Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
HUNA HAKI YA KUPATA CHOCHOTE mkuu Tena ningekuwa ndo huyo Mzee wako NINGEKUTIMULIA MBALI!!! ACHA TAMAA KWA MALI ZISIZO ZAKO!!!Hapana mkuu mimi sina shida yeyote, pale ni kwetu mkuu na nina haki ya kupata mgao sawa sawa
Maoni yetu Ni KATAFUTE MALI ZA KWAKO USIMKERE MZEE WA WATU NA GUBU LAKO LA TAMAA KWA MALI ZISIZO KUHUSUUUUI!!!!Habarini ndugu zangu, poleni na majukumu ya kazi, naombeni ushauri wenu maana nimeshikwa na gadhabu sana tangu siku ya jana.
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 39, na kwetu tumezaliwa watatu tu mimi nikiwa wa kwanza, elimu yangu ni degree 1, baada ya kumaliza chuo na kukosa ajira nikawa tu nyumbani kusikilizia mishe kama itatokea, kulitokea kutokuelewana na mzee wangu (hii nilishaielezea humu humu, baba hakutaka kabisa nimuambie mambo ya kujiunga na chama changu cha mapinduzi), akanitimua nyumbani, nikaenda kuishi kwa rafiki yangu huku maisha yakiwa magumu kweli kweli sijapata kushuhudia
Basi siku ya juzi nilimpigia simu mama kumuambia sijala nina siku ya 2, mama yangu alilia sana, nikamuomba aniombee msamaha kwa baba ili niweze kurudi kuishi kpale kwetu ila la kushangaza mama alipomuambia baba, mzee alikataa kabisa kuniona, ikabidi niende home jana kwa kulazimisha nimefika getini nikagonga alikuja mlinzi kunifungulia, alipo niona ni mimi akasema baba amesema asione uso wangu kwenye ile nyumba, nikamuambia nimerudi na hapa ni kwetu, kumbe muda huo baba anaangalia dirishani, alipo niona akatoka nje akiwa na nyundo, akaniambia nimeshakuwa mtu mzima asione kabisa pale, niliumia sana ndugu zangu, nikaona kama baba yangu amefikia kuwa na roho ya kinyama na kikatili wakati mimi pale ni kwetu, kukatokea mabishano makali sana siku ya jana.
Baada ya mabishano ya kama dk tatu sikuamini masikio na maneno ya baba yangu, alisema hivi: "wewe mbwa sikutambui, haujielewi mbwa mkubwa wewe, ndio maana kwenye urithi wangu sijakuweka na mwezi huu wa sita nauza mali zangu nawagawia ndugu zako sehemu ya pesa wakaendeleze maisha yao huko walipo" wakuu hii kauli imeniuma mnoo
Wakuu naombeni ushauri wenu, huyu mzee nataka nikamshtaki mahakamani maana mimi ni mtoto wake mkubwa na tumefanana mnooo. Mimi nilipaswa nikabidhiwa sehemu ya mali, wakuu sipati usingizi kabisa, nahisi kuchanganyikiwa kabisa, huyu mzee nataka akakae hata jela miezi mitatu ili aweze kuona uchungu wa kugawa mali kwa upendeleo
Kuna rafiki yangu alinipa option ya kwenda kwa mganga wa kienyeji ili niweze kumkamata mzee kila nitakachoongea aweze kukubaliana na mimi
Nachukua kwanza maoni yenu wakuu.
Karibuni.
Dah! SaanaaaAnatia aibu sana.
Wewe ungekua Ni mti, Basi ungekua mpapai wa kiume.
Yaani haufai popote hata kwa gogo la choo.
😡😡😡😡😡😡 huna mgao pale. Kwani umeambiwa mali za baba yako ni za kugawa kana kwamba hazina m wenyewe? Mwenye nacho huongezewa. Hao ndugu zako kama wameishajitafutia wataongezewa nawe utabaki na kijiba cha roho. Pia angalia maoni ya wengi hapa. Utajua la maana la kufanya.Hapana mkuu mimi sina shida yeyote, pale ni kwetu mkuu na nina haki ya kupata mgao sawa sawa
KATAFUTE MALI ZA KWAKO!Sio kwamba nalia, naomba ushauri wakuu
HAKUNA Cha maisha tu! Na wale wa mitaani wenye chini ya miaka 18 wakalilie wapi we jamaa acha uvivu wa KUFIKIRI.KAVUNJE HATA MAWE HUKO UONE UGUMU WA KUTAFUTA MALI!ni maisha tu mkuu
Tafuta chako,kukusaidia. Muombe akupe mtaji.Sio kwamba nalia, naomba ushauri wakuu
Jasho lako lipi?tafuta mali zako,huyo Dingo akiuza zake ni sawa tumkuu uyu mzee sasaivi nahisi ametawaliwa na roho mbaya sana, nataka nipate na mimi maali siwezi kubali jasho langu lipotee mkuu.
Baba yako ni kichwa ila kaona amezaa zuzu ndio maana kakutimua kutokana na mbanga zako za kutaka kujiunga na CCM kisa hauna ajira nyinyi ndio watu mkipewa nafasi hamtumii taaluma yenu ila mnaangalia kulinda matumbo yenu kaka profesa majalala, kudos mshua boi🤣🤣kwanza, elimu yangu ni degree 1, baada ya kumaliza chuo na kukosa ajira nikawa tu nyumbani kusikilizia mishe kama itatokea, kulitokea kutokuelewana na mzee wangu (hii nilishaielezea humu humu, baba hakutaka kabisa nimuambie mambo ya kujiunga na chama changu cha mapinduzi), akanitimua nyumbani,
alafu anasema mimi nikijana wa miaka 39...Sema mie ni mbaba...unatakiwa ungekuwa na mtoto wa miaka 19...kama ungekuwa fasta..na huyu mtoto wa miaka 19 anagekuwa na mtoto wa mwaka mmoja...So wewe ni babu. Wenzio eji ya secondary...tulisepa kimoja home...Miaka 39 bado unakaa nyumbani, kwanza shida ya kwanza ni wewe