Kitu ambacho kinanishangaza sana kuhusina na hawa wanawake, yani unaona kabisa kuna utofauti lakini ukimuuliza anaweza kataa kabisa, sijui ni kitu kinawafanya washindwe kuongea ukweli maisha yaendelee. Brother pole sana, ninavyoona kama msichana akiweza kua na mahusiano na watu wawili kwa wakati mmoja, sidhani kama atakuja badilika. Kuna maamuzi mawili;
1. kama unataka kuujua ukweli, mana inaonyesha bado kuna kaupendo flani kwake, unaweza mpa mda na ukajipa mda ili uone kama bado yeye ni yule yule ulikua nae. unajua kuna mda unaweza sema ngoja niame kumbe ndio ile unaruka mkojo unakanyaga 💩 .
2. kama moyo ushapondeka sana, fanya a wise decision kuendeleza maisha yako, hua naamini kuna wasichana wapo wengi na wazuri sana na werevu wanakusubiri, kama wewe uko na moyo mmoja wa kutulia.
Mapenzi yanahitaji mda sana ambao sisi vijana wa sikuizi hatuna.