Mimi kuna siku tena ni zaidi ya mara moja inanitokea, mara ya kwanza ilikuwa pale nje ya wizara ya ardhi niliegesha gari pembeni nikanunue gazeti narudi nakuta wale majamaa wamelifunga.
Nikaanza zozana nao wao jibu wanalonipa kamwite mwenye gari. Yani kila nalowambia wananiambia mwenye gari atalipa we unahangaika nini kamwite mwenye gari, dah ila mwisho nikampa 20,000 akalifungua nikasepa.
Mara nyingine nilikuwa pitiliza mataa wakati taa zimezuia, kumbe mbele kuna traffic, akandaka. Akaanza kunisngekuwa na boss wako usingefanya hivi na maneno mengi. Baadae, akaniomba leseni na kadi ya gari nikampatia akakuta kadi ya gari ina jina sawa na leseni. Akasema kumbe gari lako nikamjibu ndiyo, akaishia kucheka akasema yani watoto wa kishua bwana mnakula maisha kwa pesa ya baba zenu. Mimi nikacheka tu akaniandikia faini nikasepa huku nikiwaza ungejua mimi mpambanaji tu.
Mara nyingine niliacha gari lilikuwa na matatizo na mimi nina haraka nikalipaki pembeni ya barabara nikachukue boda boda, kumbe huku nyuma askari wakapita lipo, wakapita tena lipo ikabidi watanaze times ambaye katelekeza gari akalichukue mimi sikuwa na habari. Narudi baadae kulichukua nikiwa na fundi, gari silioni, namuuliza muuza matunda ndiye akaniambia wamelibeba wamelipeleka kituo cha polisi cha kawe. Kesho yake naenda kawe mkuu wa kituo akawa ananizngua kuwa nikamtafute mwenye gari, mpaka nilipofungua nikamwonyesha kitambulisho na kadi ya gari majina yana match. Aliniambia tu niwalipe waliolivuta nisepe tu.
Yani mimi nina mwili mdogo kama wa Mrehemu Ruge Mtahaba, nakutana ma mazarau sana maana hata nikivaa suti haikai ni kama imetundikwa tu.