Salaam,Shalom!!
Nimesikia Mh Mwigulu, waziri wa Fedha akilalama kuwa, Wafanyabiashara waliopewa nafasi ya kukusanya Kodi Kwa niaba ya Serikali ni chanzo Cha kukosekana mapato ya Serikali.
Ukisikiliza Kwa ufahamu kauli hiyo, analenga kuwaelekeza TRA warudi tena Kwa wafanyabiashara na kuwabana tena wakipigiwa Kodi kandamizi za miaka ya nyuma. Nia hii inapingana na Nia ya Rais ya kukusanya Kodi Kwa akili.
Nia hiyo ya kuminya wafanyabiashara Si njema, na kamwe haiwezi kuinua Uchumi wa Nchi yetu, kupata Kodi, ni LAZIMA kuwatengenezea wadau mazingira mazuri ya biashara.
Mazingira mazuri ya biashara nchini, ni pamoja na kupunguza gharama ya umeme, BWAWA limejengwa Kwa mkopo, na pesa Inatakiwa ilipwe, kupunguza Bei ya unit ya umeme kutasaidia kuongezeka Kwa domestic industries za chini, kati na juu. Kukua Kwa viwanda vya ndani kutaongeza mauzo ya nje ya Nchi, kutaongeza ajira na kuongeza mzunguko wa pesa nchini. Yote hayo, yana connection na wizara ya Fedha, Haya Mawazo ya kuuza umeme nje ya Nchi yanatoka wapi!!
Kuinua Uchumi wa Nchi ni kubadili mtizamo wa kukopa Kila kukicha. Jambo Hilo ,Mwigulu limemshinda, hivyo mtu sahihi ni kukaa nafasi hiyo ni Mh Kimei.
Waziri Mwigulu ameshindwa kuhakikisha nchi inapata pesa za kigeni za kutosha Kwa kuimarisha Exportation ya bidhaa za ndani Kwa kushindwa kuweka mazingira mazuri ya biashara, Badala yake nchi yetu inageuka gulio la bidhaa Toka china ambalo linachangia pakubwa kukosekana Kwa pesa za kigeni.
Ni Imani yangu Waziri Mwigulu hajaota mizizi, hivyo naamini ni Rahisi tu kuondolewa na kuwekwa mwingine.
Ni mengi ya kusema, lakini itoshe kusema, Mwigulu Nchemba imetosha sasa!!
Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿
Karibuni 🙏