Ushawahi kuchukuliwa poa na mtu halafu akakuta sivyo kama alivyokudhania?

Mimi kila nikienda kutembea sehemu moja hivi walikuwa wanajua mimi ni dw
Dereva tu , kutokana na uvaaji wangu simple na kujichanganya.

Kuna mitaa naenda ,natembelea hawajawahi kujua km mimi ni mtu wa aina gani ,naonekan mlugaluga tu ,maana kuna mda wa kazi nakuwa smart na weekend kuzugazuga tu....


Huwa naruhusu wanchukulie poa tu .....i dont need attention or mtu kuniheshimu kwaajili ya kitu au kwa sabanu ni fulani ....


Heshimu kila mtu , mtu yoyote anaeza kuwa msaaada kwako wakati wowote
 
Q were sss
 
Kwaiyo ulimuogopa canal...
 
Wanawake walosoma na watumishi wana changamoto sana,wengi wao huachika baada ya kuolewa ndani ya miaka 10 ya ndoa....

Nakubali. Nimeoa mtu wa namna hiyo ndoa yangu imeshikwa na Kamba nyembamba mno ya mahusiano.
Tuna mwaka wa 8 kwenye Ndoa lakini sina uhakika kama huu mwaka wa 8 nitaumaliza na yeye. Kwa kiasi kikubwa kamba ya Ndoa imeshikwa na kaka yangu, akiiachia ndoa imeisha.
 

😀😀
 
Hapo full kujichekelesha tu
 
Chief pole sana
 
Kuna mheshimiwa mmoja alikua akifika ofisini kwetu kila mtu anatetemeka, siku hiyo kaja kanikuta nikamkazia naongea nae kama mshkaji tu huku namuuliza maswali hadi mwenyewe akaingia ubaridi akaniuliza wewe kabila gani nikamwambia mimi mswahili tu, muda huo tunaongea ofisi nzima wamekimbia namuona boss kajificha anasikiliza tunachoongea, kuanzia siku hiyo yule mzee akija ofisini anaulizia yule mswahili yuko wapi, nikifika namzingua hadi tumekua washkaji kaomba namba yangu akiwa na shida ananicheki, siku hizi hata staff wengine hawamuogopi kivile kama mwanzo
 
Kuna jamaa mmoja alishawahi kunikejeli na kunidhihaki..
Akitaka kunipiga,,hata watu wakimsihi asinipige,,
Anatamba tupewe dk 10 aning,oe meno..yote ya mbele.
Basi alijaza watu sana pale mtaani.

Si unajuwa tena unapohamia mitaa mipya? Watu hawakujui vzr.
niliokolewa na Mzee mmoja Mwenye busara,,ili jamaa asinipige.

Lakini jamaa alikuwa serious kutaka kupigana na mm,
Kiisa cha kijinga kabisa..

Ikawa jamaa kila akiniona,,
ananikoromea,,Mimi nampuuza tu.

Siku moja huyo jamaa alikuja kwenye gym yetu ya mazoezi bila kujuwa.
akataka aanze kujiunga,,ili afundishwe ngumi..

Alipokuja akapewa utaratibu ,
halafu akaambiwa na vijana subiri mwandende afike..
Yeye ndy mpango mzima humu.
Jamaa alishtuka sana aliponiona kumbe mwandende mwenyewe ngumi cherehani ni Mimi..
Jamaa uso wake ulikuwa mdogo kama kijiko cha chai..

Nilichokifanya niliomba jamaa aanze na mimi ulingoni,,
Ili kupima uwezo wake,,

Kilichofata ni mayowe na vilio kutoka kwa jamaa..

Usimdharau usiyemjuwa.,
 
mods kuweni makini na UPDATE ya huu uzi,nashauri baada ya siku mbili muunganishe kwa ule wa RIKIBOY.hiyo namba iliyochukuliwa hiyo.
 
10 kilotons of TNT pitia hapa..
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ukampa za chembe?
 
Napenda kusema ila kutokana na mambo usiri wangu ngoja niendelee kusoma comment zenu
 
mkoba tena
 

I JUST MET MY TWIN IN THIS COMMENT . Cheers to that [emoji3577] you are truly living a true life . Mimi pia ndio huishi hivyo
 
dah na mim umenifanya nilete kisa changu ambacho hakina hata miezi miwili.
kuna mdada jina yupo katika ofisi fulani ni majirani zetu(home).Ni wale watu wanaoringa kupita kiasi ukimsalimia kama hakuoni vile( hii ishatokea kama mara 3) last time niko zangu na town anafanya kazi pale benjamin mkapa,nmemkuta yupo na wenzake wakati huo nilikuwa niko na kaka yangu mkubwa.

Nikamchangamkia ila mwenzangu kanilia buyu namtambulisha kwa bro kuwa huyu ndo jirani dah mixer mfyonyo juu hakuna siku roho ilikuwa inaniuma kama siku siyo.

sasa week kama 3 nyuma natokea moro nmeingia kama saa 6 hivi nikasema ngoja sku ya leo nikasalie pale upanga maamur ni mskiti ambao waislamu wengi sana wanapenda kuosha maiti pale na kwenda kuzikia makaburi ya kisutu.

Nilivyofika pale pakawa kama na stori za chini kwa chini kuwa muosha maiti amekimbia baada ya kuosha maiti zaidi ya tano kitu ambacho syo cha kawaida, basi kwenye maongezi maongezi ikajulikana kuwa kuna maiti kama 2 zimeshndwa kuoshwa ndugu hawajui na muoshaji kakimbia(hofu ya corona)

Basi tukajitokeza mimi na mwenzangu tukaingia chumba cha maiti tulikuwa kama wa 4,tukaiosha ile ya kwanza,then tukafata ile ya pili zote tukaandaa safi kabisa ila ile ya pili niligundua alikuwa na baba wa yule dada maringo.

wakati tunatoka kuosha ndugu wakatuvuta pembeni wakatupa kama laki 3,wenzangu walichukua ila mimi sikuchukua hata cent sasa kumbe aliyekuwa anatoa hela ni mdogo wa yule(dada maringo) ambae anaishi nairobi kaja kumzika mzee wake but hanijui.

basi tukachukua maiti tukaenda zetu kuzika makaburi ya kisutu, wakati narudi zangu maeneo ya home ndo nakuta msiba sasa huku zogo pembeni likiwa ni muosha maiti kukimbi, basi jamaa akaniona mdogo mtu tukasalimiana pale ile furaha aliyokuwa nayo akanishika mkono mpaka uwani ambako kulikuwa na dada zake na mjane akanitambulisha na jinsi nilivyowasaidia dada mtu(cha maringo) aliangua kilio kupita maeleozo akaniomba namba nkampa.

baada ya kama dakika 30 baada ya kurudi home nikatumiwa mesage kama gazeti ya kuniomba radhi/msamaha mie nka act humble tu japo kila siku anataka tuonane but kila akinipigia namwambia niko moro japo anafosi anitumie hata nauli nikaonane nae au aje yeye but namchomolea.

katika maisha usimdharau mtu kwani huwezi jua nani atakaekufaa kwani unaweza kuwa trilionea but msaada wako ukatoka kwa mwenye kupata sh 500 kwa siku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…