Ushauri: Wapi niwekeze hela yangu ya kustaafu kama Tsh. milioni 100

Ushauri: Wapi niwekeze hela yangu ya kustaafu kama Tsh. milioni 100

Kimla

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2008
Posts
3,810
Reaction score
6,599
Mimi sio mtaalamu wa biashara na sitaki kujenga, nataka nipate ushauri wa wapi niwekeze kwa sasa ili nizalishe kupata pesa ya kujikimu bila kuharibu mtaji hadi hapo nitakapopata maarifa bora.

Eg. Fixed account;; Je, benki gani ina-rate nzuri zaidi ya 10% kwa mwaka?

Je, ninunue tresury bills na bonds, lakini nazo sizijui vizuri. Nahitaji mtu kunishauri
Je, option ipi watu mnaifahamu.

Asante
 
Kujenga ndio sehemu utakayoiona pesa yako mpaka kufa kwako... ila uwekezaji mwingine hautabiriki.

Ila uwe makini na location unayojenga.. wapangaji wanachagua maeneo.. sio ubora wa nyumba peke yake... ukijenga kerege sijui nje ya mji.. itakula.kwako
 
Think of having industry. Fanya market research, naamini utatoboa.

Mfano;
Kiwanda cha chupi
Kiwanda cha Sox
Kiwanda cha packaging vinalipa sana kwani muelekeo wa dunia ni kila kitu kinasindikwa
Hivyo utapa kiwanda cha food packaging material
Kiwanda cha Celotape
Kiwanda cha kuprint mabox.

Njoo tushauirizane
 
Chukua 70m fanya chochote.30m zinazobaki kanunue baiskeli Japan (Kobe) . Baiskeli moja ni kati ya 15k hadi 30k Tsh
Container Moja la futi 20 linachukua Baiskeli 240 na container la futi 40 linachukua bike 500 -600.
Baiskeli moja kwa rejareja mtaani inaanzia 135k za kawaida kabisa.
Asume kila bike ifike kwa garama ya maximum Tsh 50k.the rest is profit
NB:Safari Zako 4 za kwanza kuagiza mzigo usizumunie kupata profit zumunia kurudisha mtaji badae utapiga hela sana na mm utanitumia shukran [emoji16][emoji16][emoji16]
Screenshot_20200122-221932~2.jpeg
Screenshot_20200122-221839~2.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi sio mtaalamu wa biashara na sitaki kujenga, nataka nipate ushauri wa wapi niwekeze kwa sasa ili nizalishe kupata pesa ya kujikimu bila kuharibu mtaji hadi hapo nitakapopata maarifa bora.

Eg. Fixed account;; Je, benki gani ina-rate nzuri zaidi ya 10% kwa mwaka?

Je, ninunue tresury bills na bonds, lakini nazo sizijui vizuri. Nahitaji mtu kunishauri
Je, option ipi watu mnaifahamu.

Asante
Mkuu

Mkuu kwanza nikupongeze kwa kustaafu, lakin pia nimeona kwenye uzi wako umesema hutaki kujenga ijapokuwa sjajua hutaki kujenga nyumba ya kuishi au ya biashara lakin mim kwa uzoefu wangu kwenye nyumba za biashara na ukachagua location nzuri utapata hela japo sio nyingi sana lakin utajikimu kwa maisha yako yote baada ya kustaafu.

Mfano kwa uzoefu wangu ungekuwa na kiwanja maeneo ya jirani na mji yaan kuanzia km 10 - 15 hivi kutoka mjini hiyo hela ingekutosha kujenga nyumba mbili za maana ambazo zitakuigizia kuanzia laki 8 hadi milion kwa mwezi ambayo kwa wew mstaafu ukiongezea na "retired salary" uongo maisha yanaenda bila stress kabisa.( kama huna kiwanja hii hela ni ndogo kununua kiwanja na kujenga nyumba mbili labda unaweza kununua na kujenga nyumba moja).

Naona pia umezungumzia "Fixed account" ni kweli miaka ya nyuma kidogo kuanzia 2016 ilikuwa inalipa kwani kuna benki zilikuwa zinatoa hadi 12% lakin kwa sasa kulingana na hali ya uchumi ilivyo benki nyingi zinatoa 5 % ambapo hili unaweza kulifikiria kama utashindwa kujenga nyumba ukapata hela kidogo bila stress.

Sikushauri sana ukafanye kitu kipya kabisa kwani mwisho wa sku utajikuta huna hela na hakuna ulichofanya kwani kwa umri wako kama ni kufanya kitu ilifaa uanze kabla ya kustaafu ili sasa iwe ni muda mzuri wa kukiendeleza.
 
1. Fixed deposit six months wakati unajipanga you will get max of about 7.8% ukiziacha kwenye account wanakula kodi taratibu

2. BONDS

3. TRESURY BILLS
1- 3 are the best options HELA YA KUSTAAU HAIJENGI NYUMBA UTAFILISIKA MARA MOJA NA KUFA MAPEMA......
 
Asante, je for number 1.. benk gani inafixed ya 7.8% kwa annum kwa miezi 6?
2.Bonds na Tresury billis huwa zinalipaje?
 
Wewe acha kumdanganya basikeli bei yake ni 105,000.
Ukichukua 2 pcs na kuendelea ni 95,000.
Zenji ndo kabisa 75,000.
Chukua 70m fanya chochote.30m zinazobaki kanunue baiskeli Japan (Kobe) . Baiskeli moja ni kati ya 15k hadi 30k Tsh
Container Moja la futi 20 linachukua Baiskeli 240 na container la futi 40 linachukua bike 500 -600.
Baiskeli moja kwa rejareja mtaani inaanzia 135k za kawaida kabisa.
Asume kila bike ifike kwa garama ya maximum Tsh 50k.the rest is profit
NB:Safari Zako 4 za kwanza kuagiza mzigo usizumunie kupata profit zumunia kurudisha mtaji badae utapiga hela sana na mm utanitumia shukran [emoji16][emoji16][emoji16]View attachment 1368928View attachment 1368929

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hauwezi kutapeliwa Kama hauna tamaa

Utakuja kunikumbuka siku ambayo utabakiwa na ATM iliyo empty
 
Katika kanuni tano za fedha.. Haya yafuatayi yanakuhusu.

Kwanza, usitake madili ya haraka haraka. Ukiona dili ni zuri sana, na halina effort kubwa, shtuka ,shtuka haswaa.

Pili, wekeza ktk jambo unalolijua, au fanya utafiti wa kina, ukiona umeridhika weka hela humo. Tafuta mtu mzoefu, mwenye hekima ya unachotaka kufanya, usiimgie kichwa.

Tatu, hiyo fedha igawanye. Usiingiz yote kwa pamoja, wala usiwekez ktk vitu vingi. Tenga amount kidgo, lets say Ten milion weka sehem, then angalia maendeleo.

Tumia akili ya kuzaliwa tu.
 
Mimi sio mtaalamu wa biashara na sitaki kujenga, nataka nipate ushauri wa wapi niwekeze kwa sasa ili nizalishe kupata pesa ya kujikimu bila kuharibu mtaji hadi hapo nitakapopata maarifa bora.

Eg. Fixed account;; Je, benki gani ina-rate nzuri zaidi ya 10% kwa mwaka?

Je, ninunue tresury bills na bonds, lakini nazo sizijui vizuri. Nahitaji mtu kunishauri
Je, option ipi watu mnaifahamu.

Asante

Kama hukuwekeza tangia upo kijana tegemea anguko kubwa,weka Iyo pesa bank uwe unajilipa mshahara kila mwezi hadi siku utapotangulia mbele za haki

Sent using IPhone X
 
Mkuu,kama umestaafu,huna majukumu ya kimaisha kama vile kusomesha etc na unavitega uchumi vya kukuwezesha kuishi basi nakushauri ufanye yafuatayo.

Gawa Pesa yako katika makundi manne:
Kundi la kwanza liwe urithi-
Kundi la Pili liwe sadaka
Kundi la tatu liwe akiba
Kundi la nne liwe uwekezaji

Kwenye Hela ya Urithi weka kwenye T-Bonds au kwenye Fixed deposit ya muda mrefu kutegemea na kiasi cha riba.

Hela ya sadaka tumia kuwekeza katika kutatua changampoto ya kijamii katika eneo lako.Hasa inayohusu elimu au afya.Unaweza kuanzisha NGO yako ukajenga legacy yako nzuri tua kama philantropist.Kuna mahitaji mengi sana katika jamii ambayo yanaitaji watu wenye moyo wa kutoa.Na pia unapojenga NGO yako unaweza pia kupata michango ya wafadhili ili uweze kupiga hatua kubwa zaidi na kusaidia wengi.

Kwenye hela yako ya akiba weka benki tu ili ipate faida taratibu na huku ukiitumia kwa mambo yako madogo madgo kama kununua luku n.k.

Kwenye hela yako uwekezaji hio unaweza ukatumia muda kutafiti aina ya biashara ya kufanya ambayo ina faida nzuri na usiwe na haraka nayo.

Jambo unapaswa kuwa na haraka nalo na la hela ya SADAKA.hilo anza nalo mapema sana na litakusaidia kupata BARAKA nyingi kwa kusaidia wahitaji na kuacha LEGACY katika eneo unaloishi

Nakutakia kila la heri na karibu sana iwapo unahitaji msaada na ushauri zaidi.
 
Wewe acha kumdanganya basikeli bei yake ni 105,000.
Ukichukua 2 pcs na kuendelea ni 95,000.
Zenji ndo kabisa 75,000.
Hapana hajamdanganya.

Wewe unaongelea bei za tanzania bara na visiwani ilihali yeye kaongelea kuagizia mzigo japan.
Na ni kweli hizo ndio bei za baikeli huko japan kwanzia pc 230 na kuendelea
 
Hapana hajamdanganya.

Wewe unaongelea bei za tanzania bara na visiwani ilihali yeye kaongelea kuagizia mzigo japan.
Na ni kweli hizo ndio bei za baikeli huko japan kwanzia pc 230 na kuendelea
Na wewe hujanielewa.
Nimeongelea bei ya kuuza hapa mjini ni sh 105,000 mpaka 95,000 si 135,000.
Tofauti ya 30,000 mpaka 40,000 kwa pieces moja ni kubwa sana.
 
1. Fixed deposit six months wakati unajipanga you will get max of about 7.8% ukiziacha kwenye account wanakula kodi taratibu

2. BONDS

3. TRESURY BILLS
1- 3 are the best options HELA YA KUSTAAU HAIJENGI NYUMBA UTAFILISIKA MARA MOJA NA KUFA MAPEMA......
Umemaliza Kama kweli ana Nia ya dhati afuate huu ushauri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom