Aiseee...!
Umenikumbusha mkasa mzuri tena wa zamani kidogo.
Ni mkasa wa kweli wa umfikirie ni mswahili wa low class kumbe miaka ikipita ndo anakuwa matawi ya juu.
Kulikuwa na dame, mzuri sana , miguu ya kupendeza figure eight na kwa kweli kila nikimuona moyo waenda mbio.
Na alikuwa ni cheusi mangala, super black, akicheka meno meupee ya kuvutia, juu ni afro zuri natural, hadi leo hii.
Wazazi wake nilikuwa nawafahamu, nivyo nikaona itakuwa rahisi kukubalika.
Ndo kwanza miaka hiyo nimemaliza Form six, dame anaelekea kumaliza form IV.
Sasa nikawa nimepata kibarua cha ukarani benki, hivyo vijisenti vya kununua soda sikosi.
Nikamwaga sera kwa dame yule, akawa kama ananihurumia tu maana anaona nampenda sana lakini anashindwa kuwa muwazi.
Miezi ikapita mingi tu tuna date na naona hakuna maendeleo, hadi dada zangu wakaanza kunihurumia pia, penzi linavyonitesa.
Mwisho yula dame akaniambia wazi, we bwana si saizi yangu, kwanza watoka Uswazi.Nina mchumba mtoto wa balozi fulani, famous hapa mjini.
Na wazazi wa yuledame walilielewa hilo, kulingana na dame mzuri.
Basi nilijahidi kumweleza dame wangu huyu kuwa mimi haipiti miaka miwili nitaingia chuo kikuu na nikimaliza sitakosa noti ndefu kukutunza wewe na familia, nikubalie tu.
Dame akakataa kata kata.
Siku aliyohitimisha maneno ya kunikataa niliugua, tena homa kali na ya kweli kabisa.
Nilinyong’onyea na kulala kitandani siku mbili.
Ile homa naikumbuka sana, slowly ilionfoa na kukausha upendo wote kwa yule dada.
Miaka ikapita, na kweli nikaenda UDSM, na kukamilisha kadigilii kangu na kazi nzuri nikapata.
Kazi nikaendelea kupata nzuri zaidi, kume yule dame ananifuatilia kwa mbaali.
Nikawa nimepata fiancee kwa kweli mzuri sana, tena half caste.
Huku nyuma dame cheusi akajileta, na tukala mzigo.
Aliponiuliza itakuwaje sasa, nikamwambia tu ukweli kuwa naoa miezi michache ijayo, ile chnce haikuwa yetu.
Alilia sana yule dame mzuri.
Mbaya zaidi mie kikazi nikawa matawi ya juu sana, kama nilivyomuahidi dame cheusi nilipokuwa namtongoza na akakataa.
Sikumuuliza imekuwaje na yule mtoto wa balozi, maana sikuona kama yananihusu.
Dame cheusi mangala bado ni mzuri na kajaolewa na classmate wangu.