Ushawahi kuchukuliwa poa na mtu halafu akakuta sivyo kama alivyokudhania?

Ushawahi kuchukuliwa poa na mtu halafu akakuta sivyo kama alivyokudhania?

Eti muheshimiwa we ulisikia wapi Mwanamke anatafuta mwanaume amuoe[emoji23][emoji23]
Yaani nimejikuta nachekaaa [emoji23][emoji23][emoji23]
Jinsi ulivoandika kwa hisia,

Usichokijua ni kua zaidi ya 50% ya ndoa ushawishi mkubwa hutoka kwa mwanamke, eidha wa moja kwa moja au kimazingira
Nafikiri waliokua wanakuambia utafute walimaanisha utumie mbinu hiyo.
 
Strategy without tactics is a slowest route to victory

nipe mbinu mkuu[emoji23] maana sina ushawishi nahisi, japo mipango ya Mungu pia inachangia
 
Mimi kuna siku tena ni zaidi ya mara moja inanitokea, mara ya kwanza ilikuwa pale nje ya wizara ya ardhi niliegesha gari pembeni nikanunue gazeti narudi nakuta wale majamaa wamelifunga.
Nikaanza zozana nao wao jibu wanalonipa kamwite mwenye gari. Yani kila nalowambia wananiambia mwenye gari atalipa we unahangaika nini kamwite mwenye gari, dah ila mwisho nikampa 20,000 akalifungua nikasepa.
Mara nyingine nilikuwa pitiliza mataa wakati taa zimezuia, kumbe mbele kuna traffic, akandaka. Akaanza kunisngekuwa na boss wako usingefanya hivi na maneno mengi. Baadae, akaniomba leseni na kadi ya gari nikampatia akakuta kadi ya gari ina jina sawa na leseni. Akasema kumbe gari lako nikamjibu ndiyo, akaishia kucheka akasema yani watoto wa kishua bwana mnakula maisha kwa pesa ya baba zenu. Mimi nikacheka tu akaniandikia faini nikasepa huku nikiwaza ungejua mimi mpambanaji tu.
Mara nyingine niliacha gari lilikuwa na matatizo na mimi nina haraka nikalipaki pembeni ya barabara nikachukue boda boda, kumbe huku nyuma askari wakapita lipo, wakapita tena lipo ikabidi watanaze times ambaye katelekeza gari akalichukue mimi sikuwa na habari. Narudi baadae kulichukua nikiwa na fundi, gari silioni, namuuliza muuza matunda ndiye akaniambia wamelibeba wamelipeleka kituo cha polisi cha kawe. Kesho yake naenda kawe mkuu wa kituo akawa ananizngua kuwa nikamtafute mwenye gari, mpaka nilipofungua nikamwonyesha kitambulisho na kadi ya gari majina yana match. Aliniambia tu niwalipe waliolivuta nisepe tu.
Yani mimi nina mwili mdogo kama wa Mrehemu Ruge Mtahaba, nakutana ma mazarau sana maana hata nikivaa suti haikai ni kama imetundikwa tu.
Pole sana mpambanaji
 
Strategy without tactics is a slowest route to victory

nipe mbinu mkuu[emoji23] maana sina ushawishi nahisi, japo mipango ya Mungu pia inachangia
Mikakati bila mbinu shirikishi inachelewesha ushindi,

Mbinu kuu ya kwanza ni aina ya mtu uliekuanae kwenye mahusiano, unaeza kua na mtu unaemjua A to Z na wajua kabisa hatufiki mbali lkn kwa sababu zenu bado hutaangalia pengine, mpo tu

Mbinu zipo nyingi sana inategemea na mtu uliekuanae, kikubwa zaidi ya vyote ni tabia, uzuri halisi wa kuzaliwa, mavazi na kujiremba haudumu kwa mwanaume ambae ushamvulia chupi zaidi ya miezi 6, baada ya hapo anakuona wa kawaida sana utofauti unakuja kutokana na tabia utakayoonyesha baada ya kugegedana.

Mfano mimi nilijisemea nkisharidhika na tabia sitaoa mwanamke kabla hajabeba mimba kwanza, hapo kuna mwingine yupo bize kumeza dawa au kuchoropoa unamchora tu asijue target yako ndio hiyo. (mfano tu huo usije ukaachia ya mtoto [emoji23], hatufanani)

Ila kikubwa ni aina mahusiano na marafiki pia wanachangia sana wee kuonekana ni mtu wa aina gani.
 
nmefunga dirisha la usajili[emoji23]
[emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] Usajili wangu ni kama wa Morrison kwenda simba sc, ukinisajili tu basiii umelamba dume.
 
Wengi sana mko ivo,

Mfano kuna wadada wa3 wanafanya kazi duka la jirani na kabiashara kangu sasa ofisi yao ilihamia siku za karibuni mwezi wa 5, yaani walikua na dharau hata salamu hawatoi sa ingine, ukiangalia wanavyovaa vizuri utasema ndio wenye duka..... Kumbe wanalipwa ela ndogo sanaa hata kula yenyewe wanajibana wakati mwingine wanajichanga wanakula miogo na maji
Sasa walivyojua kabiashara ni kangu basi kila mmoja kwa wakati wake anajipendekeza kiaina mi wala sina noma nimechangamka tu
Sasa mmoja kaja tu anajichekesha na utani nimnunulie saa, nkatafuta ya mda mrefu ishachoka kiaina nkampa.
Ila nilishakaa nao nkawasema kuhusu hiyo tabia yao, nkawaambia unawejikuta unamletea nyodo boss wako wa kesho au mmeo bila kujua, wananiheshimu sana sa hivi

Kuna wanawake wanaringa jamani acheni tu. Hata wanaume pia wapo.

Kuna wadada wanaringa utadhan hawaendagi chooni kukata gogo Samboko
 
KISA CHA KWANZA
Maji pwaaaa..nikasikia unatembea tembea tu huangalii.Msonyo wa haja.

Ikapita miaka mitatu nipo kwa Mama Mkubwa nasikia Mlango unagongwa,naambiwa kafungue umsikie huyo anayegonga.

Hahaha aliyenimwagia maji miaka mitatu iliyopita..

Bila yeye kujua kuwa Bro anayemtafuna ni ndugu yangu wa damu.Basi nikamkaribisha ndani bila taaabu..Nikaenda kumwamsha mwamba nikaawaacha hapo sebuleni.

Sasa kwenye ile Nyumba mimi ndio maarufu kila kona.Bro hakai dakika dogo sikia ule mzigo sijui ufanye hivi tusepe.

Basi Shemeji akaaga ooh naondoka nawahi.Wamefika nje anamuuliza Bro huyu ni ndugu yako?Anaambiwa hiyo ndio roho ya mama yangu bwana huyo kama Alfa na Omega kwa mama.

Naomba uniombe msahamaha ,nilimwagia mdogo wako maji machafu tena sikumuomba msahama ni siku nyingi sana.

KISA CHA PILI.

10 Years ago

Nimechafuka mbaya juu ya dali nikiwa nahangaika na Cables(CAT 6) ile nimeshuka nakutana na wahusika wa eneo wapo na jamaa flani.Mkuu wa pale akanisalimia kwa furaha sana pole kijana wangu.
Nawasalimia washikaji wakanyamaza kimya,nikarudia tena wakuu habari.Kimya ,..yule Boss wa eneo lile akacheka akatia neno la kutoa ile Kadhia.

Baaadae walikwama kufanya issues zao Remote Access na WIFI passwords.Mkuu akawaambia ngoja niwapeleke kwa wenye mambo yao.Tena anasema daah kijana huyu atawasaidia kwa haraka sana hana shida maana ndio wamefanya hapa pawe pa Kisasa kwa sasa.

Na ikawa hivyo..nikafanya kilichoombwa kwa utulivu maana ilikuwa Project yao muhimu sana.

Wakaja kujua mpaka walipo fikia kulala kwenye nyumba za wageni control zote ninazo kiganjani.

Meza ya kulia ni moja na tunakutana mida yote ya chakula.

😀 😀 😀 😀
Mmoja wao ndio anasema daah Mkuu unaonekana una mambo mengi sana kwa kichwa hata hufanani nayo kabisa.

Uzuri waliomba msamaha hawakuamini kama nimesamehe japo tumekuwa marafiki kwa sasa.
 
Huyo katibu mkuu nae atakuwa siyo mstaarabu tu. Kusalimia watu kwake ni shida? Ni mmoja wa wale waliolewa madaraka.
..Kweli Mkuu. Huyu Karibu Mkuu naye hakuwa muungwana. Kwani Ukatibu wake ndio unamfanya asisalimie Watu?
Huyu in amina ya wale Viongozi ambao cheki yako ya malipo yako inayohitaji Saini yake tu inaweza kukaa mezani kwake hats mwezi mzima akitaka umlambe miguu kwanza! Ni Shiidra![emoji35][emoji35]
 
Mimi imenitokea hii:

Niliweka tangazo kule love connect kuwa 'natafuta mke ' sio kuwa amepotea - hapana; yaani lengo langu nivute jiko niweke ndani.

Wakati naandika tangazo nilikuwa na asilimia 100 kuwa JF imesheheni wadada wasomi na wanaojielewa. Natambua kuwa wapo wasomi hadi kufikia level ya PhD lakini Diploma + bachelor na masters wapo wengi mno. Jamani msiwadharau wadada wa humu wengi ni wasomi na wana kazi zao za heshima mnoo.

Kwenye sifa zangu: nimesema mimi ni mweusi, mwembamba na elimu yangu ni darasa la saba😃😃😃

Aiseee yaani wadada wa Jf wote waliopitia tangazo langu hata wale wenye uhitaji kama mimi na sifa wanazo; wote wamenidharau wamepita kimya kimya. Huwezi amini; hadi leo hii sijapata pm hata moja😂😂 kweli hakuna wa kunifaa?, nahisi nadharaulika kwa hii elimu yangu ya darasa la saba😂😂.

NB: najua tatizo ni elimu yangu ya darasa la saba , na wadada wengi jf ni wasomi wa hali ya juu - form four hadi mbele huko PhD .
Jamani pamoja ni darasa la saba lakini ninatafuta mke jamani, kuwa mimi la saba sio ishu jamani.
Hadi leo hii bado wamenidharau na wala sijapata PM ya kumpata mwanamke wa ku-anzisha nae familia pamoja.

Bado nafasi ipo wadada jamani ...acheni kutudharau sisi darasa la saba.
 
Wanaume mnaolalamika wanawake wanawadharau, sasa, kama umevaa na kukaa hovyo unategemea nini?
Mbona hamshobokei wanawake walio hovyo kama ni kweli hamtilii maanani outward appearance? Mjitafakari
Kingine, inaonekana tunashida kubwa kwenye maadili yetu. Kwanini tunaambizana ya kuwa tunatakiwa tuheshimu watu wote kwasababu anaweza kuwa na kazi nzuri au unaweza kupata shida akakusaidia nk? Kwanini tusifundishane kuheshimiana kwa upendo kutoka moyoni kuliko kutishana? Hi ndio sababu tunakua wanafiki na chini kwa chini tunachukiana.
Mimi binafsi uwe muokota machupa jalalani au meneja wa wapi, nita watreat sawa bila kujali chochote. Ndio maana kwa watu wenye position kubwa au wanaotegemea special treatment kutoka kwangu wananiona nina dharau, ili hali wale watu wanadharaulika na jamii wananiona sina shida yeyote.
Kuhusu kudharaulika kwasababu ya muonekano wa nje, sijawahi. Sana sana watu wakiniona matarajio yao yanazidi hata uhalisia wangu. Lakini watu wengi, hasa wanaume wananiona nipo shallow kichwani (sexism). Wanahisi siwezi kufanya maamuzi magumu, kuchanganua mambo, kutetea hoja au kuwa na skills kwenye male-dominant fields. Wanahisi nipo kama pambo na nikiwaprove wrong kuna wanaofurahi na kuna wanaonichukia na kunipiga vitu kwa nguvu zao zote.
Maneno mema mpendwa Wordsworth. Haya, Mimi biashara yangu ni kuchoma Mkaa huku Msitu wa Pande.
Nimekupenda na ninaomba tukutane pahala tutete na tuyajenge...[emoji5][emoji5]
 
Kuna siku nipo nilikuwa sina kazi nyingi ofisini nikatoka nje hivi nikamweleza PA wangu nipo nje nachukua Juice Fresh kutoka nje kuna gari limeingia Parking kwa speed kidogo liniingie miguuni jamaa hawakuwa na hekima walinitusi Mpuuzi wewe...nimerudi Ofisini naambiwa na PA wangu Meneja kuna wageni wako nikawaruhusu waingie nakuta wale jamaa walionitusi nikawakaribisha na sentensi fupi 'Karibu ABSA' wanageuzageuza nyuso zao hawajui waanze vipi.
Wangari Maathai njoo msikilize bosi hapa
 
[emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] Usajili wangu ni kama wa Morrison kwenda simba sc, ukinisajili tu basiii umelamba dume.
Umeshakosa kama mfano wenyewe ndo morrison
 
Mikakati bila mbinu shirikishi inachelewesha ushindi,

Mbinu kuu ya kwanza ni aina ya mtu uliekuanae kwenye mahusiano, unaeza kua na mtu unaemjua A to Z na wajua kabisa hatufiki mbali lkn kwa sababu zenu bado hutaangalia pengine, mpo tu

Mbinu zipo nyingi sana inategemea na mtu uliekuanae, kikubwa zaidi ya vyote ni tabia, uzuri halisi wa kuzaliwa, mavazi na kujiremba haudumu kwa mwanaume ambae ushamvulia chupi zaidi ya miezi 6, baada ya hapo anakuona wa kawaida sana utofauti unakuja kutokana na tabia utakayoonyesha baada ya kugegedana.

Mfano mimi nilijisemea nkisharidhika na tabia sitaoa mwanamke kabla hajabeba mimba kwanza, hapo kuna mwingine yupo bize kumeza dawa au kuchoropoa unamchora tu asijue target yako ndio hiyo. (mfano tu huo usije ukaachia ya mtoto [emoji23], hatufanani)

Ila kikubwa ni aina mahusiano na marafiki pia wanachangia sana wee kuonekana ni mtu wa aina gani.
mimba sikuhizi ni qualification kubwa[emoji45][emoji45]
Kwahiyo mwanamke yoyote tu akishika mimba ndo mkeo jumla haihitaji mambo mengine!!!??

Basi wenye vizazi vya Makha ndoa tutaziskia kwa bomba
 
Mimi imenitokea hii:

Niliweka tangazo kule love connect kuwa 'natafuta mke ' sio kuwa amepotea - hapana; yaani lengo langu nivute jiko niweke ndani.

Wakati naandika tangazo nilikuwa na asilimia 100 kuwa JF imesheheni wadada wasomi na wanaojielewa. Natambua kuwa wapo wasomi hadi kufikia level ya PhD lakini Diploma + bachelor na masters wapo wengi mno. Jamani msiwadharau wadada wa humu wengi ni wasomi na wana kazi zao za heshima mnoo.

Kwenye sifa zangu: nimesema mimi ni mweusi, mwembamba na elimu yangu ni darasa la saba[emoji2][emoji2][emoji2]

Aiseee yaani wadada wa Jf wote waliopitia tangazo langu hata wale wenye uhitaji kama mimi na sifa wanazo; wote wamenidharau wamepita kimya kimya. Huwezi amini; hadi leo hii sijapata pm hata moja[emoji23][emoji23] kweli hakuna wa kunifaa?, nahisi nadharaulika kwa hii elimu yangu ya darasa la saba[emoji23][emoji23].

NB: najua tatizo ni elimu yangu ya darasa la saba , na wadada wengi jf ni wasomi wa hali ya juu - form four hadi mbele huko PhD .
Jamani pamoja ni darasa la saba lakini ninatafuta mke jamani, kuwa mimi la saba sio ishu jamani.
Hadi leo hii bado wamenidharau na wala sijapata PM ya kumpata mwanamke wa ku-anzisha nae familia pamoja.

Bado nafasi ipo wadada jamani ...acheni kutudharau sisi darasa la saba.
Wewe sio darasa La saba kwa jinsi uandishi wako tu ulivyo

hebu waombe radhi wa PhD wenzio
Ili mketi meza moja.

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom