Ushauri wenu: Nataka kujenga frame ya biashara kwa mkataba

Ushauri wenu: Nataka kujenga frame ya biashara kwa mkataba

Kv-london

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2014
Posts
2,877
Reaction score
5,022
Habar wakuu huku ndani,

Hapa kijijini kwetu Moshi kuna eneo zuri potential kwa ajili ya biashara hasa ya duka la reja reja, hardware au site ya tofali za block wamiliki wa hili eneo ni chama cha ushirika wa kahawa KNCU.

Changamoto iliyopo ni kuwa hamna frame yeyote ya kufanya hiyo biashara ni eneo tu la wazi, kuna wamama wanalima hapo mboga mboga tu for free at a zero cost.

Ninachotaka mnishauri ni hivi; ninawazo la kuomba na kuingiza nao mkataba nijenge hapo frame 🪟 za biashara then baada ya kuanza operation tuanze kukatana kwenye Kodi.

Naombeni ushauri wenu kwenye hili, na kama kuna mtu alishawahi fanya contract kama hii pia naomba ABC.

Pia naomba mtu ambaye atakuwa na mfano wa copy ya mkataba anisaidie Ili niufanyie editing iendane na mazingira yangu.

Ahsante kwa msaada wenu.
 
Piga hesabu uwekezaji wako utagharimu kiasi gani?
Piga hesabu hapo kodi kwa mwezi itakuwa kiasi gani?
Hapo utapata muda wa mkataba,

Ni mikataba mizuri mkielewana, inasaidia kiendeleza eneo,
Ila cha kwanza waone hao viongozi wa ushirika wakupe maelezo ya kina
 
Ahsante mkuu
Piga hesabu uwekezaji wako utagharimu kiasi gani?
Piga hesabu hapo kodi kwa mwezi itakuwa kiasi gani?
Hapo utapata muda wa mkataba,

Ni mikataba mizuri mkielewana, inasaidia kiendeleza eneo,
Ila cha kwanza waone hao viongozi wa ushirika wakupe maelezo ya kina
Vp unaweza kuwa na copy ya related issue kama hii Ili nione naweza vp kuingia makubaliano nao?
 
Wazo Jema.Fanya homework ya Hesabu
1.Wapangaji wanaweza Kulipa bei gani Kwa frame (au SQM Kwa Mwezi)?
2.Gharama za Kujenga SQM ni ngapi?-Hapo mnatumia materials gani Kujenga?Ni Misingi ya Mawe au Tofali?Matofali yanapatikana?Ya Aina gani?Vifaa vya ujenzi Vipo?Mafundi Makini wapo?Designers wapo?
Hizi hesabu zitakusaidia kunegotiate terms na wamilki wa Ardhi.Mkakubaliana Miaka 5 Hadi 10.Hizi hesabu ndiyo Msingi wa Mkataba.Gharama Kujenga SQM 1 ina range Kati ya 250K Hadi 500K Kwa TZ kutegemeana na Eneo.
Mfano:Miaka ya 2000 wenyeji wengi wa Karikaoo walikuwa na zile Nyumba zao za kizamani Katika Eneo lenye Thamani lakini hawana Pesa wala Maarifa.Wakaja investors,wakawa wanakubaliana terms za 40:60 au 30:70
Yaani developer (Kama Wewe) anajenga Jengo la floor 5 au 10.Developer anachukua floor Kadhaa na Mwenye Ardhi anapewa zingine.Baada ya Miaka 10 Jengo linarudi Kwa Mwenye Ardhi.
Kwa hiyo hapo ulipo piga Kwanza hesabu kabla ya Kukutana na Mmilki wa Ardhi.
 
Back
Top Bottom