Ushauri: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa 2025 chukua fomu ili uliokoe taifa letu na hili genge. Tunajua msimamo wako na uchapakazi wako

πŸ˜³πŸ˜³πŸ˜³πŸ˜³πŸƒβ€β™‚οΈπŸƒβ€β™‚οΈπŸƒβ€β™‚οΈ
 
Miaka miwili tu lakini taifa letu lina hali mbaya baada ya hili genge kukamata usukani.

Maisha ya watanzania yanatia huruma. Uwezo wa kula hata mlo mmoja ni ngumu kwa kila kaya...
Kuwa makini utasababisha hata hiyo 2025 yako unayotaka agombee asifike kwani Yeye sasa hivi amekuwa kama Swala anayewindwa na Simba, Kifaru, Chui na Nyati.

Mbarikiwe wale mlionielewa tu hapa.
 
Mmm,sijui kama anaweza kuwa nje ya hilo genge unalo lisema ,au unajitekenya ili wacheke wengine???
 
Huwezi kumtenganisha Waziri mkuu na mafanikio au failures za serikali kwani yeye ndio mtendaji mkuu wa serikali ndio maana akiamua kujiuzuru baraza lote la mawaziri litakuwa limevunjwa automatically.
 
Busara gani huyo Jamaa Mimi namjua kukuzidi wewe Hana Elimu alikuwa mwalimu shule za msingi baadae secondary baadae chama Cha walimu baadae Mkuu wa wilaya hiyo degree yake ya mchongo Elimu yake ni Diploma tu
Uwe na machache ya kusema omwana wa Tata.
 
Ndio nini?
Wanakukumbusha jinsi huyo mtu alivyo mwongo.

Na jingine la wazi ni kwamba huyu unayempigia chapuo, kama walivyokuwa vjongozi wengi wa awamu ya 5, ni mla rushwa, na pale Dodoma mpaka amejengewa nyumba na tajiri mmoja kutokana na kumsaidia kwenye uovu wake.

Kwa upeo wako mdogo, unaamini wakti boss wake anaiba pesa na kutoroshea China, huyu alikuwa hajui? Wakati boss wake anaiba ile trilioni 1.5, na kisha kuwaziba watu midomo na kufunga uhuru wa vyombo vya habari ili watu wasipate taarifa ya uovu wao, yeye hakuwa anajua wala kuhusika?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…