Ushawahi kuchukuliwa poa na mtu halafu akakuta sivyo kama alivyokudhania?

Ushawahi kuchukuliwa poa na mtu halafu akakuta sivyo kama alivyokudhania?

Juzi tu NMB Dodoma:

Jamaa flan kavaavaa tu afu na midevudevu hivi

Kaenda NMB ATM kakuta na wadada wa benki wameweka meza ya kutoa huduma kwa wateja pemben hapo. Akafika tu kauliza (bila hata kusalimia).....kwanini kadi yangu inakataa kuniunganisha NMB mkononi

Dada kamjia juu...."kwanza salimia;...vipi habari za huko,...haya tukusaidie nini??"

Jamaa hakupokea. Mie nawaangalia tu.

Dada karudia tena ...."vipi mzima mwenzetu?? Za ulikotoka??!.....mbona umekuja kasi sana??!"....

Jamaa anaeaangalia tu. Mara akauliza...."ivi ni lazima kusalimia/ au kupokea salam ya mhudumu ili nipewe huduma NMB???...

Wakaanza kumshangaa ..."unatokea wapi wewe, yani unakuja kuvamia tu bila kusalimia..." ....wamamzodoa flan.

Jamaa akaingia Benki ndani. Straight kwa Meneja. Nafkiri hakueleza shida aliyopata nje. Alimueleza tu kama kutaka kusaidiwa shida yake. Sijui ndani waliongea nini??

Wametoka na meneja...hadi pale ATM kwenye meza ya wale wadada....meneja akiwa kashika mkononi kadi ya yule mshua....akawambia wale wadada mmoja wao (sikumbuki jina)...

Meneja: .....hebu msaidie Katibu Mkuu hapa kumuunganisha na NMB Mkononi...(Meneja akaongeza:....mkuu hapa utahudumiwa)...mara meneja katuomba wote wa kwenye foleni ya ATM..."naomba ndugu tumpishe kiongozi anajambo kidogo kwenye ATM ...samahani"...wakaingia ATM meneja, mshua na yule dada.

Wakafanya mambo humo ...kidogo wakatoka. Tukaendelea.

Meneja akamsindikiza yule mshua hadi kwenye gari akaondoka meneja anapunga mkono.

Niliwaangalia wale akina dada mavi yalivyowagonga chupi. Walitoa macho sana wakawa na wasiwasi mkubwa....

Walimchukulia poa

Lakini kwa ubinadamu wetu salamu ni muhimu sana...huyu katibu mkuu si muungwana hata kidogo.

Hawakuwa na sababu ya kuogopa, hawakufanya kosa lolote
 
In my early 20s nilikuwa na gari ya Kijerumani. Nikataka kumgonga Mzee mmoja muuza madafu kwa baiskeli yule Mzee akaniangalia kwa dharau akasema 'mkishaiba magari ya Baba zenu mnakosa kabisa ustaarabu' nilikosa cha kumjibu.
Kuna demu alikuwa kanipa lift natural byuti, yeye aliambiwa na dereva bodaboda ndiyo maana mweusiii mpaka leo najiuliza alikuwa na maana gani.
 
Kuna siku tulienda Be Foward...na anko wangu mmoja toka dodoma...Sasa Anko mwenyewe kijana afu muhuni tu mtu wa fegi na miraa sasa alivyokaa kaa yani kama hana kitu...tukamkuta dada mmoja akatusikiliza, anko akamwambia anataka harrier nyeusi old model...basi dada akatuchukulia poa tu....na vile anko sio mjanja mjanja kila kitu anauliza...dada akajua hawa wamekuja kuuliza tu hakuna mteja.
Muda wa lunch ukafika dada anatuambia anataka kwenda kula, anko akamwambia ngoja tumalize then tutaenda wote...dada anasema wenzie wanamsubiri. Basi akazima PC ikabidi tutoke...sasa anko akawa kama anataka tukale na yule sista ili amzoee amchagulie gari zuri. Dada akatukataa akasema ana wenzake. Basi anko akampa 10k..next day tukarudi tukachagua gari afu tukaenda kulipia. Yule sister alikua suprised kweli
Befoward staff awe surprised mtu kuagiza Harrier old model??
 
Mwaka juzi natoka kijijini nkafika himo pale nikakuta nyomi ya abiria, nkapanga nichukue vichwa au la maana kuna siku nilichukua abiria aisee alinitesa sanaa, yaani gari ikifika speed 100 ni anaongea adi napunguza mwendo afu alikua mmama, na abiria wenzie wakawa wanamsapoti na mi napenda speed kali,

Nkapaki gari nkaenda kuzurura kuangalia mazingira nikinunua na mahitaji mbalimbali, nkaona mabinti wa3 wamekaa kinyonge baada ya kukosa usafiri na ni saa sita mchana, nkaenda kuwasalimu huku nawahoji vimaswali vya hapa na pale wa2 wakadharau ila yule mmoja akawa ananipa ushirikiano kiasi lkn mwenzie akamwambia kwa kilugha "achana na hilo limtu njoo tuongee mambo ya maana" (nilikua nmevaa ovyo tu na nguo chafu kidogo maana nilitoka porini) hapo wanalaumiana kwanini hawakwenda kupandia gari moshi mjini...

Nkamaliza kununua mahitaji yangu nkaenda washa gari nkawafuata nkamwita yule mmoja alieonyesha ushirikiano akaja nkamwambia mna sh ngapi niwapeleke dar, akasema wana elfu15, nkawaambia ungeni iwe 50 tuende wakafanya hivyo japo kwa aibu na shikamoo wakanipa[emoji23][emoji23][emoji23].

Njiani wanaongea kilugha japo sio cha kwetu kabisa ila nawaelewa sana, hapo wananiteta kiana huku wakilaumiana pengine ningewapunguzia kama wasingenidharau... Waliuliza kabla kama najua kilugha nkawadanganya mi mchaga lakini sijakulia wala kujua hiyo lugha zaidi ya salamu tu

Nkafanya makusudi nkapiga simu kwa jamaa ninaemwazima gari "oyaa mshua vipi, nipo njiani saa 3 ntakua dar nakuletea gari yako" kuskia ivo ndio wakaanza kuniteta tena nawachora tu.

Pale segera nkadakwa na trafiki kwa speed, wakati nawabembeleza nkawaambia sina kitu hii gari ilikua mkoani imeharibika mwenye nayo kaniomba niirudishe dar akaomba kadi ya gari kusoma na leseni akasema unadanganya? Au na leseni ya mwenye gari? Hayo yote walikua wanaskia, nkamalizana nae nkampoza elfu 5 akauliza hao kwenye gari ndugu zako nkamwambia hapana, akasema aliekaa mbele nimemuelewa, akaniambia zuga kidogo nichukue namba akaenda kaongea nae kachukua namba nkarudi kuendelea na safari.

Nkaskia wanaambiana "kumbe ikari li la kajamaa ka, keusani nalo hata ku" mmoja akajibu "tra isarau vandu utevaishi" alimaaninisha kumbe hili gari la haka kajamaa, wala hafanani nalo, mwenzie akamjibu, acha kudharau watu usiowajua.

Kufika dar heshima debe, kumbe walikua wanachuo niliwapeka adi UDSM,

Pisi moja niliielewa kesho yake nkala mzigo baada ya hapo anataka kunifanya kitega uchumi kanijazia mzigo wa shida zake nkampotezea.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji123]
 
Sasa kumbe na wewe ni mfanyakazi kama yeye tu

Mimi nilijua wewe ndio owner wa hiyo company mkuu
 
Mwaka 2014 nilipanda kivuko kuelekea kigamboni, pembeni yangu alikaa mtoto mzuri kama mwarabu fulani hivi ana kishepu cha maana kweli kweli, nika msalimia akakausha nikarudia tena mara ya pili akaitikia kinyonge kwasababu ya mwonekano mijdevu, nywele hazijachanwa suruali jeans na tisheti form six chini kiatu tlavota
Nikamuomba namba akaniuliza wewe unaona mimi ni saizi yako! nikamjibu nisamehe.
Baadae mwaka 2014 mwishoni nilikuwa nahitaji mtu wa manunuzi kwa mkataba wa miezi 6 katika project yangu kati ya watu 45 walio apply kuomba hiyo kazi mmojawapo nilimfananisha nayeye.
Niliwaita watu wa tatu na huyu niliye mdhania akiwepo kwaajili ya interview hakuamini alichokiona maana aliponiona alinikumbuka maana ilikuwa ni miezi kama mitatu imepita.
Walifanya interview lakini yeye hakukidhi vigezo hivyo hakupata kazi,
Na alinifuata personally kuniomba radhi na kunishawishi nimpe kazi kwani ana miaka miwili bila ajira sikuweza kupata nafasi.

Mpaka sasa sikuweza kuwasiliana naye tena ingawa mwaka 2017 alikuwa akinitumia sms za salaam kiukweli sikuweza kumjibu mtu akitweza utu wangu huwa nampuuza jumla

WADADA ACHENI MAJIVUNO
Umepoteza bila kummega

Mimi huwa nawamega kwanza halafu natupa kule .

Kuna mmoja hapa saivi ananiletega madharau sana sana sana yaani anakera Ila lazima nimmege kisadi changu kiishe safi
 
Kuna kipindi nilikuwa nafanya kazi kampuni flani.Basi siku hiyo ninetoka kufanya mazoezi ya kukimbia kama kawaida yangu asubuhi.Halafu kipindi hicho mvua ilikuwa imenyesha usiku,Sasa ninerudi pale kazini nikawa nipo napiga story na walinzi zile raba na track zimechafuka balaa.Wakaja wadada wawili na boda boda mi nkaanza kuwasalimia kwa bashasha afu ndo nilikuwa naondoka kujipiga maji.Basi wale wadada wote walinipandisha kuanzia juu hadi chini wala hawakuitikia salam wakanipita wakaenda kwa walinzi,Basi mi nkaona noma nkaondoka zangu.Kumbe wale wadada wamekuja kumuulizia meneja wameleta barua za kuomba kazi na meneja mwenyew ni mimi.Nilivorudi walinzi wananambia wale wadada walikuwa wana shida na wewe wameacha barua zao za kuomba kazi.Nikasema mbona hawajanisubiri wakasema wameona aibu,jinsi walivokudharau.Kesho yake wakarudi kuomba nnamba zangu kwa walinzi mi sikuwepo nilienda mkoani walinzi wakanipigia nikawaambia wapeni tu.Kila mmoja akawa ananipigia kwa mda wake,na wote walichezea rungu ila kazi hawakupata walikuwa wangoni mmoja alidata hadi tukabahatika pata mtoto.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji123]
 
Binafsi nina visa vingi nimewahi kumbana navyo vya kuchukuliwa powa. Hapa nitataja vinne tu.

1.Nakumbuka nilihamia sehemu fulani ofisi flani mahali fulani.
Kwa vile nilikuwa mgeni sikuhama na kitu chochote zaidi ya mi mwenyewe.

Basi nikawa na tabia ya kwenda kula kwa mama ntilie ugali wa buku japo pale jirani kulikuwako na mgahawa mmoja wa kiwango cha juu kwa ajili ya watu wa tabaka la juu .

Wateja wenzangu wengi wao walikuwa bodaboda na machinga. Yule mama ntilie pamoja na wasaidizi wake walikuwa wababe na kauli mbaya kwa wateja wao, kiujumla kwao mteja alikuwa sio mfalme bali lofa.

Jioni moja nikaomba niongezewe mboga kidogo ili nimalizie ugali wangu lakini nilijibiwa kwa jibu la dharau sana mpaka wateja wenzangu wakanicheka.

Tangu siku hiyo nikahamia kwenye mgahawa wa wadosi nikawa nakatiza kwa mamantilie naingia mgahawa wa kishua. Yule dada akawa anapatwa na mshangao kama haamini kama ninauwezo wakula kule.

Lakini pia akaanza kuniona na kampani za watu fulani ambao wanafahamika na ni maarufu eneo lile. Tangu kipindi hicho akawa anajichekesha chekesha kwangu maana alisha fahamu nafasi yangu ndani ya jamii yao ila nashukuru sikuwahi kumshobokea hata kwa salamu.


2 Nikiwa ofisini, kwa vile nilikuwa mgeni, siku moja aliingia mteja ofisini akanikuta nimekaa kwenye meza yenye ya wageni, nilifanya hivyo ili kujipatia mazingira ya urelax kwa assigment niliyokuwa nafanya kwa muda ule. Ili kufanikisha hilo kiti changu na meza yake ninavyotumia kufanyia kazi vilibaki wazi hivyo ikawa kana kwamba mi ni mgeni na boss hayupo maana kiti hakina mtu.
Mara nikaona jamaa amefungua mlango ghafla nakuanza kuuliza bila hata kusalimia. Jamaa akawa ananiuliza huku akinyosha kudole kwenye kiti cha boss " jamaa yuko wapi" nikamjibu "katoka kidogo" Mara nikaona PS anaingia ofisini na kuniuliza "huyu mgeni hajakuona kwani mbona kasema hakuna mtu"? Nikamjibu mwambie aingie.

Basi yule jamaa akaingia ila hakuwa na confudence tena maana alishavurugika kisaikolojia japo nilijitahidi kumjenga kisaikolojia na kumuhuumia vizuri.

3.Siku ingine nafika ofisini nakuta wamama wawili wamekaa kwenye benchi wanamsubiri mwenye ofisi, nikasimama na kawasalima vizuri kwa utulivu, mmoja kajibu kwa kujilazimisha kwa kubetua mdomo yaani ni kama wananishit wanaona nawapotezea muda maana wanamsubiri boss wamweleze kilio chao. Basi nikaingia ofisini kidogo kama dk 3 kisha nikatoka nnje mara nikasikia PS anawambie " nyie mbona hamwingii?, anaondoka huyo! Mara nasikia kwa nyuma watu wananikimbilia huku wanaita kwa sauti za unyonge" baba samahani tunashida na wee! Nikasimama na kuwaomba twende ofisini tuongee. Niliwahudumia vizuri japo walisha potewa na confidence maana nafsi ziliwasuta maana waliuchukulia poa mwonekano na umri wangu nadhani.


3. Juzi kati nilipanda basi kuelekea mkoa fulani. Kwa vile nilipandia njiani nikapata siti jirani na dada wa makamo bonge. Nikamsalimia vizuri ila hakuitikia kwa kutoa sauti bali akatikisa kichwa tu . Baada ya mwendo wa safari ndefu, nadhani mdada alinisoma na kugundua alini underate kwa makosa. Basi akaanza kujitahidi kuniongelesha mara ooooh, "samahani kaka eti hapa ndo wapi," ooooh, "kaka hivi we ni mwenyeji ............"(anataja jina la mji tunaoelekea) Sikumshobokea , nami nikawa namjibu kwa kutikisa kichwa tu huku niko bize na simu yangu.

4.Juzi nimehudhuria harusi ya jamaa yangu. Nilikuwa peke yangu kwa vile wife alikuwa na udhuru.
Basi nikaelekezwa kwenye meza moja ambayo tayari ilikuwa na wenza wawili (umri kati ya 30 na 35) Basi nikawasalimia kwa sauti huku nikivuta kiti na mie nikae. Yule mdada aliitikia lakini mwanaume hakuitikia.

Ukaja muda wa kugobganisha glasi kila mtu na jirani yake , kwa vile nilikuwa sina mtu mingine zaidi yao nikagonganisha nao glasi lakini naona yule mkaka kama hataki . Ok, shughuli ikaendelea naona jamaa yuko bize na kushikana shikana na mpenzi wake nami niko bize na simu yangu.

Tumekula chakula tumemaliza mi sikuwa na haraka ya kuondoka ukumbini maana nilikuwa bado namalizia kinywaji changu. Basi baada ya kumaliza kula naona msela ananyanyuka anamvuta demu anamwambia "twende zetu acha hiyo" demu akaiacha redbull ambayo ndio kwanza ameifungua. Kwa vile tulikuwa mimi na wao pale mezani nilitarajia angalau " broh sie ngoja tutangulie"!

Bada ya kama dk 15 namimi nikatoka ukumbini ili nirudi home maana ilikuwa yapata saa 7 za usiku. Nafika karibu na parking, nawakuta wale mtu na demu wake bado wapo kumbe wanasubiri bodaboda huku wakipata adhabu ya kipupwe cha usiku . Nikawapita kwa karibu, nikaingia kwenye usafiri wangu nikawasogelea nikashusha kioo kidogo na kuwaaga "jamani mi natangulia, naona nyie bado mpo". Sijui kama walijibu ama la ila nilichogundua niliona msela amekosa confidence na amekuwa mnyonge saana.


Yawezekana kuwa na madhaifu ya kibinadamu ila kujisocialize na watu bila kujali hadhi zao ni faida kwako kuliko hasara.
 
Kuna shida hapo either unashindana na wanaume uonekane mko sawa. Na ilhali unakojoa umechuchumaaa na mwanaime amesimama. Yaani hautaki kukubali kuwa mwanaume yuko juu yako. Labda ka elimu ulikopata kanakupa ujasiri na unajiona kama laweza kuoa mwanaume.

Yaani sijui kama utadumu na mwanaume .
Labda uoe umuweke mjini ila ukiolewa sidhani
Am sorry ila ni mtizamo wangu.

Tukiamua kukojoa huku tumesimama inawezekana.

Wazee wa zamani walikuwa nasimama zao..... LoL
 
Nilikaribishwa na binamu zangu me nikaenda, kufika nikakuta wageni ambao ni mama yao mkubwa na mama mdogo, mdogo wao pia mzazi mwenzie yule me mkubwa. Kuna wanaonijua pale na wengine hawanijui Ila wananisikia. Baada ya kutambulishwa hakuna aliyenijali kabisa hadi nikajisikia unyonge yaani ni wale vijana ndio walinihudumia kila kitu hawakuwa na muda na Mimi kabisa hao ke. Ikapita kama mwaka mmoja hivi dogo akataka kuoa wakafanya kikao kwa mama ya mdogo Mimi sikwenda niliwaambia chochote watakachohitaji nitatoa Ila sitofika hapo, baadae muoaji akaniomba harusi iingilie nyumbani kwangu baada ya wiki mbili watakwenda kwenye chumba chao nikawakubalia. Ikawa kila akiulizwa swali bwana harusi mtarajiwa anajibu nitamuuliza dada X. Ikabidi wamwambie huyu X aje hapo atudhirishie kama kweli yeye atabeba mzigo huo na haya mengine unayoyataja, akanipigia simu palepale nikajibu Jumamosi ijayo nitakuja kweli nikaenda nikaulizwa yote nikakubali. Nikawaelekeza kwangu hivyo wakaja tukafanya harusi wakaondoka [emoji3][emoji3][emoji3]. Kuanzia hapo heshima juu. Maana wote walihudhuria, kubwa na Kali yule aliyekuwa ananipandisha na kunishusha siku iso na jina akanieleza matatizo yake ya ugonjwa nikamugharamikia. Hadi sasa heshima juu. Nashukuru simdharau mtu ila napenda kuwa mkweli na sijutii hilo, hivyo jibu langu mtu anaweza fikiri nimemdharau
 
Sh
Binafsi huwa sipendi MTU anayependekeza salamu. Ujue salamu ni aina ya malipo ama kumnunua MTU moyo wake ili akusaidie kitu Fulani. Ina mana bila ya salamu husaidiwi.
MIE hata ukinipita bila ya salamu afu unarudi umepotea njia nakuelekeza kiroho safi na hata ukinisalimia kama kuninunua ili ndipo nikuelekeze MIE naipotezea salamu yako na kama Nina muda nakupeleka mpaka unakoenda.

Warusi ukiwauliza kitu afu wakakusaidia na ukiwashukuru wanaikataa shukrani yako kwa kuuliza ya nini iyo shukrani. Ina mana wako willing kukusaidia bila hata kuwalipa.

Sasa bongo ndipo utashangaa MTU anakomalia salamu utadhani itamuwekea chakula mezani.

Binafsi sipendi kusalimiwa naonaga kama ni utumwa Fulani yaani ni lazima usalimie kila asubuhi. MIE wangu aishanielewa hakuna salamu hata kama nikitoka kwa wiki nzima. Nikirudi unapita muda kidogo tunaanza story za huku home na huko nilikokuwa.

Wazazi wangu hawakuwa watu wa kudemand salamu kila siku asubuhi. Ilikuwa ni kuamshwa kuwahi shambani basis.
Mpaka umri huu huwa nikienda home salamu ni zile siku za ugeni wiki ikishapita hakuna salamu.

Pia siamini kuwa salamu ndio heshima.

Nina imani masikini anapenda sana salamu mana kwa njia hiyo anajisikia faraja sana anadhani naye anajariwa. Masikini ndiye anayetembelea ndugu zake waliofanikiwa na kuwaongelea na kuringishia watu. Kuwa usinidharau yule karibu mkuu ni mdogo wangu nimemsomesha MIE. Ni kama Mwita weitara akasomeshwa na kaka yake aliyekuwa nauza mayai hapo kipunguni saivi sijui wanakaa kivule.
Ni mfano tu nimetolea hapa kwa karibu mkuu.

Salamu ni muhimu ila isiwe lazima jamani .yaani kuna watu wanaifanya kuwa basic needs kwao.
Binafsi nikiwaga home kwetu huwa siishi kwa furaha mana kila unayepishana naye yabidi u pay attention kwake na umpatie salamu tena usimame mpige story kidogo.sasa ole wako uje upite usalimie ukipunga mkono nakuambia ,Fulani anaringa kisa akasoma ,ama ana Hela.

Ila nikiwa town salamu sio lazima naishi kwa Uhuru hakuna MTU anayejiliza kuwa umetupita bila ya salamu rafiki.

Binafsi kunyenyekea ama kunyenyekewa sipendi.

Haya shikamooni wana jf wote waliozaliwa 65 kurudi nyuma. Wa 66 mpaka 1990 mambo vipi. Waliozaliwa 90 mpaka 2020 mnipe heshima Yangu

Unadhani kwa salamu Umepata nini katika maisha yako hata nisingekusamia si ungebaki na shida zako zilezile ama kuna kitu kimeongezeka.


Binafsi I hate salamu ingawa ni opener ya maongezi. Kuna watu naowakubali sana binafsi unamuuliza MTU kitu anakujibu mwishoni unashukuru na kumpatia salamu yake unasepa. Watu wa ivyo huwa naowanga ni matajiri rohoni kwao ni matajiri rohoni mwao!!!!!
Shikamooo brother
 
mtu mmoja hivi anamiliki hisa nyingi zaidi eFM media.
Namuonagaonaga hivi kama Hisa anazomiliki huyo jamaa zinaweza kuwa na thamani gani kwa pesa, au utajiri wake unaweza kuwaje maana radio naichuliaga poa.

Naomba eleza kama unajua.
 
Kwanza naomba 'nidiclee' kwamba mm ni mmoja wa ME ambae si mtu wa fashion, yani mimi sijui kuvaa kabisa na sina hiyo passion ya pamba pamba. Nishawahi kusemwa sana na ma-ex wangu kuhusu uvaaji wangu lakini haikusaidia kitu.

Sasa weekend iliyopita nilienda sehemu moja flani hivi amazing, chimbo la uhakika haswaa, limejitenga na limetulia kweli. Nilipigilia kipensi changu na ka t-shirt flan hivi local nikachagua sehem nikakaa, kutizama vizuri nikaona kuna meza amekaa mdada mmoja hivi and of coz she is gud looking nikaamua kujitosa angalau kumpa hata hi 'coz tulikuwa wateja 2 tu, nikamfata nikamsalimu.

Yule dada kwanza alinishusha kuanzia juu mpaka chini then akaitikia salamu yangu ki-design kama namsumbua flani hivi. Nikaomba kujumuika nae kama asipojali. Jibu lake ndo lilinitoa confidence kabsa, alinambia: "Kwahiyo kaka unadhani kila msichana akikaa peke yake anahitaji kampani? Hapana sihitaji" Dah, mwanamme nikajizoazoa pale nikarudi nilipokaa. Nilikaa kama masaa ma3 hivi nikaamsha zangu. Sasa kilichotokea jana ndo kimenifanya niandike huu uzi.

Nilipokea maagizo kuanzia J3 ya wiki hii kuwa leo watakuja watu wa Taasisi flani ya kifedha kutoa semina kwa sisi wafanyakazi kwa ajili ya kutushawishi kujiunga na huduma za Taasisi yao, hivyo mimi nikapewa jukumu la kuwakaribisha na kuwapeleka sehemu ambapo semina itafanyika.

Asubuhi mida kama ya saa 3 hv ugeni ukafika, walikuwa watu kama 7 hivi, kati yao alikuwepo yule dada nilieonana naye weekend.

Wakaingia ofisini nikawakaribisha, wakati mkubwa wao anatoa introduction macho nikayakaza kwa yule dada, bahati nzuri tukagonganisha macho, akashtuka flani, nikajua kashanikumbuka.

Baada ya semina kuisha ikafika kipindi cha watu kujiunga sasa kwa walioshawishika. Nikamfata yule dada nikamuomba aje anielekeze namna ya ujazaji fomu. Alivyofika tu, nikamuuliza "Unanikumbuka?" Akachekaaa, akaniambia "Yani wewe, sikutarajia kama unaweza kuwa unafanya kazi huku", nikamuuliza ulitarajia niwe nafanya kazi wapi? Akaishia kucheka tu. Mawasiliano yake kanipa; fresh bila shida kabisa.

Sasa naomba kuuliza wadau, mshawahi kukutana na situation ya namna hii?
Swali, Umeshapiga????
 
Back
Top Bottom