Ushauri: Watoto wanataka kuishi na Baba ambaye aliachana na Mama yao baada ya kuanzisha mahusiano na Mwanaume mwenziye

Ushauri: Watoto wanataka kuishi na Baba ambaye aliachana na Mama yao baada ya kuanzisha mahusiano na Mwanaume mwenziye

mfua
Kuna rafiki yangu mmoja amekutana na changamoto za kifamilia. Yeye ni singo maza, ila huwa tunapeana kampani na ushauri mbalimbali pale panapohitajika.

Waliachana na mumewe, miaka saba iliyopita na walifanikiwa kupata watoto wawili wa kiume; ambao kwa sasa mmoja ana miaka 13 na mwingine 9. Sababu kubwa ya kuachana, ilikuwa fumanizi; na mbaya zaidi baada ya kuachana, yule mwanaume alitafuta mwanaume mwenzie na kumfanya mke, wakawa wanaishi pamoja.

Siku za hivi karibuni, huyu mwanamume aliyezaa na huyu singo maza akawa anawataka watoto wake; anataka akaishi nao. Kutokana na tabia ya huyo mwanaume, mama wa watoto hayuko tayari waende kwa baba yao, kwa sababu anahofia anaweza kuwaharibu watoto kutokana na hiyo kashfa aliyokuwa nayo.

Chakusikitisha usiku huu, huyu singo maza amenipigia simu kuniomba ushauri; kuwa watoto joni ya leo wanalia na wanataka waende kuishi na baba yao. Mama kwa uchungu anafikiria, gharama alizotumia kuwalea na leo watoto wanataka waende kwa baba yao asiyekuwa na msimamo au akili za kiume. Hofu kubwa, baba yao anaweza kuwaharibu.

Nilichomshauri, hili swala walimalize kifamilia; wazazi wa pande zote mbili wakae waangalie namna ya kutatua huo mgongano.

Wakuu, leteni ushauri...
MFUASI WA DAVID CAMEROON NA KIZAZI CHAKE, MUNGU TUKINGE NA HAYA
 
Aende mahakamani
 
Kwa kesi nazosikia mara nyingi watu wa hivyo huwaingilia mpaka watoto wao,sasa sijui itakuaje yaani
 
Kwa tabia hiyo kama ni kweli ningekuwa mimi Mamndenyi huyo mwanaume nisingeongea naye mpaka kifo.

Hao watoto ningewaambia ukweli kuhusu tabia ya baba yao.

Misikiti Makanisa hadi miti ingejua tabia ya huyo baba labda ahame nchi.
Ndo suluhisho hilo?
 
Kama anao ushahidi wa huyo mwanaume kuishi na mwanaume mwenzake, anaweza kuutumia ustawi jamii kubaki na watoto kisheria.
 
Kama anao ushahidi wa huyo mwanaume kuishi na mwanaume mwenzake, anaweza kuutumia ustawi jamii kubaki na watoto kisheria.
Ana ushahidi huyo mume anaishi na huyo mwanaume km mke na mume? Hili suala ni pana sana.
 
Kwanza tuanze na wewe shoga inamaana mme wa rafiki ako humjui,
Na kama humjui basi huyo sio rafiki ako
Na kama ni rafiki ako kweli basi urafiki wenu umeanza baada ya kuachika

Je kashawahi kukusimulia kisa kama hichi hapo mwanzo au ni baada ya watoto kutaka kwenda kukaa na baba yao

Na kama ni kweli baba yao shoga kwanini alikuwa anawaruhusu watoto kwenda kumpa hai baba yao

Bibie hapo unafungwa kamba na kwa ramli chonganishi huyo best ako anakutegemea wewe sana yaan wewe ndo mtatuaji wa shida zake hata kifedha

Je kashawahi kukusimulia kuwa amewahi kutoa tigo ili tuunganishe dots
 
Yani kwamba mtoto mpk anakua hajui kuwa duniani vipo UTAKAVYOVIPATA NA HUVIHITAJI NA UTAKAVYOVIHITAJI NA HUVIPATI.

Ni namna mbovu sana ya malezi.

Kwamba CHOCHOTE UTAKACHO NI LAZIMA UPATE.
kwa mbinu chafu, safi, kwa kujeruhi wengine , kwa kuondoa utu binafsi ila mradi UPATE.
aiseeeh!!

Niliwahi kumwambia mtu tujifunze hata kuwa rejected ni aina ya stadi tunapaswa kufundisha watoto.
Ili wabaki salama, dujia hii watu sio wema.

Sio wakati wote anapaswa kuwa A PRIVILEDGED.
Sio kila kitu mradi tunaweza kuwapatia ni cha kuwapa.
Mtoto ajue mzazi anaweza
kusema HAPANA hata katika yale kwa jicho lake anaona nI NDIO.
Wakati mwingine sina sababu ya kuelezea sababu.

Mtoa mada mwambie rafiki yako
NO is a COMPLETE SENTENCE!!
Sasa hii habari ya watoto wanalilia kwenda kwa baba yao, yeye mama anaona kabisa baba si mzazi salama.
HAKULAZIMIKA HATA KUWAZA ANAPASWA KUWAELEZA SABABU!!

Hakuna kwenda , na hakuna kwenda amaanishe
Huyo baba hata angekuwa mama, upambane Naye binafsi kwa kumwambia sikuruhusu kukaa na watoto kwa kuwa 1,2,3. Na ukilazimisha nitawaambia watoto, watu wengine na Mamlaka husika kwann nakataa usiishi na watoto.
Ukihitaji kuwaona, njoo uwasalimie nyumbani kwangu.
Kuna vitu sio vya kuwa lelemama, SPEAK!!
ONESHA MSIMAMO NA USIMAMIE.
 
Back
Top Bottom