Ushawahi kuchukuliwa poa na mtu halafu akakuta sivyo kama alivyokudhania?

Ushawahi kuchukuliwa poa na mtu halafu akakuta sivyo kama alivyokudhania?

Siku moja nikiwa bank ya Exim na deposit pesa, while tupo kwenye foleni ghafla alikuja mzee fulani ana asili ya kihindi, mzee alikua normal tu yani ukimuona alivyo unaweza sema ni homeless maana allikua kawaida sana. Sisi tupo kwenye foleni ghalfa akaja nahisi ni meneja wa bank akasema jamani naombeni mmpisheni huyu babu hapa, nyie wote hamieni dirisha lingine, muda si mrefu mtu wa kuwahudumia atakuja.

Kiukweli yule mzee binafsi sikua nimemdharau kama ile dharau ya kujikweza, ila kiukweli nilikua nimemchukulia poa, hasa ukijumlisha na tukio la kuhamishwa dirisha la kupata huduma.

Yule mzee bhana alikua na begi kubwa kama la wale wanaopandia milima, alifungua akatoa rambo (kipindi hicho zilikua hazijafungiwa) rambo kubwa zile za kufungia mabegi kama mtu unasafiri.
Aiseh ile rambo ilikua imejaa pesa mpaka juu haifungi vizuri, kwa haraka haraka zilikua zinaonekana noti za elfu 10 kwenye mabunda ya kama milioni 1, moja hivi, . Kiukweli kila mtu alibaki ameduwaa, basi binafsi nikiangalia pesa niliyokua na deposit nikachoka kabisa nikajisemea hakika hapa dunia kuna wengine tunawasindikiza watu kuishi [emoji3]

All in all lesson niliyopata siku ile ni kwamba usimchukulie mtu yoyote poa.
Kiukweli huyo ni msukule wa kihindi alitumwa kuleta zile pesa na mdogo wake, amini hivo
 
Aiseee...!
Umenikumbusha mkasa mzuri tena wa zamani kidogo.

Ni mkasa wa kweli wa umfikirie ni mswahili wa low class kumbe miaka ikipita ndo anakuwa matawi ya juu.

Kulikuwa na dame, mzuri sana , miguu ya kupendeza figure eight na kwa kweli kila nikimuona moyo waenda mbio.
Na alikuwa ni cheusi mangala, super black, akicheka meno meupee ya kuvutia, juu ni afro zuri natural, hadi leo hii.
Wazazi wake nilikuwa nawafahamu, nivyo nikaona itakuwa rahisi kukubalika.
Ndo kwanza miaka hiyo nimemaliza Form six, dame anaelekea kumaliza form IV.

Sasa nikawa nimepata kibarua cha ukarani benki, hivyo vijisenti vya kununua soda sikosi.
Nikamwaga sera kwa dame yule, akawa kama ananihurumia tu maana anaona nampenda sana lakini anashindwa kuwa muwazi.
Miezi ikapita mingi tu tuna date na naona hakuna maendeleo, hadi dada zangu wakaanza kunihurumia pia, penzi linavyonitesa.

Mwisho yula dame akaniambia wazi, we bwana si saizi yangu, kwanza watoka Uswazi.Nina mchumba mtoto wa balozi fulani, famous hapa mjini.
Na wazazi wa yuledame walilielewa hilo, kulingana na dame mzuri.

Basi nilijahidi kumweleza dame wangu huyu kuwa mimi haipiti miaka miwili nitaingia chuo kikuu na nikimaliza sitakosa noti ndefu kukutunza wewe na familia, nikubalie tu.
Dame akakataa kata kata.

Siku aliyohitimisha maneno ya kunikataa niliugua, tena homa kali na ya kweli kabisa.
Nilinyong’onyea na kulala kitandani siku mbili.

Ile homa naikumbuka sana, slowly ilionfoa na kukausha upendo wote kwa yule dada.

Miaka ikapita, na kweli nikaenda UDSM, na kukamilisha kadigilii kangu na kazi nzuri nikapata.
Kazi nikaendelea kupata nzuri zaidi, kume yule dame ananifuatilia kwa mbaali.

Nikawa nimepata fiancee kwa kweli mzuri sana, tena half caste.
Huku nyuma dame cheusi akajileta, na tukala mzigo.
Aliponiuliza itakuwaje sasa, nikamwambia tu ukweli kuwa naoa miezi michache ijayo, ile chnce haikuwa yetu.
Alilia sana yule dame mzuri.

Mbaya zaidi mie kikazi nikawa matawi ya juu sana, kama nilivyomuahidi dame cheusi nilipokuwa namtongoza na akakataa.
Sikumuuliza imekuwaje na yule mtoto wa balozi, maana sikuona kama yananihusu.
Dame cheusi mangala bado ni mzuri na kajaolewa na classmate wangu.
Huu mwandiko si wa mtu mwenye ' digrii' nakataa katu katu[emoji21][emoji21][emoji21]
 
Kuna jamaa yangu amejenga hotel yake dodoma kali tu vyumba 10 na lowest ni chumba cha 55,000/=, na jamaa mwili wake ni mdogo mdogo hivi...basi juzi walikuja watu wa ccm kwenye teuzi zao wakafikia pale, kama bahati na jamaa yangu alikua pale hotelini kavaa pensi na tshirt anatoka nje tu akaitwa na wale watu wa ccm wakamuita jamaa wakamuuliza hii hotel ni ya nani (design kama walikua wanabishana) jamaa akasema yake, [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] wakampa mitusi wakajua kalewa ameleta utani wakamfukuza na kumfukuza pale....basi mwamba akasepa, wakamuita receptionist wakamuuliza akawajibu vile vile, ghafla meza ikapoa na utulivu ukaja, kibaya zaidi wakamuona mwamba anatoka zake na BMW lake X6....
 
Hao huwa wanatumwa ku deposit hela za maduka makubwa au ya jumla wala sio matajiri. Kama unaenda sana benki utawaona wengi tu hata waswahili usitishike mkuu wametumwa hao.
Watu wa hovyo hovyo wanaodeposit hela zao kabisa kabisa wako Makete

Wakinga balaa bwana, kuna kazee ukikakuta dukani kwake kanakula viazi vya kuchoma, hata supu kanaona anasa

Kakipeleka pesa benki kanabeba kwenye rambo lakini kwa mtazamo wa nje huwezi kukadhania

Wakinga/wabena wengi hawafanani na pesa yao
 
Kunasiku Weekend nilikuwa bored ukizingatia mama watoto wangu alisafiri kikazi LA nikafikiria kwenda sehemu locally nibarizi nikaona ni drive mjapani kutoka mikocheki Aim nipitie kufanya Shopping ya baadhi ya zaga ambazo nitazitumia nikifika ufukweni basi nikatoka nyumbani mikocheki mpaka Mcity nikafanya Shopping ile natoka napakiza zaga sindio nataka kufungua mlango niingie kwenye mpira mlinzi kanidukua akaanza kunidandia unataka kufanya nini gari la watu wewe mwizi nimepigwa nabutwaa namwambia Afande tatizo nini huu mpira wangu basi nikawaonesha Documents ndio wakaamini mimi nikaingia nawasikia aisee watoto wa washua mtoto mdogo anaPush Gari kama hii.

Walinikata moto wote ile siku nikarudi zangu Mikocheni kulala tu.
We jamaa hukomi tu, kujimwambafai[emoji15][emoji15][emoji15][emoji86]

scorpio me kuna mtu anakuchokoza bado[emoji16][emoji16][emoji1787][emoji1787]
 
Siku nyengine nilikuwa na meeting na wawekezaji ambao walikuwa tunafanya kama partnership na kampuni yao in terms of cammision based, ile meeting tulikuwa tunafanyia pale Akemi lwasababu ile ni Open Restaurant kwa mtu yeyote nilikodi Restaurant yote kukawa na walinzi wakuzuia watu wanaoingia hawausiki kazi yote ya kuOrganize kikao nilimuachia PA wangu nilichelewa kidogo sasa kufika pale mjengoni nikapanda na lift kufika mlangoni walinzi wananizuia shuka chini PA wangu akaona akawaambia 'BOSS' aisee waliomba msamaha nikawaambia Cool.

Watu wengi hawaamini kuona kijana wa makamo nina mafanikio niliyonayo.
[emoji2772][emoji2772][emoji2772][emoji2772]
 
Onana na PA wangu Millenium Tower floor ya 10 atakupa ratiba yote.
Asaaa mkuuu itabidi ufanikishe swala langu la kukuchukulia poa na hela zakoo za mawazo nipe ratiba yakoo
 
Siku nyengine nilikuwa na meeting na wawekezaji ambao walikuwa tunafanya kama partnership na kampuni yao in terms of cammision based, ile meeting tulikuwa tunafanyia pale Akemi lwasababu ile ni Open Restaurant kwa mtu yeyote nilikodi Restaurant yote kukawa na walinzi wakuzuia watu wanaoingia hawausiki kazi yote ya kuOrganize kikao nilimuachia PA wangu nilichelewa kidogo sasa kufika pale mjengoni nikapanda na lift kufika mlangoni walinzi wananizuia shuka chini PA wangu akaona akawaambia 'BOSS' aisee waliomba msamaha nikawaambia Cool.

Watu wengi hawaamini kuona kijana wa makamo nina mafanikio niliyonayo.
Tangu wafukue uzi wako sikuamini tena

Kwani Cammision ndio kitu gani?
 
sisi wengine baada ya hapo ndio huwa tunafunga vioo mazima,yaani fanya kama hatujawahi kukutana.

mimi jamaa alinisimulia hii tabia ya kudharau mikakati ya mtu katika maisha yake, usione mtu kazini yupo yupo tu miaka inaenda ukamdharau kwamba hana mipango, utajichanganya.

jamaa anasema wameanza kazi mwaka mmoja na huyo mshikaji wake, yeye akawa amepanga nyumba ya gharama kama 250k,usafiri wa kusumbulia watumjini nk. mwenzake yupo yupo tu. nyumba katafuta ya 120k, gari hakununua nk.

wamefanya kazi kama miaka 8 hivi. baadae siku moja wanapiga story jamaa yangu sasa akaanza maneno ya kumsimanga jamaa, oooh we vipi bana hela hatuoni wapi unapeleka, upo upo tu kama mshamba.jamaa akakereka ikabidi amuonyeshe salio bank, akasoma kwa utulivu ilikuwa ni 68mil, kwenye simu kuna 7mil.

baada ya pale jamaa siku yake iliharibika sana.
Mkuu mpe hai huyo jamaa nwenye 7mil kwenye simu,nwambie anitafute nijue siri ya urembo
 
Back
Top Bottom