Ushawahi kuchukuliwa poa na mtu halafu akakuta sivyo kama alivyokudhania?

Ushawahi kuchukuliwa poa na mtu halafu akakuta sivyo kama alivyokudhania?

Kwanza naomba 'nidiclee' kwamba mm ni mmoja wa ME ambae si mtu wa fashion, yani mimi sijui kuvaa kabisa na sina hiyo passion ya pamba pamba. Nishawahi kusemwa sana na ma-ex wangu kuhusu uvaaji wangu lakini haikusaidia kitu.

Sasa weekend iliyopita nilienda sehemu moja flani hivi amazing, chimbo la uhakika haswaa, limejitenga na limetulia kweli. Nilipigilia kipensi changu na ka t-shirt flan hivi local nikachagua sehem nikakaa, kutizama vizuri nikaona kuna meza amekaa mdada mmoja hivi and of coz she is gud looking nikaamua kujitosa angalau kumpa hata hi 'coz tulikuwa wateja 2 tu, nikamfata nikamsalimu.

Yule dada kwanza alinishusha kuanzia juu mpaka chini then akaitikia salamu yangu ki-design kama namsumbua flani hivi. Nikaomba kujumuika nae kama asipojali. Jibu lake ndo lilinitoa confidence kabsa, alinambia: "Kwahiyo kaka unadhani kila msichana akikaa peke yake anahitaji kampani? Hapana sihitaji" Dah, mwanamme nikajizoazoa pale nikarudi nilipokaa. Nilikaa kama masaa ma3 hivi nikaamsha zangu. Sasa kilichotokea jana ndo kimenifanya niandike huu uzi.

Nilipokea maagizo kuanzia J3 ya wiki hii kuwa leo watakuja watu wa Taasisi flani ya kifedha kutoa semina kwa sisi wafanyakazi kwa ajili ya kutushawishi kujiunga na huduma za Taasisi yao, hivyo mimi nikapewa jukumu la kuwakaribisha na kuwapeleka sehemu ambapo semina itafanyika.

Asubuhi mida kama ya saa 3 hv ugeni ukafika, walikuwa watu kama 7 hivi, kati yao alikuwepo yule dada nilieonana naye weekend.

Wakaingia ofisini nikawakaribisha, wakati mkubwa wao anatoa introduction macho nikayakaza kwa yule dada, bahati nzuri tukagonganisha macho, akashtuka flani, nikajua kashanikumbuka.

Baada ya semina kuisha ikafika kipindi cha watu kujiunga sasa kwa walioshawishika. Nikamfata yule dada nikamuomba aje anielekeze namna ya ujazaji fomu. Alivyofika tu, nikamuuliza "Unanikumbuka?" Akachekaaa, akaniambia "Yani wewe, sikutarajia kama unaweza kuwa unafanya kazi huku", nikamuuliza ulitarajia niwe nafanya kazi wapi? Akaishia kucheka tu. Mawasiliano yake kanipa; fresh bila shida kabisa.

Sasa naomba kuuliza wadau, mshawahi kukutana na situation ya namna hii?
Aiseee...!
Umenikumbusha mkasa mzuri tena wa zamani kidogo.

Ni mkasa wa kweli wa umfikiriaye ni mswahili wa low class, kumbe miaka ikipita ndo anakuwa matawi ya juu.

Kulikuwa na dame, mzuri sana , miguu ya kupendeza figure eight na kwa kweli kila nikimuona moyo waenda mbio.
Na alikuwa ni cheusi mangala, super black, akicheka meno meupee ya kuvutia, juu ni afro zuri natural, hadi leo hii.
Wazazi wake nilikuwa nawafahamu, nivyo nikaona itakuwa rahisi kukubalika.
Ndo kwanza miaka hiyo nimemaliza Form six, dame anaelekea kumaliza form IV.

Sasa nikawa nimepata kibarua cha ukarani benki, hivyo vijisenti vya kununua soda sikosi.
Nikamwaga sera kwa dame yule.
Yeye akawa kama ananihurumia tu, maana anaona nampenda sana lakini anashindwa kuwa muwazi.
Miezi ikapita mingi tu, tuna date na kila tukionana naona hakuna maendeleo, hadi dada zangu wakaanza kunihurumia pia, penzi linavyonitesa.

Mwisho yule dame akaniambia wazi, we bwana si saizi yangu, kwanza watoka Uswazi.
Akaniambia nina mchumba mtoto wa balozi fulani, famous hapa mjini.
Na wazazi wa yule dame walilielewa hilo, kulingana na dame mzuri.

Basi sikukata tamaa, nilijahidi kumweleza dame wangu huyu kuwa mimi haipiti miaka miwili nitaingia chuo kikuu na nikimaliza sitakosa noti ndefu kukutunza wewe na familia, nikubalie tu.
Dame akakataa kata kata.

Siku aliyohitimisha maneno ya kunikataa niliugua, tena homa kali na ya kweli kabisa.
Sikujua kuwa penzi literaly ni homa ya moyo!
Nilinyong’onyea na kulala kitandani siku mbili.

Ile homa naikumbuka vizuri sana.
Slowly homa iliondoa na kukausha upendo wote kwa yule dada.
Nilistaajabu hata mimi kwani nikajiuliza , kwa nini niteseke?
Na kwa muda mrefu sikutafuta tena msichana mwingine awe girlfriend wangu wa kudumu, ile homa iliniumiza ifikra.

Miaka ikapita, na kweli nikaenda UDSM, na kukamilisha kadigilii kangu na kazi nzuri nikapata.
Kazi nikaendelea kupata nzuri zaidi, kumbe yule dame, cheusi mangala, ananifuatilia kwa mbaali.

Miaka mingi ikapita, na mambo yangu alhamdulilhi yakawa si mabaya sana.
Wakati huo ikawa nimepata fiancee kwa kweli mzuri sana, tena half caste.


Huku nyuma dame cheusi akajileta, na tukala mzigo.
Aliponiuliza itakuwaje sasa, nikamwambia tu ukweli kuwa naoa miezi michache ijayo, ile chance haikuwa yetu.
Alilia sana yule dame mzuri.

Mbaya zaidi mie kikazi nikawa matawi ya juu sana, kama nilivyomuahidi dame cheusi nilipokuwa namtongoza na akakataa.
Sikumuuliza imekuwaje na yule mtoto wa balozi, maana sikuona kama yananihusu.
Dame cheusi mangala bado ni mzuri na akajaolewa na classmate wangu.

UPDATE:
Tunaandika hadithi ambazo ni za ukweli kabisa.
Cheusi Mngala baadaye niliambiwa mume wake alikuja fariki kwa ugonjwa wa sukari.
Ingawaje wengi tuihisi ni kale kaugonjwa kanako sumbua.
Kilichonishtua majuzi ni kuambiwa Cheusi Mangala naye kafariki, nilivyompenda nililia!
 
Mimi kwangu ni tofauti kidogo kwani watu wengi hunichukulia kama mtu mkuubwa kutoka kwenye idara Fulani nyeti kutokana na muonekano wangu,, wananipa heshima zote hadi najionea wivu ! Wakati mwingine nafaidi nisivyostahili ila basi tu wacha iwe hivyo!
 
Mimi tangu O'level sijawahi kuwa na ule mwonekano wa kidenti, nilikuwa Hip Hop sana Dickies juu na chini, Converse za kutosha, Double Denim (jeans) chini tim boots ukiniona waweza sema tozi flani hivi au muhuni tu, watu wasionifahamu walikuwa wanani-underestimate sana, nilitambua hilo na wala halikunipa tabu. Nakumbuka early 2010's nikiwa nakaribia kufanya UE ya mwisho watu walikuwa bize sana, mi kama kawaida sina habari na mtu ndo kwanza napiga misele Jamatini (Dom). Sasa kuna mwana mmoja alikuwa anaishi room opposite na yetu katika bweni flani hivi, nilikuwa nimemwacha mwaka mmoja ila kozi tofauti, jamaa tangu tumefahamiana alikuwa ananipimia kama mtu nisiejali hivi, sasa a week before UE, tukiwa cafeteria na wana na huyo jamaa alikuwepo, tulivyomaliza kula tu, wana wakasema wanarudi class kukazia, mi nikasema narudi room kula music. Dah mshikaji uzalendo ukamshinda ikabidi anichane tu, akasema mzee baba "be watchful tusijehitimu wote mwakani" mi nika-smile tu, wanangu wengine wakacheka sana kisha tukapotea. Around November hivi karibia na graduation, nimeamka asubuhi missed calls kibao moja wapo ya ex wangu nilimwacha college. Nikamtwangia, neno lake la kwanza tu akasema sawa kipanga, you are a good cheater, sikumwelewa zaidi akasema hebu cheki website ya chuo. Banaaa eeh kucheki tu mwana nime-top darasa, overall 4+ flani hivi na nnahitajika kwenye convocation ceremony the next day nikachukue zawadi, nikadandia Shabiby fastaaa. Nimetoka kuchukua joho si nikakutana na yule mwana, sikuongea kitu zaidi ya salamu ila aliona aibu kinoma maana alikuwa ni classmate wa ex wangu, na keshapata habari akaishia tu kusema sawa super star sikuwezi.
Hahahaha mkuu umenikumbusha mbali Sana
Mimi nilivokua chuo wale washikaji waliokua wananifata kupiga misele kalibia wote walidisko ilifika hatua mtu akidisco wanauliza kwani ulikua na urafiki na buzitata?

Ila walichokua hawajui Mimi nasoma sehem zenye makelele na sio sehem iliyotulia so nlikua nikitaka kupiga msuli ni lazima nianzishe zogo darasan hapo ndo mambo yanapanda Ila wenzangu walikua hawajui kwamba hapo mm ndo mambo yanapanda kinoma.
 
Kiukweli mimi iko tofaut nina mwili na sura flani ya kiboss niki chomekea unaweza kujua nina miliki kampuni au ni mtu flani wa kitengo ninacho shukuru popote ninapoingia huwa ninachangamkiwa sana hata barabaran trafki nikiwapiga mkwara huwa wananiachia kwa adabu zote.
Uko wapi pacha wangu!!!?
 
Mi kuna mwaka flani nilipewa promotion kwenda kuwa branch manager mkoa flani. Sasa sabab nilikua bachelor nikauza vitu vyote nikabaki na mabegi ya nguo nikapaki kwenye ndinga nikaamsha. Nikafika mkoani mida ya sa 9 na mafuta yalikua yamekaribia kuisha nikasema nikachomoe mpunga kwenye atm ya hiyo bank ninayofanyia kazi. Nilivomaliza kutoa hela na muda wa bank bado nikasema niingie kumsalimia branch manager aliyepo maana tulikua tunafahamiana. Ile kuingia reception mdada mmoja matata sana ndo yupo pale na pembeni kaka jamaa mwingine..nikamsalimia akaitika vizuri tu,nikamwambia naomba kuonana na meneja..akainua macho kuniangalia...akanambia sema shida yako...nikamwambia shida yangu ni personal,akasema huwezi kumuona ..tena kwa madharau. Na yule jamaa wa pembeni akaniangalia akaendelea na ishu zake.Nikamwambia basi sawa ntampigia simu,akanijibu kwa kejeli kumbe namba yake unayo...yule jamaa wa pembeni akacheka..nikasepa nikaenda kuchkua hotel. Jion nikamcall meneja nikamwambia nipo nishafika akafurahi sana maana kama nilimsurprise na skumwambia kama nilifika ofisin. Jioni akanitafuta tukapiga vyombo huku akinionesha machimbo. Kesho yake asubuhi kwenye morning talk akawaambia staff meneja mpya kashafika atakuja mchana kuwasalimia. Mchana wake nikaibuka... Hahahahaaaa basi wapenzi wasikilizaji mtamalizia wenyewe kilichofuata.

Kisa cha pili ni sehem nilipoenda kupanga room maana sikua na familia na vitu niliuza so nikazama kama ninja...wakawa na madharau yao mi sina time nao mpaka wamekuja kujua badae sana ndo wanajichekesha maana hata gari nilikua silazi pale hapakua na parking.
Safii
 
Siku moja nikiwa bank ya Exim na deposit pesa, while tupo kwenye foleni ghafla alikuja mzee fulani ana asili ya kihindi, mzee alikua normal tu yani ukimuona alivyo unaweza sema ni homeless maana allikua kawaida sana. Sisi tupo kwenye foleni ghalfa akaja nahisi ni meneja wa bank akasema jamani naombeni mmpisheni huyu babu hapa, nyie wote hamieni dirisha lingine, muda si mrefu mtu wa kuwahudumia atakuja.

Kiukweli yule mzee binafsi sikua nimemdharau kama ile dharau ya kujikweza, ila kiukweli nilikua nimemchukulia poa, hasa ukijumlisha na tukio la kuhamishwa dirisha la kupata huduma.

Yule mzee bhana alikua na begi kubwa kama la wale wanaopandia milima, alifungua akatoa rambo (kipindi hicho zilikua hazijafungiwa) rambo kubwa zile za kufungia mabegi kama mtu unasafiri.
Aiseh ile rambo ilikua imejaa pesa mpaka juu haifungi vizuri, kwa haraka haraka zilikua zinaonekana noti za elfu 10 kwenye mabunda ya kama milioni 1, moja hivi, . Kiukweli kila mtu alibaki ameduwaa, basi binafsi nikiangalia pesa niliyokua na deposit nikachoka kabisa nikajisemea hakika hapa dunia kuna wengine tunawasindikiza watu kuishi [emoji3]

All in all lesson niliyopata siku ile ni kwamba usimchukulie mtu yoyote poa.
Hao huwa wanatumwa ku deposit hela za maduka makubwa au ya jumla wala sio matajiri. Kama unaenda sana benki utawaona wengi tu hata waswahili usitishike mkuu wametumwa hao.
 
Aiseee...!
Umenikumbusha mkasa mzuri tena wa zamani kidogo.

Ni mkasa wa kweli wa umfikirie ni mswahili wa low class kumbe miaka ikipita ndo anakuwa matawi ya juu.

Kulikuwa na dame, mzuri sana , miguu ya kupendeza figure eight na kwa kweli kila nikimuona moyo waenda mbio.
Na alikuwa ni cheusi mangala, super black, akicheka meno meupee ya kuvutia, juu ni afro zuri natural, hadi leo hii.
Wazazi wake nilikuwa nawafahamu, nivyo nikaona itakuwa rahisi kukubalika.
Ndo kwanza miaka hiyo nimemaliza Form six, dame anaelekea kumaliza form IV.

Sasa nikawa nimepata kibarua cha ukarani benki, hivyo vijisenti vya kununua soda sikosi.
Nikamwaga sera kwa dame yule, akawa kama ananihurumia tu maana anaona nampenda sana lakini anashindwa kuwa muwazi.
Miezi ikapita mingi tu tuna date na naona hakuna maendeleo, hadi dada zangu wakaanza kunihurumia pia, penzi linavyonitesa.

Mwisho yula dame akaniambia wazi, we bwana si saizi yangu, kwanza watoka Uswazi.Nina mchumba mtoto wa balozi fulani, famous hapa mjini.
Na wazazi wa yuledame walilielewa hilo, kulingana na dame mzuri.

Basi nilijahidi kumweleza dame wangu huyu kuwa mimi haipiti miaka miwili nitaingia chuo kikuu na nikimaliza sitakosa noti ndefu kukutunza wewe na familia, nikubalie tu.
Dame akakataa kata kata.

Siku aliyohitimisha maneno ya kunikataa niliugua, tena homa kali na ya kweli kabisa.
Nilinyong’onyea na kulala kitandani siku mbili.

Ile homa naikumbuka sana, slowly ilionfoa na kukausha upendo wote kwa yule dada.

Miaka ikapita, na kweli nikaenda UDSM, na kukamilisha kadigilii kangu na kazi nzuri nikapata.
Kazi nikaendelea kupata nzuri zaidi, kume yule dame ananifuatilia kwa mbaali.

Nikawa nimepata fiancee kwa kweli mzuri sana, tena half caste.
Huku nyuma dame cheusi akajileta, na tukala mzigo.
Aliponiuliza itakuwaje sasa, nikamwambia tu ukweli kuwa naoa miezi michache ijayo, ile chnce haikuwa yetu.
Alilia sana yule dame mzuri.

Mbaya zaidi mie kikazi nikawa matawi ya juu sana, kama nilivyomuahidi dame cheusi nilipokuwa namtongoza na akakataa.
Sikumuuliza imekuwaje na yule mtoto wa balozi, maana sikuona kama yananihusu.
Dame cheusi mangala bado ni mzuri na kajaolewa na classmate wangu.
Hii imekaa kama kilimo cha matikiti tumeona faida tu bila changamoto na hasara.

Ujaeleza chuo ulipata mkopoa ua hukupata, ujaeleza mbilinge za Lecture Sup, Carry nk

Ujaeleza msoto wa ajira na michakato mingine.

Ujaeleza Intiview ulizogonga kutoka kazi moja hadi nyengine.

Vizurungu vya michepuko, muda wa kula tujaona au ulikuwa auli, muda wa kwenda Toilet, muda wa kulala, kucheki Movie nk.

Yaani wewe ujaonesha kuna siku ulipoteza nauri 😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Hao huwa wanatumwa ku deposit hela za maduka makubwa au ya jumla wala sio matajiri. Kama unaenda sana benki utawaona wengi tu hata waswahili usitishike mkuu wametumwa hao.
[emoji3][emoji3] wenye hela wengi huogopa kupeleka hela benki wao wenyewe kwani wanakuwa targeted na wahalifu hivyo huwatumia wafanyakazi wao au mtu yeyote anayemwamini kwenda kudeposit.

Wale wajaza rambo kwenye mabenki huwa si wamiliki wa zile hela.


** Hawa waaminifu wa kudeposit mahela ya maboss wao huwa ka mapoyoyo dizaini hivi lakini wanapewaga posho kwa kazi hiyo, au mshahara unakuwa mkubwa.

Ukiwa mjanja mjanja huwezi pewa hiyo kazi.
 
Hii imekaa kama kilimo cha matikiti tumeona faida tu bila changamoto na hasara.

Ujaeleza chuo ulipata mkopoa ua hukupata, ujaeleza mbilinge za Lecture Sup, Carry nk

Ujaeleza msoto wa ajira na michakato mingine.

Ujaeleza Intiview ulizogonga kutoka kazi moja hadi nyengine.

Vizurungu vya michepuko, muda wa kula tujaona au ulikuwa auli, muda wa kwenda Toilet, muda wa kulala, kucheki Movie nk.

Yaani wewe ujaonesha kuna siku ulipoteza nauri 😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
Du.. mimi huyo?
 
Dah[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mm miaka hii nimeanzisha michezo ya kizungu. Nikiwa na mihadi na mtu nionane nae namuelekeza aje sehemu ya kulia chakula hotel kubwa kubwa nikifika kule naagiza kisosi kidogo cha mboga za majani au kikombe cha maziwa na yai moja la kuchemsha hapo najua hata 10K haifiki. Mda huo chai inachemka nachukua sim naanza kuchambua timu za kubet huku namsubiri best yangu aje. Basi wahudumu wanajuaga huyu jamaa mnyamwezi au kaishi sana mbele, kumbe nawaangalia wazungu Instagram alafu naigiza.
 
Mimi uzuri nna adabu simdharau mtu kwakweli ila kuna Mtu aliwahi kuvuka matarajio yangu yani sikutegemea.
Maana jamaa alitaka nikamfanyie kazi fulani akanambia niandike namba aatanicheki anatumia Tecno S series[emoji23] nikadharau nikajisemea huyu nae nani🤣,siku ya kazi kaja kunichukua Offisini na Range rover sport anaishi Cliffside resiidence
toure dr hakuna kazi nililipwa kama hio mtu unafanya kazi huku unakunywa Moet Chandon Shampaigne

Iyo ni kazi au danga?
 
Kuna mfalme mmoja India alienda London kwenye ofisi za Roll royce akiwa amevaa kawaida tuu akaambulia dharau kisa muonekano wake baadae akaja akiwa amevaa mavazi ya kifalme akahakikisha amenunua magari ya Rolls Royce na kuyapeleka India ambapo aliyageuza yawe magari ya kubebea takataka.

Waliishia kuja kuomba msamaha kwa aibu.

Strory yake hii hapa

 
Nakumbuka nilifika kwenye kijiofisi changu mfanyakazi akanipa kimemo chenye namba za simu kimeandikwa mimi fulani naomba unipigie, ukweli nilisita ila nikaamua kumpigia simu akapokea na kuahidiana kukutana pale ofisini siku inayofata

Walikuja mabinti wawili wamechafuka miguuni vumbi na wanavuja jasho tu, wakajitambulisha na kueleza shida yao ambayo nilipaswa kumsaidia eneo la wazi la ofisi ili afanye ujasiriamali.

Nikiangalia hadhi ya ofisi na aina ya idea yake havifanani, nikapiga moyo konde

Nilimruhusu nikamwambia umeme na maji vyote asilipie yeye aendelee bure kabisa, Mungu alivyo mkubwa baada ya miezi kadhaa yule binti akapata ajira sehemu nyeti sana na amekuwa masaada mkubwa sana kwenye mambo yangu.

Tusiwadharau watu
 
hii ilitokea i think miaka 20 almost, ilikuwa kijiweni tunapiga story huku wengine wanacheza draft Asa muuza kahawa kapita akaitwa na mshikaji mmoja hivi alete kahawa yule jamaa akasema wape wote kahawa walioko hapa basi bwana muuza kahawa akagawa kahawa, Asa yule jamaa alinunua kahawa sijui alitofautiana nini na jamaa aliyekua anacheza naye draft mara tukasikia anamwambia yule jamaa" wee utanambia nini kahawa yenyewe nimekununulia" basi yule jamaa alghafurika sana na maneno ya yule mshikaji, basi jamaa akaanza kuwapigia madereva wake waje pale kijiweni wakaja dereva tax, coast,dsm wakazipaki pembeni na jamaa alikuwa mpole huwezi mzania, basi wale dereva wakamulizaa" vp bosi mbona umetuita jamaa kwa upole akasema huyu jamaa kaninunulia kahawa kikombe kimoja tuu kaanza kunisema, wale madereva wakaanza kumsema jamaa yaani unamchukulia powa huyu bosi wetu na si haya magari tuu anamaduka na mahotel, yule jamaa aliyenunua kahawa akaona aibu

yaani hakuna aliye amini pale kijiweni kama jamaa anaweza kumiliki mali kiasi kile kutokana na muonekano wake kila mtu alimrespect jamaa

ndg zangu tuache dharau haifai
 
hii ilitokea i think miaka 20 almost, ilikuwa kijiweni tunapiga story huku wengine wanacheza draft Asa muuza kahawa kapita akaitwa na mshikaji mmoja hivi alete kahawa yule jamaa akasema wape wote kahawa walioko hapa basi bwana muuza kahawa akagawa kahawa, Asa yule jamaa alinunua kahawa sijui alitofautiana nini na jamaa aliyekua anacheza naye draft mara tukasikia anamwambia yule jamaa" wee utanambia nini kahawa yenyewe nimekununulia" basi yule jamaa alghafurika sana na maneno ya yule mshikaji, basi jamaa akaanza kuwapigia madereva wake waje pale kijiweni wakaja dereva tax, coast,dsm wakazipaki pembeni na jamaa alikuwa mpole huwezi mzania, basi wale dereva wakamulizaa" vp bosi mbona umetuita jamaa kwa upole akasema huyu jamaa kaninunulia kahawa kikombe kimoja tuu kaanza kunisema, wale madereva wakaanza kumsema jamaa yaani unamchukulia powa huyu bosi wetu na si haya magari tuu anamaduka na mahotel, yule jamaa aliyenunua kahawa akaona aibu

yaani hakuna aliye amini pale kijiweni kama jamaa anaweza kumiliki mali kiasi kile kutokana na muonekano wake kila mtu alimrespect jamaa

ndg zangu tuache dharau haifai
chai
 
Back
Top Bottom