumia hizo pesa. Pili kuna sheria za ndani ya nchi ambazo nazo haziruhusu uingizwaji wa fedha holela toka nje kwa ajili ya kuchochea vurugu hivyo zinaweza zisiruhusiwe kuingizwa.

Katika siasa hakuna adui wala rafiki wa kudumu kama kweli uko interested na siasa utakuwa unalijua hilo.

Fanya kazi ujiletee maendeleo usidanganywe na wanasiasa.
Mkuu;
Hawa vijana wanaofanya ''schoolboy politics'' hawawezi kukuelewa!

Mtu anayedhani anajua wakati hajui ni vigumu sana kama sio haiwezekani kumuelimisha na kukubali kuelimika!

Yaani anafikiri nchi inaendeshwa tu kinadharia huku yeye akiwa nyuma ya keyboard/keypad!
 
Maccm yana akili za ajabu sana kilichowafanya ccm kuiba kura , kupora ushindi , kufunga , kuteka , kubambika kesi , kupiga , kujeruhi , kuua na kumwaga damu za watu wasio na hatia sio kula we Pimbi ? .
Ccm wana silaha 2 tu. Vyombo vya dola na ulaghai wa pesa na vyeo. Uzuri zinajulikana na wala haziwezi kutupa tabu
 
bali wanasiasa kweli wenye uchungu na nchi yao. Waliopo kwenye siasa kwa dhumuni la kuleta itikadi mbadala inayoenda kuleta mabadiliko ya kweli nchini katika maendeleo ya wananchi
Humkuti wa hivi hata mmoja katika vyama ulivyovitaja
 
Muulize Halima mdee ana haya majibu!
Maccm yana akili za ajabu sana kilichowafanya ccm kuiba kura , kupora ushindi , kufunga , kuteka , kubambika kesi , kupiga , kujeruhi , kuua na kumwaga damu za watu wasio na hatia sio kula we Pimbi ? .
 
Kama tuna siasa ya Kupinga ili tupate nafasi ya kula basi ni bora tusiwe na siasa. Maaana siasa kama siasa ni ushindani wa itikadi katika kufanikisha maendeleo ya wananchi na Taifa
Halima anayo majibu ya maswali yako!
 
Wakiamua kuwafukuza wawe makini Kwakuwa ndugai atakaa nao Bunheni na watatumika kuanzisha CDM B, rejea kufa kwa CUF mpk Maalim Seif kujikuta ACT
 
Wakiamua kuwafukuza wawe makini Kwakuwa ndugai atakaa nao Bunheni na watatumika kuanzisha CDM B, rejea kufa kwa CUF mpk Maalim Seif kujikuta ACT
Vyovyote vile. The two options I have recommended should be considered.
 
Halima anayo majibu ya maswali yako!
Huyo uliyemtaja hana credibility yeyote ya kusema lolote na akaaminika. She has lost everything. Hakuna kitu ata simamia bungeni na kukisema akaaminika tena!!
 
Back
Top Bottom