Ushawahi kuchukuliwa poa na mtu halafu akakuta sivyo kama alivyokudhania?

Tatizo mzee unakula Sana kaya

Inakupa makonfidensi Sana[emoji1]
 
Hahahaha alichezea vitasa[emoji1787][emoji1787]
 
Ile ambayo Magu ameifugia?
 
[emoji28][emoji38][emoji1787]
 
Hii kitu nakumbuka ilikuwa ni kwa my husband. Alinipost Instagram siku ya birthday yangu. Kuna wadada na wakaka wakamtext inbox kumuuliza huyo ni mkeo kweli au utani?!

Wanastaajabu sababu hawakudhania anaweza kuwa na mwanamke kama mimi kwa maana ya uzuri [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23].

Nikamwambia lets kiss tuwatumie video wasijehisi unapost wanawake za watu.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu picha tafadhali na sie tukuone..
 
mimi binafsi nachukuliwa poa sana na naendelea kuchukuliwa poa kwasababu sina mwendelezo chanya ( sina maendeleo) ila naamini wanaonichukulia poa ipo siku watajuta na kusutwa na nafsi zao juu yangu as long as bado kijana na nina ndoto na mipango kedekede yakitimia watainamisha vichwa vyao chini


ngoja nimwage hiki kisa nilichosimuliwa na mwalimu wangu. huyu ticha wangu alienda kariakoo kama sio posta kwenye maduka ya kuuza vifaa vya kielektroniki maana laptop yake ilikua na shida akahitaji kifaa flani kama spear. sasa wakati anaelekea kuingia kwenye mojawapo ya duka kubwa mlinzi akamchukulia poa kwa mwonekano wake( ticha ni mfupi, mweusi, ana mwili mdogo na ana ulemavu wa mkono mmoja sijawahi juaga chanzo cha ulemavu wake) kwa ukali mlinzi akawa anamhoji


mlinzi; weweee simama hapo, UNAKWENDA WAPI?

ticha; kwani huku watu wanakwenda wapi?

mlinzi; UNAKWENDA KUFANYA NINI HUKO?

ticha; kwani huku watu wanakwenda kufanya nini?

mlinzi; Unarudisha maswali kwangu hebu nipatie kitambulisho chako


ticha akazama kwenye begi akamtolea Id kucheki ni mwalimu wa shule ya sekondari mojawapo wilaya ya temeke. mlinzi akabaki ameduwaa nadhani alijua atakua ni ombaomba wale wa jiji maana ticha hakua smart hata kidogo.ticha kuzama ndani akamkuta mzungu sijui mhindi dukani kwa kuua kabisa mwalimu akaeleza shida yake ya kifaa anachohitaji kwa lugha ya malkia kwa ufasaha kabisa maana hiyo lugha yeye ndo mwalimu hilo somo, mlinzi akachoka. hakufanikiwa kupata alichokitafuta ila kwa lugha ya kibiashara yule mhindi akamuambia mzigo umeisha ila mpaka next week mzigo utakua umefika.



nadhani huyo mlinzi licha ya aibu zake alipata funzo kubwa kuliko sisi.



huyu ticha ni memba mkongwe huku jf na tukiwa shule alituambiaga mtandao wa kuongeza maarifa ni jamii forum sio ile ya ajabuajabu. nimekumis sana mwalimu mwaka juzi nilionana nae kwa mara ya mwisho nikamwambia saivi na mi ni mwanajf akaniambia 'kuwa makini bhana usije ukawa unabishana na mwalimu huko jf'



nakutakia kheri na uzima tele mwalimu wangu nakukumbuka sana
 
Hakuna uzi niliowaji kuupenda na nimecheka sanaaa toka nimejiunga humu wacha nisome yangu mwisho[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…