Kuna jamaa mmoja alishawahi kunikejeli na kunidhihaki..
Akitaka kunipiga,,hata watu wakimsihi asinipige,,
Anatamba tupewe dk 10 aning,oe meno..yote ya mbele.
Basi alijaza watu sana pale mtaani.
Si unajuwa tena unapohamia mitaa mipya? Watu hawakujui vzr.
Basi niliokolewa na Mzee mmoja Mwenye busara,,ili jamaa asinipige.
Lakini jamaa alikuwa serious kutaka kupigana na mm,,kisa cha kijinga kabisa..
Basi ikawa jamaa kila akiniona,,ananikoromea,,Mimi nampuuza tu.
Siku moja huyo jamaa alikuja kwenye gym yetu ya mazoezi bila kujuwa.
akataka aanze kujiunga,,ili afundishwe ngumi..
Alipokuja akapewa utaratibu ,halafu akaambiwa na vijana subiri mwandende afike..
Yeye ndy mpango mzima humu.
Jamaa alishtuka sana aliponiona kumbe mwandende mwenyewe ngumi cherehani ni Mimi..
Jamaa uso wake ulikuwa mdogo kama kijiko cha chai..
Nilichokifanya jamaa niliomba aanze na mimi ulingoni,,
Ili kupima uwezo wake,,
Kilichofata ni mayowe na kilio kwa jamaa..
Usimdharau usiyemjuwa.