Ushawahi kuchukuliwa poa na mtu halafu akakuta sivyo kama alivyokudhania?

Aiseee...!
Umenikumbusha mkasa mzuri tena wa zamani kidogo.

Ni mkasa wa kweli wa umfikiriaye ni mswahili wa low class, kumbe miaka ikipita ndo anakuwa matawi ya juu.

Kulikuwa na dame, mzuri sana , miguu ya kupendeza figure eight na kwa kweli kila nikimuona moyo waenda mbio.
Na alikuwa ni cheusi mangala, super black, akicheka meno meupee ya kuvutia, juu ni afro zuri natural, hadi leo hii.
Wazazi wake nilikuwa nawafahamu, nivyo nikaona itakuwa rahisi kukubalika.
Ndo kwanza miaka hiyo nimemaliza Form six, dame anaelekea kumaliza form IV.

Sasa nikawa nimepata kibarua cha ukarani benki, hivyo vijisenti vya kununua soda sikosi.
Nikamwaga sera kwa dame yule.
Yeye akawa kama ananihurumia tu, maana anaona nampenda sana lakini anashindwa kuwa muwazi.
Miezi ikapita mingi tu, tuna date na kila tukionana naona hakuna maendeleo, hadi dada zangu wakaanza kunihurumia pia, penzi linavyonitesa.

Mwisho yule dame akaniambia wazi, we bwana si saizi yangu, kwanza watoka Uswazi.
Akaniambia nina mchumba mtoto wa balozi fulani, famous hapa mjini.
Na wazazi wa yule dame walilielewa hilo, kulingana na dame mzuri.

Basi sikukata tamaa, nilijahidi kumweleza dame wangu huyu kuwa mimi haipiti miaka miwili nitaingia chuo kikuu na nikimaliza sitakosa noti ndefu kukutunza wewe na familia, nikubalie tu.
Dame akakataa kata kata.

Siku aliyohitimisha maneno ya kunikataa niliugua, tena homa kali na ya kweli kabisa.
Sikujua kuwa penzi literaly ni homa ya moyo!
Nilinyong’onyea na kulala kitandani siku mbili.

Ile homa naikumbuka vizuri sana.
Slowly homa iliondoa na kukausha upendo wote kwa yule dada.
Nilistaajabu hata mimi kwani nikajiuliza , kwa nini niteseke?
Na kwa muda mrefu sikutafuta tena msichana mwingine awe girlfriend wangu wa kudumu, ile homa iliniumiza ifikra.

Miaka ikapita, na kweli nikaenda UDSM, na kukamilisha kadigilii kangu na kazi nzuri nikapata.
Kazi nikaendelea kupata nzuri zaidi, kumbe yule dame, cheusi mangala, ananifuatilia kwa mbaali.

Miaka mingi ikapita, na mambo yangu alhamdulilhi yakawa si mabaya sana.
Wakati huo ikawa nimepata fiancee kwa kweli mzuri sana, tena half caste.


Huku nyuma dame cheusi akajileta, na tukala mzigo.
Aliponiuliza itakuwaje sasa, nikamwambia tu ukweli kuwa naoa miezi michache ijayo, ile chance haikuwa yetu.
Alilia sana yule dame mzuri.

Mbaya zaidi mie kikazi nikawa matawi ya juu sana, kama nilivyomuahidi dame cheusi nilipokuwa namtongoza na akakataa.
Sikumuuliza imekuwaje na yule mtoto wa balozi, maana sikuona kama yananihusu.
Dame cheusi mangala bado ni mzuri na akajaolewa na classmate wangu.

UPDATE:
Tunaandika hadithi ambazo ni za ukweli kabisa.
Cheusi Mngala baadaye niliambiwa mume wake alikuja fariki kwa ugonjwa wa sukari.
Ingawaje wengi tuihisi ni kale kaugonjwa kanako sumbua.
Kilichonishtua majuzi ni kuambiwa Cheusi Mangala naye kafariki, nilivyompenda nililia!
 
Mimi kwangu ni tofauti kidogo kwani watu wengi hunichukulia kama mtu mkuubwa kutoka kwenye idara Fulani nyeti kutokana na muonekano wangu,, wananipa heshima zote hadi najionea wivu ! Wakati mwingine nafaidi nisivyostahili ila basi tu wacha iwe hivyo!
 
Hahahaha mkuu umenikumbusha mbali Sana
Mimi nilivokua chuo wale washikaji waliokua wananifata kupiga misele kalibia wote walidisko ilifika hatua mtu akidisco wanauliza kwani ulikua na urafiki na buzitata?

Ila walichokua hawajui Mimi nasoma sehem zenye makelele na sio sehem iliyotulia so nlikua nikitaka kupiga msuli ni lazima nianzishe zogo darasan hapo ndo mambo yanapanda Ila wenzangu walikua hawajui kwamba hapo mm ndo mambo yanapanda kinoma.
 
Uko wapi pacha wangu!!!?
 
Safii
 
Hao huwa wanatumwa ku deposit hela za maduka makubwa au ya jumla wala sio matajiri. Kama unaenda sana benki utawaona wengi tu hata waswahili usitishike mkuu wametumwa hao.
 
Hii imekaa kama kilimo cha matikiti tumeona faida tu bila changamoto na hasara.

Ujaeleza chuo ulipata mkopoa ua hukupata, ujaeleza mbilinge za Lecture Sup, Carry nk

Ujaeleza msoto wa ajira na michakato mingine.

Ujaeleza Intiview ulizogonga kutoka kazi moja hadi nyengine.

Vizurungu vya michepuko, muda wa kula tujaona au ulikuwa auli, muda wa kwenda Toilet, muda wa kulala, kucheki Movie nk.

Yaani wewe ujaonesha kuna siku ulipoteza nauri 😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Hao huwa wanatumwa ku deposit hela za maduka makubwa au ya jumla wala sio matajiri. Kama unaenda sana benki utawaona wengi tu hata waswahili usitishike mkuu wametumwa hao.
[emoji3][emoji3] wenye hela wengi huogopa kupeleka hela benki wao wenyewe kwani wanakuwa targeted na wahalifu hivyo huwatumia wafanyakazi wao au mtu yeyote anayemwamini kwenda kudeposit.

Wale wajaza rambo kwenye mabenki huwa si wamiliki wa zile hela.


** Hawa waaminifu wa kudeposit mahela ya maboss wao huwa ka mapoyoyo dizaini hivi lakini wanapewaga posho kwa kazi hiyo, au mshahara unakuwa mkubwa.

Ukiwa mjanja mjanja huwezi pewa hiyo kazi.
 
Du.. mimi huyo?
 
Dah[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 

Iyo ni kazi au danga?
 
Kuna mfalme mmoja India alienda London kwenye ofisi za Roll royce akiwa amevaa kawaida tuu akaambulia dharau kisa muonekano wake baadae akaja akiwa amevaa mavazi ya kifalme akahakikisha amenunua magari ya Rolls Royce na kuyapeleka India ambapo aliyageuza yawe magari ya kubebea takataka.

Waliishia kuja kuomba msamaha kwa aibu.

Strory yake hii hapa

 
Nakumbuka nilifika kwenye kijiofisi changu mfanyakazi akanipa kimemo chenye namba za simu kimeandikwa mimi fulani naomba unipigie, ukweli nilisita ila nikaamua kumpigia simu akapokea na kuahidiana kukutana pale ofisini siku inayofata

Walikuja mabinti wawili wamechafuka miguuni vumbi na wanavuja jasho tu, wakajitambulisha na kueleza shida yao ambayo nilipaswa kumsaidia eneo la wazi la ofisi ili afanye ujasiriamali.

Nikiangalia hadhi ya ofisi na aina ya idea yake havifanani, nikapiga moyo konde

Nilimruhusu nikamwambia umeme na maji vyote asilipie yeye aendelee bure kabisa, Mungu alivyo mkubwa baada ya miezi kadhaa yule binti akapata ajira sehemu nyeti sana na amekuwa masaada mkubwa sana kwenye mambo yangu.

Tusiwadharau watu
 
hii ilitokea i think miaka 20 almost, ilikuwa kijiweni tunapiga story huku wengine wanacheza draft Asa muuza kahawa kapita akaitwa na mshikaji mmoja hivi alete kahawa yule jamaa akasema wape wote kahawa walioko hapa basi bwana muuza kahawa akagawa kahawa, Asa yule jamaa alinunua kahawa sijui alitofautiana nini na jamaa aliyekua anacheza naye draft mara tukasikia anamwambia yule jamaa" wee utanambia nini kahawa yenyewe nimekununulia" basi yule jamaa alghafurika sana na maneno ya yule mshikaji, basi jamaa akaanza kuwapigia madereva wake waje pale kijiweni wakaja dereva tax, coast,dsm wakazipaki pembeni na jamaa alikuwa mpole huwezi mzania, basi wale dereva wakamulizaa" vp bosi mbona umetuita jamaa kwa upole akasema huyu jamaa kaninunulia kahawa kikombe kimoja tuu kaanza kunisema, wale madereva wakaanza kumsema jamaa yaani unamchukulia powa huyu bosi wetu na si haya magari tuu anamaduka na mahotel, yule jamaa aliyenunua kahawa akaona aibu

yaani hakuna aliye amini pale kijiweni kama jamaa anaweza kumiliki mali kiasi kile kutokana na muonekano wake kila mtu alimrespect jamaa

ndg zangu tuache dharau haifai
 
chai
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…