Ushawahi kuchukuliwa poa na mtu halafu akakuta sivyo kama alivyokudhania?

Ushawahi kuchukuliwa poa na mtu halafu akakuta sivyo kama alivyokudhania?

Kuna mheshimiwa mmoja alikua akifika ofisini kwetu kila mtu anatetemeka, siku hiyo kaja kanikuta nikamkazia naongea nae kama mshkaji tu huku namuuliza maswali hadi mwenyewe akaingia ubaridi akaniuliza wewe kabila gani nikamwambia mimi mswahili tu, muda huo tunaongea ofisi nzima wamekimbia namuona boss kajificha anasikiliza tunachoongea, kuanzia siku hiyo yule mzee akija ofisini anaulizia yule mswahili yuko wapi, nikifika namzingua hadi tumekua washkaji kaomba namba yangu akiwa na shida ananicheki, siku hizi hata staff wengine hawamuogopi kivile kama mwanzo
Tatizo mzee unakula Sana kaya

Inakupa makonfidensi Sana[emoji1]
 
Kuna jamaa mmoja alishawahi kunikejeli na kunidhihaki..
Akitaka kunipiga,,hata watu wakimsihi asinipige,,
Anatamba tupewe dk 10 aning,oe meno..yote ya mbele.

Basi alijaza watu sana pale mtaani.

Si unajuwa tena unapohamia mitaa mipya? Watu hawakujui vzr.

Basi niliokolewa na Mzee mmoja Mwenye busara,,ili jamaa asinipige.

Lakini jamaa alikuwa serious kutaka kupigana na mm,,kisa cha kijinga kabisa..
Basi ikawa jamaa kila akiniona,,ananikoromea,,Mimi nampuuza tu.

Siku moja huyo jamaa alikuja kwenye gym yetu ya mazoezi bila kujuwa.

akataka aanze kujiunga,,ili afundishwe ngumi..

Alipokuja akapewa utaratibu ,halafu akaambiwa na vijana subiri mwandende afike..
Yeye ndy mpango mzima humu.

Jamaa alishtuka sana aliponiona kumbe mwandende mwenyewe ngumi cherehani ni Mimi..

Jamaa uso wake ulikuwa mdogo kama kijiko cha chai..

Nilichokifanya jamaa niliomba aanze na mimi ulingoni,,
Ili kupima uwezo wake,,

Kilichofata ni mayowe na kilio kwa jamaa..

Usimdharau usiyemjuwa.
Hahahaha alichezea vitasa[emoji1787][emoji1787]
 
It was a suprise kwangu.

Jirani yangu aliekuwa anajifanya ni boss wa Ikulu mtaani muda wote kanuna na miwani yake mieusi alikuja kunihudumia Chai Ofisini kwa Mama Salma Kikwete wakati wa WAMA, kumbe Alikuwa Office attendant pale tena wale wa oya oya na mie na wenzangu tulienda kupeleka project paper ya ki NGO chetu ambacho ni Hayati kwa sasa kuanzia 2015.
Ile ambayo Magu ameifugia?
 
Nakumbuka kuna kipindi nilikuwa nakula sehemu(mgahawa).sasa ylule mpishi alikuwa akiniletea dharau sana kwa sababu nilikuwa naulizia ugali kila siku nikiwa pale,alikuwa analeta shobo zaidi kwa wale wanaonunua chipsi.

Lakini mwisho wa siku alikuja kubadilika alipogundua mimi ndiyo mkulima wa vile viazi anavyouza.
[emoji28][emoji38][emoji1787]
 
Hii kitu nakumbuka ilikuwa ni kwa my husband. Alinipost Instagram siku ya birthday yangu. Kuna wadada na wakaka wakamtext inbox kumuuliza huyo ni mkeo kweli au utani?!

Wanastaajabu sababu hawakudhania anaweza kuwa na mwanamke kama mimi kwa maana ya uzuri [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23].

Nikamwambia lets kiss tuwatumie video wasijehisi unapost wanawake za watu.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii kitu nakumbuka ilikuwa ni kwa my husband. Alinipost Instagram siku ya birthday yangu. Kuna wadada na wakaka wakamtext inbox kumuuliza huyo ni mkeo kweli au utani?!

Wanastaajabu sababu hawakudhania anaweza kuwa na mwanamke kama mimi kwa maana ya uzuri [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23].

Nikamwambia lets kiss tuwatumie video wasijehisi unapost wanawake za watu.....

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu picha tafadhali na sie tukuone..
 
mimi binafsi nachukuliwa poa sana na naendelea kuchukuliwa poa kwasababu sina mwendelezo chanya ( sina maendeleo) ila naamini wanaonichukulia poa ipo siku watajuta na kusutwa na nafsi zao juu yangu as long as bado kijana na nina ndoto na mipango kedekede yakitimia watainamisha vichwa vyao chini


ngoja nimwage hiki kisa nilichosimuliwa na mwalimu wangu. huyu ticha wangu alienda kariakoo kama sio posta kwenye maduka ya kuuza vifaa vya kielektroniki maana laptop yake ilikua na shida akahitaji kifaa flani kama spear. sasa wakati anaelekea kuingia kwenye mojawapo ya duka kubwa mlinzi akamchukulia poa kwa mwonekano wake( ticha ni mfupi, mweusi, ana mwili mdogo na ana ulemavu wa mkono mmoja sijawahi juaga chanzo cha ulemavu wake) kwa ukali mlinzi akawa anamhoji


mlinzi; weweee simama hapo, UNAKWENDA WAPI?

ticha; kwani huku watu wanakwenda wapi?

mlinzi; UNAKWENDA KUFANYA NINI HUKO?

ticha; kwani huku watu wanakwenda kufanya nini?

mlinzi; Unarudisha maswali kwangu hebu nipatie kitambulisho chako


ticha akazama kwenye begi akamtolea Id kucheki ni mwalimu wa shule ya sekondari mojawapo wilaya ya temeke. mlinzi akabaki ameduwaa nadhani alijua atakua ni ombaomba wale wa jiji maana ticha hakua smart hata kidogo.ticha kuzama ndani akamkuta mzungu sijui mhindi dukani kwa kuua kabisa mwalimu akaeleza shida yake ya kifaa anachohitaji kwa lugha ya malkia kwa ufasaha kabisa maana hiyo lugha yeye ndo mwalimu hilo somo, mlinzi akachoka. hakufanikiwa kupata alichokitafuta ila kwa lugha ya kibiashara yule mhindi akamuambia mzigo umeisha ila mpaka next week mzigo utakua umefika.



nadhani huyo mlinzi licha ya aibu zake alipata funzo kubwa kuliko sisi.



huyu ticha ni memba mkongwe huku jf na tukiwa shule alituambiaga mtandao wa kuongeza maarifa ni jamii forum sio ile ya ajabuajabu. nimekumis sana mwalimu mwaka juzi nilionana nae kwa mara ya mwisho nikamwambia saivi na mi ni mwanajf akaniambia 'kuwa makini bhana usije ukawa unabishana na mwalimu huko jf'



nakutakia kheri na uzima tele mwalimu wangu nakukumbuka sana
 
Hakuna uzi niliowaji kuupenda na nimecheka sanaaa toka nimejiunga humu wacha nisome yangu mwisho[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom