Englishlady
JF-Expert Member
- Apr 11, 2013
- 2,736
- 3,644
Juzi tu NMB Dodoma:
Jamaa flan kavaavaa tu afu na midevudevu hivi
Kaenda NMB ATM kakuta na wadada wa benki wameweka meza ya kutoa huduma kwa wateja pemben hapo. Akafika tu kauliza (bila hata kusalimia).....kwanini kadi yangu inakataa kuniunganisha NMB mkononi
Dada kamjia juu...."kwanza salimia;...vipi habari za huko,...haya tukusaidie nini??"
Jamaa hakupokea. Mie nawaangalia tu.
Dada karudia tena ...."vipi mzima mwenzetu?? Za ulikotoka??!.....mbona umekuja kasi sana??!"....
Jamaa anaeaangalia tu. Mara akauliza...."ivi ni lazima kusalimia/ au kupokea salam ya mhudumu ili nipewe huduma NMB???...
Wakaanza kumshangaa ..."unatokea wapi wewe, yani unakuja kuvamia tu bila kusalimia..." ....wamamzodoa flan.
Jamaa akaingia Benki ndani. Straight kwa Meneja. Nafkiri hakueleza shida aliyopata nje. Alimueleza tu kama kutaka kusaidiwa shida yake. Sijui ndani waliongea nini??
Wametoka na meneja...hadi pale ATM kwenye meza ya wale wadada....meneja akiwa kashika mkononi kadi ya yule mshua....akawambia wale wadada mmoja wao (sikumbuki jina)...
Meneja: .....hebu msaidie Katibu Mkuu hapa kumuunganisha na NMB Mkononi...(Meneja akaongeza:....mkuu hapa utahudumiwa)...mara meneja katuomba wote wa kwenye foleni ya ATM..."naomba ndugu tumpishe kiongozi anajambo kidogo kwenye ATM ...samahani"...wakaingia ATM meneja, mshua na yule dada.
Wakafanya mambo humo ...kidogo wakatoka. Tukaendelea.
Meneja akamsindikiza yule mshua hadi kwenye gari akaondoka meneja anapunga mkono.
Niliwaangalia wale akina dada mavi yalivyowagonga chupi. Walitoa macho sana wakawa na wasiwasi mkubwa....
Walimchukulia poa
Lakini kwa ubinadamu wetu salamu ni muhimu sana...huyu katibu mkuu si muungwana hata kidogo.
Hawakuwa na sababu ya kuogopa, hawakufanya kosa lolote