Ushauri: Wilaya za Kibaha na Bagamoyo zihamishiwe Dar es Salaam, Mbagala na Kigamboni zipelekwe mkoa wa Pwani

Tuliza munkari kwanza ndugu yangu,mawazo ya mtu mmoja hayawezi kuwa sheria,ni vizuri na wewe ukatoa mapendekezo yako,ila kiukweli mkoa wa pwani kijiografia unatesa wakazi wake wa wilaya za kusini ,rufiji,kilwa nk wanapofuata hiuduma kibaha
Hakika wanahitaji kufanyike kitu
Toa maoni yako nini kifanyike kuwasaifia watu hawa
 
Kwanza kilwa haipo kati ya wilaya zilizopo mkoa wa pwani.
Kufanana kwao tamaduni kati ya Wamatumbi na Wandengereko hakufanyi wawe sehemu Moja kiutawala.
Kilwa ni wilaya iliyopo Kaskazini zaidi katika mkoa wa Lindi hivyo kuwapa tabu wakazi kwenda Lindi mjini kupata huduma.

Kuna ukweli wa wakazi wa Wilaya za mkuranga, Kibiti, Rufiji na Mafia yenye visiwa kama jaja, kwake, koma na Mafia yenyewe kupata shida kwenda Mkoani ambapo ni kibaha.

Ila ukweli mwingine watu kutoka wilaya ya kisarawe, Bagamoyo pia hupata shida kwenda makao makuu ya mkoa kupata huduma kwa sababu miundombinu sio rafiki.

Kwa nini? Kwa sababu Mzizima ilizaliwa kwa kukataa eneo la mkoa wa pwani lililoendelea zaidi ambalo lipo kati kati hivyo kuwapa shida watu wa Wilaya hizo kutoka wilaya Moja kwenda nyingine lazima wapite Mzizima.
Tatizo hili pia utalikuta Mbeya maana mbeya mjini imezungukwa na mbeya vijijini

Nini kifanyike? Anzisha Metropolis itakayo jumuisha hayo maeneo ambayo yapo integrated na Dar es Salaam ambayo nadhani itakuwa biggest and largest Metropolicies katika afrika.

Kwa sababu kiuchumi hayo maeneo yapo dependent kwa Dar es salaam.

Je issue ya kutengeneza mkoa mpya ipo viable endapo makao makuu yakiwekwa yakiwa kilwa ila utamlazimisha mtu wa Kisenvule kusafiri zaidi ya kilometer 300 kwenda makao yapya makuu ambao hata kutoka dar mpaka morogoro ni kilometer 200 chaguo ni lako wenye maamuzi.

Kwa nini usitengenezwe mkoa mpya wa kuzihusisha wilaya za Mkuranga, Kibiti, Rufiji na Mafia na ikaitwa Mzizima. Ambayo makao yake makuu yatakuwa Kibiti ila hii itakuwa ni kuongeza gharama za serikari, najua wengi watataka mkuranga kwa sababu ni karibu Mbagala.

Wilaya ya kilwa ni wilaya kubwa katika mkoa wa Lindi
 
Uko sahihi kuasi ila ukitengeneza mkoa mpya wenye wilaya za kibiti rufiji,mafia na mkuranga,huu utakuwa mkoa masikini sana Tanzania,hizo wilaya kubaki kataa uchumi wake uko chini sana.ndio maana ikapendekezwa mbagala na sehemu ya kigamboni iwe sehemu ya huo mkoa mpya
 
Tatizo mliwahi kuambiwa na wanasiasa kuwa ukubwa /udogo wa eneo la mkoa linadumaza ama linachochea maendeleo.

Hii kauli si kweli......
 
Kwahiyo mtu akitoka Mbagala au Kigamboni ambako utakua ni mkoa wa pwani na anata kwenda Chalinze kwenye mkoa wake huo huo bado itamlazimu kupitia mkoani Dar, right?? Then unakua umefanya nini? Mi kwa mtazamo wangu, mkoa wote wa pwani hasa wilaya za Bagamoyo, Kibaha, Chalinze zingeingia Dar tu, baadhi ya maeneo ya Kilwa yapelekwe Lindi au laa na yenyewe yaje Dar tu
 
Nilibidi nigoogle kujua GDP ya kila wilaya ,
Idadi ya wakazi wake,
Ukubwa wa kila wilaya
Kujua mikoa na wilaya masikini Tanzania.

Mkoa mzima wa pwani una wakazi wasiopungia Milioni Moja.

Hivyo bado Tanzania Kuna mikoa na wilaya masikini zaidi na hazijawa dissolved kwa sababu hakuna economic potential.

Pili: kwa miaka 8 au 9 Kuna viwanda vingi vilivyoanzishwa mkuranga kiasi kwa takwimu 2020/2021 haziwezi kuwa masikini

Tatu: hizi wilaya zote zote na kibaha zipo ohe ahe kiuchumi, usichanganyikiwe na kibaha mjini pale ingia mbwinde huko utajionea.

Kwa hiyo issue ya umasikini hakuna wilaya iliyo na afadhali.

Nne: Uanzishwaji wa Wilaya mpya huwa unategemea tu economic output pekee basi tusingeanzisha wilaya ya mkalama kule singida.

Tano: Hebu angalia hiyo ramani vizuri halafu nipe economic potential ya kibaha na Bagamoyo ilioishinda Mkuranga na Rufiji.

Sababu yako sioni kama Ina mashiko
 
Kinachotokea hakuna miundombinu ya kutosha ila huwezi sema unaipeleka huko uliposema.

Angalia hiyo ramani unafikiri shida ni nini?
 
Kinachotokea hakuna miundombinu ya kutosha ila huwezi sema unaipeleka huko uliposema.

Angalia hiyo ramani unafikiri shida ni nini?View attachment 2136306
Sasa hata wewe fikiria hadi kina mzee Mpiri na wenyewe wanajiijia tu Dar watakavyo; you know why? Watu wa mkoa wa pwani by nature hawaitofautishi Dar na mkoa wao, hu mkoa ungevunjwa tu na kuirudisha MZIZIMA bwana
 
Pwani na Dar zinatakiwa ziwe mkoa mmoja
 
Hapo ukitoa kibaha,bagamoyo na kisarawe unabaki na watu laki nne???angalia data zako😀😀😀laki nne hao unaweza kuwapata mbagala peke yake
 
Sasa hata wewe fikiria hadi kina mzee Mpiri na wenyewe wanajiijia tu Dar watakavyo; you know why? Watu wa mkoa wa pwani by nature hawaitofautishi Dar na mkoa wao, hu mkoa ungevunjwa tu na kuirudisha MZIZIMA bwana
Ya tukiwa huku vijijini kwetu hatusemi tunaenda dar ila tunaenda mjini
Kwa maana sehemu ya mkoa iliyoendelea zaidi
Hata kila Kijiji mkoani pwani Kuna mjini kwake
 
Hapo ukitoa kibaha,bagamoyo na kisarawe unabaki na watu laki nne???angalia data zako[emoji3][emoji3][emoji3]laki nne hao unaweza kuwapata mbagala peke yake
Unafanya nisijue tunacho bishania ila naheshimu hoja zako.

Wilaya ya kilwa Ina watu 190,000 peke, pamoja na ukubwa wote ilionao hivyo kuiunganisha na mkuranga Bado hujatatua.

Dar Es Salaam Ina wakazi Milioni sita mpaka Saba hivi yaani Ina zaidi ya asilimia kumi ya idadi ya watu Tanzania nzima.

Mbagala ndio Jimbo linaloongoza kwa idadi ya watu Dar es Salaam yote ikifuatiwa na Jimbo la ukonga
Chamazi ndio kata inayoongoza kwa idadi kubwa ya watu kuliko kata yoyote iliyokuwa ndani ya mkoa wa Dar es salaam ikifuatiwa na kata ya Msongola ilala

Mbagala ukiitoa nje ya Dar es Salaam inajisimamia yenye na kuwa na Mamlaka ya jiji kwa vigezo vyetu.

Inasadikika Mbagala Ina zaidi ya wakazi Milioni Mbili na zaidi

Lakini Kigamboni na gongo la mboto au Mkuranga inaweza kuipita Mbagala kwa sababu Mbagala imeshajaa labda iongozewe maeneo kutoka mkuranga kama watu wanavyo taka Yale Yale ya kutaka maeneo yaliyoendelea kutoka mkuranga yaletwe dar es salaam

Napendekeza Lile Lile kuanzishwe Metropolis ndio dawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…