Ushauri: Waziri wa Mambo ya Ndani jiuzulu, DCI aondolewe na Rais aunde tume inayojitegemea ifanye uchunguzi wa kina

Kwanini useme waziri awajibike na sio Rais ? Kwanini usishauri Rais ndio awajibike, kwanini humgusi yeye na unaongelea wa chini yake ? Je yeye ni nani ?

. Ili Waziri ajiuzulu, Rais pia awajibike…. Asibaki kuwa mtoa mikeka isiyo na tija yoyote kwenye utendaji , do you think akitoka waziri NDIO hali itabadilika…..?

Why accountability iwe kwa waziri tu na sio kwa huyo aliyemteua…..waziri ndio kateka mtu , hata yeye alipata taarifa baada ya tukio

Unasema Rais huwa hawajui, I think you are out of control ,
Mwalimu did the same , Aliua sana watu , Ben did the same , aliua sana watu, JK did the same , aliua sana watu , Ngosha did the same , aliua sana watu , Samia is doing the same na ni urith wao kutoka kwa mwalimu….. unajidanganya unaposema hawajui…… unahitaji kujifunza positions ya Rais katika nchi

The only president aliyekataa kufa na aibu matakoni mbele ya muumba wake ni Ali Hassan

Hawa wengine ni uzao wa shetani, watatu kati yao walishakufa
 
Waziri wa Tanzania au upo ndotoni
 
My friend, I don't dispute kwamba raisi nae apaswa kuwajibika kwenye hili lakini waziri ambae ana dhamana alopewa na raisi na JMT ni mtu wa kwanza kuwajibika linapotokea jambo au majambo kama haya.

Pia nilisema kwamba raisi huwa hafahamu hili, hapo nikiri kwa mazingira haya huenda ikawa sivyo ninavyowaza lakini naamini kuwa kuna ajenda kubwa nyuma ya matukio haya na moja ya ajenda hizo ni kumharibia kiongozi wa juu kunofanywa na watu wasoridhika na mambo fulanifulani.

Kwa kuwa raisi huwa briefed na waziri Masauni, pamoja na IGP na DCI basi yeye (raisi) apaswa kuwaambia kuwa nafasi zao ni "unattainable" kwamba hawezi kufanya kazi nao.

Akijiuzulu waziri Masauni na DCI akaondolewa pengine pamoja na IGP na ikakundwa tume huru ya uchunguzi kubaini wasojulikana makatili.

Ndo maana hata ubalozi wa Marekani umesisitiza pia kuwepo uchunguzi huru bila kugusia kujiuzulu kwa waziri au raisi maana hiyo hatua weye wafahamu ni ngumu kutekelezwa.
 
Huyu sio Kiongozi wa kwanza kumkuta huko Chadema,kuja kina Wangwe,Mawazo na wale wengine wa Vyama vinginevyo.

Uchunguzi wa Polisi utatoa majibu,Tume ni kupoteza hela
 
Jamaa bado hajaandika barua tu.!?? Aisee .. AFRICA .!!?
 
Huyu sio Kiongozi wa kwanza kumkuta huko Chadema,kuja kina Wangwe,Mawazo na wale wengine wa Vyama vinginevyo.

Uchunguzi wa Polisi utatoa majibu,Tume ni kupoteza hela
Polisi hawawezi kujichunguza wenyewe, maana tumeambiwa walionekana wamebeba silaha na pia matehemu aliingizwa kwenye gari ya Landcruiser hardtop.

Tume si lazima ilipwe kama itahusisha watu waliomo humohumo serikalini kwani watakuwa wakilipwa mshahara uleule.

This is not funny stuff, its serious.
 
Kwenye Kipindi changu chote kwenye Tasnia hii ya habari sikumbuki siku nyingine zaidi ya siku ya Jana ambapo ndipo nilipoona Taifa likisimama pamoja kwa lugha moja na kwa kupaza sauti moja. Sauti iliyokuwa ikisika kutokea pande zote za Nchi ilikuwa, "Haki itendeke kwa Bw. Mohamed Ali Kibao". Mzee Ali alikuwa kiongozi wa CHADEMA, Bahati mbaya kurasa zake za uhai zimefungwa kikatili baada ya Uhai wake kufisadiwa na kuporwa na wale "wasiofahamika", katika hali isiyoweza kusimulika kirahisi.

Leo Jumatatu Mzee Kibao atapumzishwa kwenye makazi yake ya Milele, nyuma akituachia Maswali mengi, hofu, wasiwasi na uoga unaofunikwa na fukuto la kutaka kuona hatua zikichukuliwa kwa wote wanaohusika na tukio hilo la kinyama.

Kauli ya Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoitoa jana jioni kupitia mitandao yake ya kijamii akiagiza mamlaka hususan vyombo vya uchunguzi kumpatia taarifa ya kina kuhusu mauaji ya Mzee Kibao imeamsha hisia nyingine mpya ya kutaka uwajibikaji zaidi miongoni mwa wale wanaoonekana kushindwa kutimiza majukumu yao kikamilifu.

"Nchi yetu ni ya kidemokrasia na kila raia ana haki ya kuishi, serikali ninayoiongoza haivumilii vitendo vua kikatili vya namna hii.", Ujumbe wa Rais ulisomeka.

Wengi wa watumiaji wa mitandao ya kijamii wanaamini kuwa kauli ya Rais Samia haitoshi, ilihali bado Waziri wa mambo ya ndani Hamad Masauni, Mkuu wa Polisi ya Tanzania IGP Camillus Wambura na Kamishna wa operesheni na mafunzo Awadh Jumbe, wote wapo Maofisini. "Wote wajiuzulu kutokana na wimbi la utekaji na mauaji ya raia nchini", wamesema watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii.

Ismail Jussa Mwanachama wa ACT Wazalendo amenukuliwa akisema "Uchunguzi huru wa kimahakama (Independent Judicial Inquiry) tu tena uwe HURU hasa ndiyo unaweza kutupa ukweli kuhusu matukio haya ya utekaji na mauaji yanayoendelea nchini. Na wakati tunasubiri hatua hiyo, hawa wawili (Masauni na Wambura) wanapaswa kuondolewa bila ya kuchelewa kwa kushindwa kazi!"

Mtumiaji wa mtandao wa X aliyejitambulisha kama Luhaga Mpina amechapisha andiko lake akisema, "Tweet hii ( Ya Rais Samia) ingependeza zaidi kama ingeambatana na utenguzi wa mara moja wa Waziri wa Mambo ya Ndani Masauni na IGP Wambura. Watu hawa wanatia doa baya kwenye uongozi wako. Vitendo vya kutekana na kutishana vimetamalaki mno hali inayoleta hofu kwa Watanzania."

Martin Masese naye kupitia ukurasa wake wa X amesema "Kama kweli RAIS @SuluhuSamia angelikuwa ameumizwa na kukereka na tukio la Mzee #AllyMohammedKibao kutekwa, kuteswa, kuuuwawa na kutupwa UNUNIO, tungeona hadi muda huu kuna watu wamewajibishwa akiwepo MASAUNI. Huwezi kuwa WAZIRI wa mambo ya ndani watu wanatekwa na kuuwawa. NO.

Aidha katika hatua nyingine, baadhi ya wananchi wametaka uboreshaji wa mfumo wa utendaji wa Jeshi la Polisi, wakiamini kuwa hatua hiyo ndiyo itakayoiweka Tanzania na Raia wake kuwa salama kwa kuondokana na vitendo vya mateso, udhalilishaji, ukandamiza, mauaji na utekaji unaoonekana kushamiri kwa siku za hivi karibuni.

Bw. Onesmo Mushi, mtumiaji wa Mtandao wa X anasema "Kuwa na independent oversight body mwenendo wa jeshi la polisi nayo ni kupoteza muda tu. Unaoversee nini ili ureport kwa nani afanye nini? As long as tutaendelea kuwa na jeshi linaloapa kutii amri za watawala, haya matukio hayawezi kuisha.

..... So long as tutaendelea kuwa na katiba inayomfanya Rais kuwa Mungu mtu, polisi wataendelea kutumika kulinda dola tu. Hata ukifanya overhaul ya jeshi zima la polisi leo na kuintroduce structure mpya, bila kugusa madaraka ya kimungu aliyopewa Rais ni kazi bure.

Bw. Onesmo amepingana na Kiongozi mstaafu wa Chama cha ACT Wazalendo Bw. Zitto Kabwe ambaye awali alichapisha taarifa yake akisema "Tume huru ya uchunguzi, Presidential Commission of Inquiry, kwa mujibu wa Sheria ndiyo njia sahihi, bora na ya kuaminika kupata ukweli wa tukio hili na mengine kama hili."
 
Bw. Onesmo amepingana na Kiongozi mstaafu wa Chama cha ACT Wazalendo Bw. Zitto Kabwe ambaye awali alichapisha taarifa yake akisema "Tume huru ya uchunguzi, Presidential Commission of Inquiry, kwa mujibu wa Sheria ndiyo njia sahihi, bora na ya kuaminika kupata ukweli wa tukio hili na mengine kama hili."View attachment 3092150
 
Ushauri wa kipumbavu ,ninyi mlikuwa wapi wakati inatengenezwa ile sheria ya kuzuia Hao vibaka wa TISS kushitakiwa mwaka 2023 ?
Wewe unafikiri huu utekaji na mauaji yanayofanyika yanafanywa na watu baki ?
Unadhani hayana maelekezo hayatoki kwa Rais mwenyewe na executive branch yake ?
Unadhani TISS ,Polisi ,Jwtz , magereza nk hawahusiki na huu ushenzi ?
Au hujui kwa kuna task force za mauaji na utekaji na blackmail zikiundwa tangu enzi za Magufuli ? Tena hadi TRA walikuwemo , ile kutaifisha pesa za watu na kufungia accounts zao na kuwapa vitisho watu ?
Wewe unafikiri hili suala lipo juu juu tu ?
 
Amuharibie nini ? Kuna lolote amefanya la maana linaloweza kuharibiwa?

Nchi ipo Kama alivoikuta…… Tena ameenda kuharibu kila kitu

Unaposema kuna mpango wa kumuharibia , ni lipi liharibiwe ambalo amelifanya la maana . Acha Kona Kona be straight
Hana cha kuharibiwa na hakuna mpango wowote. Kutwa yupo angani
Nani anaangalia nchi, Kona Kona nyingi ….. hakuna mpango chochote
Awajibike
 
Tumeona Raisi kawatoa mawaziri wengine kama Ummy, January na Nape na kumwacha waziri ambaye kwa wengi hafanyi kazi vizuri. Mambo kama haya ndiyo yanaleta watu kufikiri upendeleo kwa Wanzanzibari
 
Kujiuzulu kwake kutazuia watu kutekwa??
mawaziri wangapi wamekuja na kuondoka na hayo mambo bado yapo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…