Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Marehemu alipenda sana kufanya kazi na watu wanafiki. Uwezo wake mdogo, wakati wa utawala wa marehemu, ulimfanya afanye mambo mengi kwa kukurupuka.Busara gani huyo Jamaa Mimi namjua kukuzidi wewe Hana Elimu alikuwa mwalimu shule za msingi baadae secondary baadae chama Cha walimu baadae Mkuu wa wilaya hiyo degree yake ya mchongo Elimu yake ni Diploma tu
Kule Mtwara alimsimamisha daktari bingwa wa upasuaji ambaye alikuwa mmoja tu mkoa mzima, kisa kuna mama kalalamika mbele yake kuwa kabla ya upasuaji aliambiwa alipe 80,000. Naye kwa kukurupuka na kutafuta sifa za kijinga, akatangaza pale pale kuwa eti amemsimamisha kazi huyo daktari. Kuja kufanya uchunguzi, sh. 80,000 haikuwa rushwa bali ni kiwango cha utaratibu wa kuchangia gharama za matibabu, na aliyekuwa akipokea pesa hiyo wala hakuwa daktari, daktari alimwelezea tu yule Mama utaratibu uliopo kwenye hospitali.
Kwa aibu, kimya kimya, akaamuru daktari arudishwe kazini. Daktari naye akagoma kutokana na kudhalilishwa kwenye mkutano wa hadhara, hospitali ikabakia bila ya daktari bingwa wa upasuaji.