Ushauri wenu: Baba anataka kuuza mali, hataki kunigawia mimi mwanae

Popote alipo baba yako mwambie anywe balimi 3 malipo kwangu. Baba kama huyu ndio mzazi bora kabisa mwaka huu
 
Mwambie mzee pale ni kwa wazazi wako, yeye ndio anatakiwa atoke aende kwa wazazi wake. Kama hawakumtafutia Cha kurithi ajijue anaanzaje maisha[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Acha auzee, ale na mkewe, mzee baba tafuta zakoo! African family succession plan kwenye issue za biashara na mali hakunaga, kwa sababu ya uselfishii.

Mzee toka hapo nenda mkoa mwingine katafute maisha ila wewe usije kuwafanyia watoto wako.
 
Mwakani una 40 unatakiwa uanze kumlea babako kwani na wewe tayari uzee umeanza.
Pengine umejua kwanini babako kachukia wewe kujiunga ccm?
Ukijua hili maisha yako yatabadilika mara moja japo umechelewa kidogo.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Wewe ungekua Ni mti, Basi ungekua mpapai wa kiume.
Yaani haufai popote hata kwa gogo la choo.
 
Habarini ndugu zangu, poleni na majukumu ya kazi, naombeni ushauri wenu maana nimeshikwa na gadhabu sana tangu siku ya jana.

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 39, na kwetu tumezaliwa watatu tu mimi nikiwa wa kwanza, elimu yangu ni degree 1, baada ya kumaliza chuo na kukosa ajira nikawa tu nyumbani kusikilizia mishe kama itatokea, kulitokea kutokuelewana na mzee wangu (hii nilishaielezea humu humu, baba hakutaka kabisa nimuambie mambo ya kujiunga na chama changu cha mapinduzi), akanitimua nyumbani, nikaenda kuishi kwa rafiki yangu huku maisha yakiwa magumu kweli kweli sijapata kushuhudia

Basi siku ya juzi nilimpigia simu mama kumuambia sijala nina siku ya 2, mama yangu alilia sana, nikamuomba aniombee msamaha kwa baba ili niweze kurudi kuishi kpale kwetu ila la kushangaza mama alipomuambia baba, mzee alikataa kabisa kuniona, ikabidi niende home jana kwa kulazimisha nimefika getini nikagonga alikuja mlinzi kunifungulia, alipo niona ni mimi akasema baba amesema asione uso wangu kwenye ile nyumba, nikamuambia nimerudi na hapa ni kwetu, kumbe muda huo baba anaangalia dirishani, alipo niona akatoka nje akiwa na nyundo, akaniambia nimeshakuwa mtu mzima asione kabisa pale, niliumia sana ndugu zangu, nikaona kama baba yangu amefikia kuwa na roho ya kinyama na kikatili wakati mimi pale ni kwetu, kukatokea mabishano makali sana siku ya jana.

Baada ya mabishano ya kama dk tatu sikuamini masikio na maneno ya baba yangu, alisema hivi: "wewe mbwa sikutambui, haujielewi mbwa mkubwa wewe, ndio maana kwenye urithi wangu sijakuweka na mwezi huu wa sita nauza mali zangu nawagawia ndugu zako sehemu ya pesa wakaendeleze maisha yao huko walipo" wakuu hii kauli imeniuma mnoo

Wakuu naombeni ushauri wenu, huyu mzee nataka nikamshtaki mahakamani maana mimi ni mtoto wake mkubwa na tumefanana mnooo. Mimi nilipaswa nikabidhiwa sehemu ya mali, wakuu sipati usingizi kabisa, nahisi kuchanganyikiwa kabisa, huyu mzee nataka akakae hata jela miezi mitatu ili aweze kuona uchungu wa kugawa mali kwa upendeleo

Kuna rafiki yangu alinipa option ya kwenda kwa mganga wa kienyeji ili niweze kumkamata mzee kila nitakachoongea aweze kukubaliana na mimi

Nachukua kwanza maoni yenu wakuu.

Karibuni.
Wewe bado una akili za chekechea miaka 36 unalalamika ungekuwa huna baba na mama ungeishije?
Unapaswa utambue kuwa wewe kwa Sasa maada baba yu hai huna haki ya kurithi chochote. Unaitwa mrithi na kuwa na haki ya madai yoyote ikiwa mzazi wako amekufa period.
 
Miaka 39??? Mkuu unaweza ukawa unaleta masikhiara humu, sidhani kama kuna binadamu mwenye umri huo anaweza akawa na akili kama hizo ulizozielezea...! Kama ni kweli basi mkuu una safari ndeeefu mno humu duniani na akhera
 
Badala mnishauri kwa mawazo mazuri kila mmoja ananishambulia kwa maneno makali, roho mbaya zitawahuwa, mnaona nikipata ulisi ntawapita kimaendeleo
 
Hauna hiyo haki, hizo ni mali za wazazi wako na wanaweza kuzigawa wanavyotaka.
Katafute mali zako.
Hapana mkuu mimi sina shida yeyote, pale ni kwetu mkuu na nina haki ya kupata mgao sawa sawa
 
Badala mnishauri kwa mawazo mazuri kila mmoja ananishambulia kwa maneno makali, roho mbaya zitawahuwa, mnaona nikipata ulisi ntawapita kimaendeleo
Haahaaahaaaaaaa...
We kweli "kikohozi"!.
 
Labda mganga ampooze! Mali ni ya baba anaamua ampe nani! Mahakamani utaambiwa "mali mlitafuta pamoja na baba? Kama sivyo tafuta chako
 
muache auze, ila akimaliza hatutaki ya kina DIAMOND NA BABA YAKE
 
Habarini ndugu zangu, poleni na majukumu ya kazi, naombeni ushauri wenu maana nimeshikwa na gadhabu sana tangu siku ya jana.

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 39, na kwetu tumezaliwa watatu tu mimi nikiwa wa kwanza, elimu yangu ni degree 1, baada ya kumaliza chuo na kukosa ajira nikawa tu nyumbani kusikilizia mishe kama itatokea, kulitokea kutokuelewana na mzee wangu (hii nilishaielezea humu humu, baba hakutaka kabisa nimuambie mambo ya kujiunga na chama changu cha mapinduzi), akanitimua nyumbani, nikaenda kuishi kwa rafiki yangu huku maisha yakiwa magumu kweli kweli sijapata kushuhudia

Basi siku ya juzi nilimpigia simu mama kumuambia sijala nina siku ya 2, mama yangu alilia sana, nikamuomba aniombee msamaha kwa baba ili niweze kurudi kuishi kpale kwetu ila la kushangaza mama alipomuambia baba, mzee alikataa kabisa kuniona, ikabidi niende home jana kwa kulazimisha nimefika getini nikagonga alikuja mlinzi kunifungulia, alipo niona ni mimi akasema baba amesema asione uso wangu kwenye ile nyumba, nikamuambia nimerudi na hapa ni kwetu, kumbe muda huo baba anaangalia dirishani, alipo niona akatoka nje akiwa na nyundo, akaniambia nimeshakuwa mtu mzima asione kabisa pale, niliumia sana ndugu zangu, nikaona kama baba yangu amefikia kuwa na roho ya kinyama na kikatili wakati mimi pale ni kwetu, kukatokea mabishano makali sana siku ya jana.

Baada ya mabishano ya kama dk tatu sikuamini masikio na maneno ya baba yangu, alisema hivi: "wewe mbwa sikutambui, haujielewi mbwa mkubwa wewe, ndio maana kwenye urithi wangu sijakuweka na mwezi huu wa sita nauza mali zangu nawagawia ndugu zako sehemu ya pesa wakaendeleze maisha yao huko walipo" wakuu hii kauli imeniuma mnoo

Wakuu naombeni ushauri wenu, huyu mzee nataka nikamshtaki mahakamani maana mimi ni mtoto wake mkubwa na tumefanana mnooo. Mimi nilipaswa nikabidhiwa sehemu ya mali, wakuu sipati usingizi kabisa, nahisi kuchanganyikiwa kabisa, huyu mzee nataka akakae hata jela miezi mitatu ili aweze kuona uchungu wa kugawa mali kwa upendeleo

Kuna rafiki yangu alinipa option ya kwenda kwa mganga wa kienyeji ili niweze kumkamata mzee kila nitakachoongea aweze kukubaliana na mimi

Nachukua kwanza maoni yenu wakuu.

Karibuni.
Dogo acha ujinga pambana upate mali zako.
Hizo ni mali zake ana haki ya kukunyima
 
Back
Top Bottom