Mimi ni Mama wa mtoto mmoja, sijaolewa ila nina kazi yangu nzuri tu ni Mhasibu katika Halmashauri moja hivi, kipato changu ni kizuri tena sana. Kuna mwanaume niko naye huu ni mwaka wapili ananipenda na mimi nampenda. Yeye naye ni mfanayakzi lakini katika kampuni binafsi.
Kikipato namzidi hilo kwangu si tatizo, shida nikuwa, tangu kuwa naye kwenye mahusiano hajawahi kunipeleka kwake hata kwa bahati mbaya, kila sikua anakuja kwangu na nikimuambia mambo ya kunipeleka kwake ananiambia muda bado mpaka tujuane vizuri.
Sijui chochote kuhusu yeye ila ananiambia hajaoa, kuna rafiki yake mmoja tu ndiyo kanitambulisha kwake na mdogo wake wakike, wote wananiambia kuwa bado hajaoa. Sasa shida nikuwa, kuna kipindi mwaka jana mwishoni nilikua naangalia kwenye simu nikakuta kapiga picha ya vyeti vya ndoa ambavyo vina majina yake, nikamuuliza vipi mbona kama una ndoa akanijibu achana na mambo ya picha utachanganyikiwa.
Basi mimi nilikaa kimya kwani lainihakikishia kuwa ni picha tu lakini hajaoa. Lakini miezi miwili iliyopita nilikua kwenye mtandao, mara nikakuta kuna mwanamke kampost, kaandika maneno mengi sijui wewe ndiyo maisha yangu, pumzi yangu na mambo kibao kumsifia huyo mwanamke.
Wamepiga naye picha nyingi tu yaani zile za studio, maeneo mbalimbali na ni kama anampost mara kwa mara kama wana familia. Mimi kwenye hiyo akaunti ameniblock ila hajui kama nina akaunti nyingine fekero naitumia kufuatilia umbea.
Nimemuuliza ananiambia kwani unakosa nini si nakuridhisha achana na mitandao. Hajawahi kunipa hata shilingi kumi mimi ndiyo nampa kwani ana kipato kizuri ila nimemzidi, namsaidia sana kama mume wangu ila nina hofu, hivi anaweza kuwa ni mume wa mtu kweli ananidanganya, nashindwa kuelewa kwani kila nikimuuliza ananikatalia!