Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Bila shaka mheshimiwa Masauni waziri wa mambo ya ndani umepata ujumbe kwamba hali ya usalama wa raia si nzuri.
Jukumu la kwanza kabisa la serikali ni kulinda raia wake na mali zao na wizara ya mambo ya ndani ndo yenye jukumu hilo na pia kuhakikisha ulinzi wa raia wake na mstakabali wa uchumi wa nchi upo sawa.
Wizara ya mambo ya ndani kupitia idara yake ya jeshi la polisi lina wajibu wa kuzuia au kuondoa uhalifu na kuwahakikishia raia wake kwamba wapo salama wao pamoja na mali zao.
Waziri ana wajibu wa kuhakikisha polisi watenda majukumu yao kwa ueledi, nidhamu na hawaonei raia bali kupata imani kwa raia hao kwamba jeshi hilo lawajali na pia lipo pamoja nao.
Nchi ikilindimwa na majanga kama haya ya utekaji, utesaji na uuaji wa raia wake pasipo kukamatwa kwa wahusika jambo hilo huzusha tafrani, hofu, mashaka na sintofahamu kubwa. Mwishowe hali ya wanachi kisiasa, kijamii, kisaikolojia na kiuchumi huathirika kwani raia hujawa hofu ya kwenda kwenye shughuli zao za kila siku kwa kuhofia kutekwa na kuishia kuuawa.
Kwa matukio haya ya utekaji, utesaji na mauaji ya watanzania wenzako wapaswa kujitafakari sana hali ni mbaya.
Hata kama watekaji, watesaji na wauaji ni majambazi na wahuni wengine, bado jeshi la polisi lisingechukua muda ulopita kabla haijawakamata wahusika na kuwafikisha kwenye mikono ya sheria.
Hadi sasa waziri Masauni umeshindwa kulisimamia kiuweledi jeshi la polisi lifanye kazi yake ipasavyo ya kuwatambua, kuwakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wahusika wote wanoleta madhila haya kwa wananchi wenzao.
Kama kipindi cha huko nyuma jeshi la polisi liliomba msaada wa JWTZ kushughulikia tatizo la Kibiti, basi huu ni wakati mwingine tena wa kufanya hivyo.
Wananchi wameingiwa sana na hofu kwamba mtu aweza fuatiliwa akikata tiketi, akipanda basi kwenda safari na kuishia kuteremshwa mahala kisha kupotezwa na baadae mwili wake kukutwa umetupwa kama mzoga.
Mheshimiwa waziri wapaswa kujiuliza kwanini sasa hivi ndo matukio haya yameshika tama? Je, tatizo ni nini na kwanini wanachama wa Chadema pekee ndo wahanga?
Pia Je, ni jambo lipo watu hawa wanotekwa la kuhatarisha usalama wa taifa wamelitenda?
Kwa mtazamo wangu, nimebaini kuwa ni ważi kwamba serikali kupitia vyombo vyake vya doła kuna kitu imegundua au kuna mambo ya hatari ambayo watekwaji hawa wameyafanya.
Ukiachila mbali suala la Sativa ambae lengo la watekaji wake lilikuwa ni aliwe na mafisi huko pori la Katavi, lakini hawa akina Soka na wenzie wawili, ni mambo yepi wamerekodiwa wakiyazungumza ambayo yahatarisha usalama wa CCM na serikali yake?
Mapendekezo.
1. Waziri Masauni ajiuzulu na ateuliwe waziri mwingine.
2. Waziri mpya wa mambo ya ndani aunde tume ya uchunguzi na aipe siku 14 kubaini wahusika wa matukio yote likiwemo tukio la Mbeya la wanachama wa Chadema kutekwa na kupigwa vibaya na polisi.
Tume hii pia iwahusishe wawakilishi wa Chadema au mwanasheria wake na pia iwe na mwakilishi wa familia za wahanga wa matukio yanotokea.
3. Kwa kuwa serikali kupitia raisi mwenyewe Samia Hassan imekiri kuwa kuna tatizo mahala, litakuwa jambo la busara kumuondoa mkurugenzi wa makosa ya jinai DCI ili kupisha uchunguzi wa tume.
Ningesema IGP nae aondoke lakini yaonekana tatizo lipo kwenye operesheni ambapo pia yumo mkuu wa operesheni na mafunzo na DCI hivyo ni bora watafutwe watu wengine wanofaa.
4. Kwa kuwa CCM kupitia katibu wake wa Itikadi na uenezi imekiri kuwepo tatizo, litakuwa ni jambo la dharura na uharaka kubaini watu waliomo ndani ya chama ambao kwa namna moja au ingine wahusika na matukio haya ambayo yataiweka Tanzania kundi moja na nchi za Chile au Vietnam na bila kusahau wakati wa utawala wa Adolf Hitler ambapo vikosi mbalimbali vilokuwa vikihusiana na serikali vilikuwa vikiteka watu na watu hao wasipatikane tena.
Watu hawa wakibainika ni lazima wafutwe uanachama na kisha kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
5. Baada ya tume kumaliza uchunguzi wake na ikibainika kuwa vikosi vya serikali vyahusika na matukio haya, serikali iwalipe fidia wale wote ambao wameshurika na matukio haya.
Ni lazima watekaji hawa au watu wasojulikana watambuliwe ili kufahamu ni akina nani na si wahamiaji haramu wanotumiwa kwa kazi chafu au raia wa nchi zingine ambao hadi sasa wameonyesha kiwango cha juu cha ukatili dhidi ya watanzania. Hiyo ni kwasababu imeelezwa kuwa watu hawa huficha sura zao zisitambulike kirahisi na pia huvaa kiraia.
Ni vigumu kuamini kwamba nchi yetu kwa sasa imezalisha watu wasojulikana wenye ukatili wa kutisha.
Isitoshe, haikulikani idadi iso rasmi ya raia wengine wanotekwa na kupotezwa jambo ambalo ni la hatari sana.
Au sasa hivi nchi imegeuka na kuwa Ukraine ambako watu wasombwa tu mitaani na kwenda kupotea kwenye vita na Russia?