Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Kuna rafiki yangu mmoja amekutana na changamoto za kifamilia. Yeye ni singo maza, ila huwa tunapeana kampani na ushauri mbalimbali pale panapohitajika.
Waliachana na mumewe, miaka saba iliyopita na walifanikiwa kupata watoto wawili wa kiume; ambao kwa sasa mmoja ana miaka 13 na mwingine 9. Sababu kubwa ya kuachana, ilikuwa fumanizi; na mbaya zaidi baada ya kuachana, yule mwanaume alitafuta mwanaume mwenzie na kumfanya mke, wakawa wanaishi pamoja.
Siku za hivi karibuni, huyu mwanamume aliyezaa na huyu singo maza akawa anawataka watoto wake; anataka akaishi nao. Kutokana na tabia ya huyo mwanaume, mama wa watoto hayuko tayari waende kwa baba yao, kwa sababu anahofia anaweza kuwaharibu watoto kutokana na hiyo kashfa aliyokuwa nayo.
Chakusikitisha usiku huu, huyu singo maza amenipigia simu kuniomba ushauri; kuwa watoto joni ya leo wanalia na wanataka waende kuishi na baba yao. Mama kwa uchungu anafikiria, gharama alizotumia kuwalea na leo watoto wanataka waende kwa baba yao asiyekuwa na msimamo au akili za kiume. Hofu kubwa, baba yao anaweza kuwaharibu.
Nilichomshauri, hili swala walimalize kifamilia; wazazi wa pande zote mbili wakae waangalie namna ya kutatua huo mgongano.
Wakuu, leteni ushauri...