Ushawahi kuchukuliwa poa na mtu halafu akakuta sivyo kama alivyokudhania?

Ulichokiongea ni kweli,nipo hapa Makambako,yote hayo nayashuhudia,watu hawafanani na pesa wanazomilimi,hawana kabisa mpango wa kupendeza.
 
Mkuu salamu ndiyo ilimfanya muoji asitishe kuowa, kisa tuu miongoni mwa watu aliongozana nao alikuwepo kaka yake sijui baba yake mdogo, basi kufika kule kwa yule binti wakakutana na kaka wa yule binti akawasalimia mambo vp wazee basi ndugu yake jamaa alimind na akamshauri usiowe huyu mwanamke basi mwenzangu na mimi ilibidi atii amri, ila ukiangalia salamu ya mambo vp ndiyo chanzo. Na alikua kampa mimba mtoto wa watu
 
Hao huwa wanatumwa ku deposit hela za maduka makubwa au ya jumla wala sio matajiri. Kama unaenda sana benki utawaona wengi tu hata waswahili usitishike mkuu wametumwa hao.

Na ni kweli hata mim siku nikijisikia hupeleka pesa za kampuni [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kila mtu kaandika ya kwake ngoja na mimi niandike ya kwangu kipindi ninemaliza form 4 mkoa fulani nikaenda mkoa mwingine kuna ndugu zangu nimekaa pale ndugu yangu kafungua banda la mkaa nikasema ngoja nikae hapa niuze basi watu wanakuchukulipia poa sana km muuza mkaa huna jipya.mara tokeo limetoka huyo advance then chuo ila watu wengi mtaa ule hawakujua harakati zangu baada ya mkaaa maraa eeeh nikapata field karibia na mtaani pale pale kuna shirika la uma nikaa kitengo matata full upepo kwa hiyo wale waliokuwa wananiona muuza mkaaa walikuwa hawaamini kinachoendelea


Funzo usimdharau mtu kwa muonekano
 
Atakuwa mshirikina sio bure.
 
Jamani muache uchafu.Tutakuja kulaumiana bure.
 
Swala la kutokidhi vigezo ni sawa...ila kama uliumia nakukataliwa pia.
 
So anajuta kua kapoteza nafasi ya umarioo?
Lazima ajute mkuu, hata mimi ningejuta pia,
Kimsingi yule dada alikua mdogo na jamaa umri umeenda na maisha yanazingua utaachaje fursa kama hiyo?

Wakati mwingine sio lazima mwanaume ndio amuinue mwanamke hata mwanamke anayo nafasi ya kumuinua mwanaume kama fursa ipo.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hivi mnazungumzia uchafu, Muonekano wa asili au kuvaa kinyume na mazingira?

Hili la mwisho ndio changamoto yangu, tisheti, jeans na raba halafu naingia popote hivyo hali inayopelekea nionekane ujana mwingi

Na mimi nasema nafanya nachopenda
 
Kwa vile yeye ni katibu mkuu ndio asisalimie? Alishindwa nini kusalimia, kujitambulisha na kuomba huduma? Tujenge utamaduni wa kuheshimu kazi za watu wakiwa maofisini kwao hata kama umewazidi cheo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…