Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,595
Asali ni mojawapo ya vyakula vinayofahamika kuwa na sifa ya kubeba vimela vya masalia ya bakteria wanaoitwa Clostridium botulinum.
Bakteria hawa ni hatari kwa watoto wenye umri chini ya mwaka mmoja kwa kuwa mfumo wao wa kinga za mwili hasa kwenye utumbo huwa bado ni dhaifu. Wanaweza kukaa humo na kuzaliana kwa wingi, kisha huzalisha sumu (botulinum neurotoxin) ambayo huathiri mfumo wa fahamu kwa kusababisha tatizo linaloitwa Infant botulism.
Ikiwa sumu hii itazalishwa mwilini, inaweza kumfanya mtoto agome kula, apatwe na choo kigumu, kupooza kwa mfumo wa upumuaji, kuweweseka, kulegea kwa misuli ya uso, kutapika na kukauka kwa midomo.
Kwa kuwa tatizo hili halionekani mara kwa mara, pia kwa kuwa ni ngumu kujua asali iliyo salama na isiyo salama kwa kutazama, Kituo Cha Udhibiti na Kinga ya Magonjwa Cha Marekani (CDC) hushauri watoto wenye umri chini ya mwaka mmoja wasipewe asali kama sehemu ya kuwakinga.
Watoto wenye umri zaidi ya mwaka mmoja, wajawazito, wazee na makundi mengine yote wanaweza kutumia chakula hiki chenye utajiri mkubwa wa virutubisho pasipo shida yoyote kwa kuwa miili yao huwa na kinga imara ya kuharibu sumu inayoweza kuzalishwa mwilini ikiwa bakteria hao watakuwepo.
Chanzo: CDC