Tokea hii itokee zimepita Kama wiki tatu hivi....
Baada ya kumaliza chuo huku ajira zikiwa ni ndoto za Abunawasi Kama sio Alinacha, mzee wangu aliamua kunipiga tafu ili tusije kulaumiana huko mbele. Alifumba macho akavunja kibubu akanunua trekta jipya "Massey Ferguson 275" likiwa na tela pamoja na majembe yake halafu akanikabidhi funguo na kadi na kuniambia Kama ninataka mali nitazipata shambani.
Katika kusubiri msimu wa kwenda kuzitafuta mali shambani nikaamua kulipeleka trekta kijijini kwetu maana sio mbali ili niwe nawabebea watu mizigo. maisha ni kujiongeza shekhe! Alhamdulillah, kazi inaenda vizuri hasa ukizingatia suka mimi mwenyewe! Sometimes hata mshua mwenyewe akishirikiana na mama huwa wananipiga mzinga, nawatoa kiroho safi. Kimsingi hata zile text za "Baby nikuambie kitu" siziogopi huwa nazijibu pasina shida yoyote!
Last week nilipata dili la kubeba tofali. Wakati wapakiaji wanaendelea na kazi ghafla Kuna jamaa alikuja pale site akiwa na mwanamke! Walikuwa wamependeza wenyewe, wanawaka hatari na jua lile la utosi wananukia marashi tu. Mikogo yao ilitosha kuonyesha wapo kwenye lindi la huba na mahaba yasiyoelezeka.
Wakafika pale huku wanajipukuta vumbi kwa leso, site hapataki utanashati. Basi jamaa akalitazama trekta Kama traffic anayetafuta kosa, halafu bila hata salamu japo sio lazima akaniuliza linabeba gunia ngapi za mahindi, nikamtajia gunia 35. Akatikisa kichwa kuonyesha ni uwezo mdogo sana! Mbulumundu kabisa, wakati Kijiji kizima trekta langu ndio kubwa na linabeba kuliko wengine wote! Kwanza kijiji chote matrekta yapo matatu tu na langu ndio King of the empire! Nilimvumilia maana mteja sio fala ni mfalme.
Basi akajinyonganyonga pale, akajishingondoa paleee, akajimwemwesa kwa pozi za ashuo mbele ya demu wake halafu akauliza gharama za usafiri, nikamtajia. Akasema,
"Eeh... dogo mbona unapiga sana, bosi wako anajua lakini?" Achana kwanza na ishu za bosi, kwanini aniite dogo tena mbele ya demu wake hasa ukizingatia bei niliyomtajia ni very reasonable? Why? Why always me!
Mjinga aliniharibia siku, shubamiti! Akaongeza chumvi kwenye kidonda,
"Kama vipi nipe namba ya mwenye trekta niongee nae maana nyie madereva huwa mnazingua Sana!" Itoshe tu kusema yule jamaa aliondoka kwa dharau huku akisapotiwa na demu wake! Nilipoteza pambano na sikujisikia vizuri.
Wale wanaopakia tofali ndio wakaniambia kuwa jamaa na demu wake wote ni walimu wa shule ya msingi hapo kijijini. Wanavimba sababu wamesoma. Sasa nikashangaa wanalingia elimu au ajira? Diploma ya kumfanya mtu alinge kweli? Kama wanalinga kwa sababu ya ajira, je wangekuwa makatibu wa elimu wizarani ingekuaje? Just imagine jamaa ndio angekuwa Makonda, hapo mjini Daslam mngeishije? Basi siku ikaisha hivyo kinyonge!
Juzi kati mzee aliniambia nisiache ku apply nafasi za ualimu zilizotangazwa na serikali hata Kama uwezekano wa kupata ni 0.000. So siku hiyo sikwenda bush kwenye trekta nikabaki town ili nifanye application! Nikaenda internet cafe ili mambo yaende fasta!
Kama nusu saa hizi nikasikia sauti Kama naifahamu hivi, kugeuza shingo kumbe yule jamaa na demu wake wanaingia wakiwa na jamaa mwingine. Tukagongana macho, wakatoa macho Kama mjusi kapigwa spana! Hawakutarajia kuniona pale! Dereva wa trekta na macomputer wapi na wapi? nikawapotezea!
Kumbe wamekuja kumsaidia kufanya application yule jamaa ni mshkaji wao. Walikuwa hawajui vitu vingi na mhudumu wa pale cafe hakuwa na msaada kwao akawaambia waje kuniuliza Mimi maana kaniona nafanya application. Hawakuamini kabisa! Dereva wa trekta anafanya application? Kivipi yaani?
Ulikuwa mtihani mzito kwao, liliwashuka, sura zao zikasawijika, wakakosa pozi, wakacharara, waliishiwa kwa kweli ila watafanyaje? Wakaja huku wanajichekesha wakanisalimu kwa kunipa mkono bila ajizi na Mimi nikawapa mkono na tabasamu langu la uongo usiojificha mdomoni.
Wakashangaa Sana kuona ninabonyeza sehemu ya TCU badala ya NACTE. Wakaniuliza nimesoma chuo gani, usitake kujua niliwajibu Nini ila unajua tena sisi wa UDSM tunavyojionaga tumeyapatia maisha! Niliwajibu kwa kadri inavyopaswa!
Yule binti akasema, "sio mbaya lakini, umejishikiza kwenye kuendesha trekta" nikamuangalia usoni nikamwambia hapana Lile trekta ni langu nashindwa kumuajiri dereva maana wanakuwaga wasumbufu Sana! Nilihakikisha wanajua hadi kipato changu kuwa wakiunganisha mishahara yao wote Kama mambo yakikaa sawa Mimi naingiza ndani ya wiki mbili tu.
Jamaa mkosa adabu alikosa raha. Kwenye kiti palikuwa hapakaliki mbaya zaidi demu wake aliweza kwenda sawa na upepo ali connect na Mimi vizuri kabisa! Hadi namba ya simu alinipa ili wakiwa vizuri nikawabebee mahindi yao.
Sasa hapa Nina namba ya simu ya demu, tunachati tu WhatsApp kuhusu changamoto za Maisha na fursa za baadae. Ghafla nimekuwa motivation speaker wake! Ananichukulia Kama role model wake! Sijui Kama jamaa nimemsamehe au vipi acha niendelee kuchati na demu wake kwanza!