Ushawahi kuchukuliwa poa na mtu halafu akakuta sivyo kama alivyokudhania?

Ushawahi kuchukuliwa poa na mtu halafu akakuta sivyo kama alivyokudhania?

Sasa mkuu uko BOT halafu unavaa tshirt chakavu za mtumba na pensi. Lazma uonekane kibaka tu! Dada alihisi utamuibia iphone ake 🤣!!!

Lol...ukiwa mjini hapa jipende. Kuwa smart vaa vizuri, japo sio lazima uwe tozi ila atleast vaa ki bro simple tu! Saa kali, sandals au lightweight shoes outfit bomba tu... Dar kuna maduka mengi mno kiasi kwamba ukishindwa kuwa smart utakuwa na tatizo mahali. Usisahau kunukia
Dar kupendeza si rahisi kama watu wanavyodhani,otherwise uwe mvaa "sare sare maua" ila uktaka vaa uwe unique kwa dar lazma uwe na Dooo,yani uwe na mawe kiaina flani hivi...

uwe mtu unaweza enda shopping ukatumia 100k and above maana nguo/viatu,nk unavinunua kwa jumla na sio kwa reja reja,ukisema ununue kiatu kwa reja reja Yani unaenda dukani unataka 1 pair

asee bei zake hazina tofaut na maduka ya mikoani,hata huko k.koo ukienda unataka ETI kiatu pair 1 lazima bei iwe ya moto,kiufupi DAR CITY usipofanya mishe zakuingiza pesa ya kutosha utavaa ila

utavaa "sare sare maua",ila kwenye upande wa kunukia mkazi wa DAR akinuka asee "amejitakia" tena mtu akiwaga karibu yangu halafu anaharufu ya ajabu simkwepeshi,namchana LIVE maana hamna sehemu ina manukato bei rahisi kama DAR.
 
Sasa kama hata uyo wa kupata wapi namba hayupo ntafanyaje[emoji15]
Mimi wanajua nachagua sana kumbe walaa basi tu napenda ustaarabu,mwanaume anaeandika bac,xaxa,kwio ake sitaki kabisa bora niwe mtawa[emoji2]
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
mimba sikuhizi ni qualification kubwa[emoji45][emoji45]
Kwahiyo mwanamke yoyote tu akishika mimba ndo mkeo jumla haihitaji mambo mengine!!!??

Basi wenye vizazi vya Makha ndoa tutaziskia kwa bomba
Hiyo nimetolea mfano mimi, ndio ilikua target yangu kipindi hicho, sijamaanisha na wewe ufanye hivyo
 
Kipindi fulani nilikuwa nasafiri na garimoshi kutoka bara kuelekea pwani nikawa katika chumba daraja la pili na wasafiri wenzangu watano (chumba kimoja kina vitanda 6 katika behewa daraja la pili).

Kulikuwa na vijana watatu kila mara wanasimuliana habari za vichwa vya treni vya umeme (electric locomotives) sasa katika kusimuliana kwao wakawa wameshika kimaongezi mkuu mmoja tulikuwa nae alikuwa mtu mzima mi nawasikiliza katika moja na mbili wakaanza kuelezea vitu sivyo mi nikawa nimeingilia yale maongezi kwa kuwaambia hapo kidogo siyo sahihi.

Bwana mdogo mmoja wapo akanijia juu sisi ndiyo wataalamu wa hiyo fani mi nikakaa kimya. Safari ikaendelea tukafika sehemu moja inaitwa Kitalaka kichwa kikasumbua sana abiria wengi wakawa wameshuka chini kutahamaki tukihisi labda tatizo la upepo (watu wa vyombo hivi wanaita brake binding yani breki kukamata magurudumu pasipo dereva kukamata breki).

Bahati mbaya au nzuri kuchungulia namuona dereva nikamuita jina kumuuliza tatizo nini, akatahamaki mno kumbe wataalamu mpo humu mmekaa vyumbani njoo aisee. Kweli nilishuka tukaenda kutatua tatizo tukarudi. Vijana niliwaonea huruma aisee yule mzee ndiyo akaanza kuniuliza kila alilohitaji. Vijana wakaji introduce kuwa wametoka field basi nao pia wakawa huru kuuliza kila walichopendelea.
 
Mm miaka hii nimeanzisha michezo ya kizungu. Nikiwa na mihadi na mtu nionane nae namuelekeza aje sehemu ya kulia chakula hotel kubwa kubwa nikifika kule naagiza kisosi kidogo cha mboga za majani au kikombe cha maziwa na yai moja la kuchemsha hapo najua hata 10K haifiki. Mda huo chai inachemka nachukua sim naanza kuchambua timu za kubet huku namsubiri best yangu aje. Basi wahudumu wanajuaga huyu jamaa mnyamwezi au kaishi sana mbele, kumbe nawaangalia wazungu Instagram alafu naigiza.
we nakuona unataka kunifundisha tabia mbaya wewe..
 
Mada hii toka imepostiwa huwa natamani kuchangia but ubize na uvivu wa kuandika vinanishinda Nguvu.

Ngoja leo nitoe kisa kimoja katika visa vyangu vingi vya maisha yangu.

Mwaka 2008 nikimuuguza mzee wangu katika hospital moja kigoma ipo sehem mmoja panaitwa Manyovu ile hospital kama sijasahau itakuwa inaitwa Nyamasovu.

Nikiwa kijana mdogo katika watu walokuwa wakiwauguza na kusimamia wagonjwa wao, Manessi walinichukulia poa sana. Mda mwingne walinifokea kipindi wananipa maelekezo.

Namkumbuka nessi mmoja mdogo kama wa miaka 20-22 hivi. Mzee alikuwa kafanyiwa sajari na alikuwa kawekewa mipira yakutolea uchafu mwilini hivyo kuna muda ilikuwa ikijaa naenda kumwita yule nessi aje atoe na kum badirishia mfuko wa uchafu , alikuwa ananitizama kwa dharau sana. Kuna siku akanitamkia kabisa " we kaka mbona msumbufu? Nikajibu nessi me naangalia uhai wa mzee wangu akanambia Kwani baba yako ndo atakuwa wa kwanza kufa, ? Ivi mnahisi Manessi tunafurahia kuchezea uchafu wa wagonjwa wenu? Ungesoma nawewe ukawa nessi ukaona tunachokifaidi sisi. " duh! Kiukweli niliumia sana.

Kwa uwezo wa MUNGU mzee akapona , siku ninaendea ruhusa ili tumrudishe nyumbani kale kanessi kakaniambia kwa kejeli "Baba wa Taifa amepona " nikajifanya sijaelewa kakaongeza et "unahangaika utafkiri unamuuguza Yesu " kipindi hicho nilkuwa bado nasoma ko nikawa napretend ustaarabu ili nisiharibu cv .

Baada ya miaka kupita nikiwa nishasahau siku moja nipo kwenye ndege pakawa kuna mdada siti ya mbele yangu (kama siti ya3 toka kwangu upande wa kushoto) ananiangalia sana. Yani kila dakika anageuka tukikutabisha macho me naangalia pembeni nikiinua macho tena nakuta ananiangalia tena. Nikahisi labda ni x wangu flan iv katika ma x zangu. Tulivyoshuka mw/ Julius Nyerere watu wakaanza kushuka nikawa nimeinamia simu naiwasha baada yakuizima kipindi ndege inaanza safari nikainuka ile navua mkanda nainuka kuotoa begi juu nakuta watu wengi washashuka kabaki dada mmoja tu na wahudumu wa ndege. Nikashuka chini ile nipo kwenye ngazi akanigusa mtu kwa nyuma nikageuka sikuwa namkumbuka akajitambulisha kumbe ndo yule nessi. Kwakuwa sikuwa mtu wakuweka kinyongo nikamchangamkia tukatoka nje nikawa nasubiri Dogo aniijie na gari la home kumbe yeye hana usafiri anawaza tax nikamkazia kama sioni shida yake akajishusha mwenyewe akaomba lift nikamchukua hadi tunafika ubungo hajasema anaenda wapi kumbe alijiendeleza kielim ko anasoma Md muhimbili ila dsm hana mwenyeji ko nikampeleka napoishi akalala (mana ilikuwa ishakuwa usiku) kesho asbuhi me nayeye hatukuweza kuonana mana nilikuwa nina mishe zangu zilizonileta mjini ko alivyoamka akaoga akapata chai dogo akampeleka chuoni. Aisee alinipigia simu usiku wake eti ndo ananiuliza mzee anaendeleaje. Then sikutaka tuyaongelee ya kipindi kile ila alinisihi sana nimsamehe na kuanzia siku hiyo heshima mpaka sasa
 
Kwanza naomba 'nidiclee' kwamba mm ni mmoja wa ME ambae si mtu wa fashion, yani mimi sijui kuvaa kabisa na sina hiyo passion ya pamba pamba. Nishawahi kusemwa sana na ma-ex wangu kuhusu uvaaji wangu lakini haikusaidia kitu.

Sasa weekend iliyopita nilienda sehemu moja flani hivi amazing, chimbo la uhakika haswaa, limejitenga na limetulia kweli. Nilipigilia kipensi changu na ka t-shirt flan hivi local nikachagua sehem nikakaa, kutizama vizuri nikaona kuna meza amekaa mdada mmoja hivi and of coz she is gud looking nikaamua kujitosa angalau kumpa hata hi 'coz tulikuwa wateja 2 tu, nikamfata nikamsalimu.

Yule dada kwanza alinishusha kuanzia juu mpaka chini then akaitikia salamu yangu ki-design kama namsumbua flani hivi. Nikaomba kujumuika nae kama asipojali. Jibu lake ndo lilinitoa confidence kabsa, alinambia: "Kwahiyo kaka unadhani kila msichana akikaa peke yake anahitaji kampani? Hapana sihitaji" Dah, mwanamme nikajizoazoa pale nikarudi nilipokaa. Nilikaa kama masaa ma3 hivi nikaamsha zangu. Sasa kilichotokea jana ndo kimenifanya niandike huu uzi.

Nilipokea maagizo kuanzia J3 ya wiki hii kuwa leo watakuja watu wa Taasisi flani ya kifedha kutoa semina kwa sisi wafanyakazi kwa ajili ya kutushawishi kujiunga na huduma za Taasisi yao, hivyo mimi nikapewa jukumu la kuwakaribisha na kuwapeleka sehemu ambapo semina itafanyika.

Asubuhi mida kama ya saa 3 hv ugeni ukafika, walikuwa watu kama 7 hivi, kati yao alikuwepo yule dada nilieonana naye weekend.

Wakaingia ofisini nikawakaribisha, wakati mkubwa wao anatoa introduction macho nikayakaza kwa yule dada, bahati nzuri tukagonganisha macho, akashtuka flani, nikajua kashanikumbuka.

Baada ya semina kuisha ikafika kipindi cha watu kujiunga sasa kwa walioshawishika. Nikamfata yule dada nikamuomba aje anielekeze namna ya ujazaji fomu. Alivyofika tu, nikamuuliza "Unanikumbuka?" Akachekaaa, akaniambia "Yani wewe, sikutarajia kama unaweza kuwa unafanya kazi huku", nikamuuliza ulitarajia niwe nafanya kazi wapi? Akaishia kucheka tu. Mawasiliano yake kanipa; fresh bila shida kabisa.

Sasa naomba kuuliza wadau, mshawahi kukutana na situation ya namna hii?
Mimi nimekutana na jamaa mmoja ambaye tukikaa nae mtaani uswahilini kwetu. Kipindi hiko nimemaliza undergraduate degree yangu sijapata mchongo,nipo na washkaji mtaani tunabadilishana mawazo akawa anakuja mara nyingi dukani hasa akitokea kazini.
Jamaa alikua ni mtumishi wa halmashauri flan hivi nahisi. Basi alikua anawasalimia wale wenzangu kisa anawajua familia yao ilikua poa mimi ananiona nimechoka ananipotezea. Tambo nyingi kitaa haziishi.
Sasa mwaka juzi kaja ofisini kwetu kupata huduma,hamadi! anakutana na mimi nafungua mlango wa ofisi yangu na imeandikwa kuwa mimi ndie mkuu wa lile eneo..
Akaanza aaah...kumbe kaka upo hapa. Mbona husemi kama siku hizi unakitengo kumbe...mimi nikabaki namuitikia tu.

Mwisho, Mungu huwainua awatakao na kuwashusha awatakao...tuache dharau!
 
Dah maneno yake[emoji23][emoji23]
Mada hii toka imepostiwa huwa natamani kuchangia but ubize na uvivu wa kuandika vinanishinda Nguvu.

Ngoja leo nitoe kisa kimoja katika visa vyangu vingi vya maisha yangu.

Mwaka 2008 nikimuuguza mzee wangu katika hospital moja kigoma ipo sehem mmoja panaitwa Manyovu ile hospital kama sijasahau itakuwa inaitwa Nyamasovu.

Nikiwa kijana mdogo katika watu walokuwa wakiwauguza na kusimamia wagonjwa wao, Manessi walinichukulia poa sana. Mda mwingne walinifokea kipindi wananipa maelekezo.

Namkumbuka nessi mmoja mdogo kama wa miaka 20-22 hivi. Mzee alikuwa kafanyiwa sajari na alikuwa kawekewa mipira yakutolea uchafu mwilini hivyo kuna muda ilikuwa ikijaa naenda kumwita yule nessi aje atoe na kum badirishia mfuko wa uchafu , alikuwa ananitizama kwa dharau sana. Kuna siku akanitamkia kabisa " we kaka mbona msumbufu? Nikajibu nessi me naangalia uhai wa mzee wangu akanambia Kwani baba yako ndo atakuwa wa kwanza kufa, ? Ivi mnahisi Manessi tunafurahia kuchezea uchafu wa wagonjwa wenu? Ungesoma nawewe ukawa nessi ukaona tunachokifaidi sisi. " duh! Kiukweli niliumia sana.

Kwa uwezo wa MUNGU mzee akapona , siku ninaendea ruhusa ili tumrudishe nyumbani kale kanessi kakaniambia kwa kejeli "Baba wa Taifa amepona " nikajifanya sijaelewa kakaongeza et "unahangaika utafkiri unamuuguza Yesu " kipindi hicho nilkuwa bado nasoma ko nikawa napretend ustaarabu ili nisiharibu cv .

Baada ya miaka kupita nikiwa nishasahau siku moja nipo kwenye ndege pakawa kuna mdada siti ya mbele yangu (kama siti ya3 toka kwangu upande wa kushoto) ananiangalia sana. Yani kila dakika anageuka tukikutabisha macho me naangalia pembeni nikiinua macho tena nakuta ananiangalia tena. Nikahisi labda ni x wangu flan iv katika ma x zangu. Tulivyoshuka mw/ Julius Nyerere watu wakaanza kushuka nikawa nimeinamia simu naiwasha baada yakuizima kipindi ndege inaanza safari nikainuka ile navua mkanda nainuka kuotoa begi juu nakuta watu wengi washashuka kabaki dada mmoja tu na wahudumu wa ndege. Nikashuka chini ile nipo kwenye ngazi akanigusa mtu kwa nyuma nikageuka sikuwa namkumbuka akajitambulisha kumbe ndo yule nessi. Kwakuwa sikuwa mtu wakuweka kinyongo nikamchangamkia tukatoka nje nikawa nasubiri Dogo aniijie na gari la home kumbe yeye hana usafiri anawaza tax nikamkazia kama sioni shida yake akajishusha mwenyewe akaomba lift nikamchukua hadi tunafika ubungo hajasema anaenda wapi kumbe alijiendeleza kielim ko anasoma Md muhimbili ila dsm hana mwenyeji ko nikampeleka napoishi akalala (mana ilikuwa ishakuwa usiku) kesho asbuhi me nayeye hatukuweza kuonana mana nilikuwa nina mishe zangu zilizonileta mjini ko alivyoamka akaoga akapata chai dogo akampeleka chuoni. Aisee alinipigia simu usiku wake eti ndo ananiuliza mzee anaendeleaje. Then sikutaka tuyaongelee ya kipindi kile ila alinisihi sana nimsamehe na kuanzia siku hiyo heshima mpaka sasa
 
Dar kupendeza si rahisi kama watu wanavyodhani,otherwise uwe mvaa "sare sare maua" ila uktaka vaa uwe unique kwa dar lazma uwe na Dooo,yani uwe na mawe kiaina flani hivi...

uwe mtu unaweza enda shopping ukatumia 100k and above maana nguo/viatu,nk unavinunua kwa jumla na sio kwa reja reja,ukisema ununue kiatu kwa reja reja Yani unaenda dukani unataka 1 pair

asee bei zake hazina tofaut na maduka ya mikoani,hata huko k.koo ukienda unataka ETI kiatu pair 1 lazima bei iwe ya moto,kiufupi DAR CITY usipofanya mishe zakuingiza pesa ya kutosha utavaa ila

utavaa "sare sare maua",ila kwenye upande wa kunukia mkazi wa DAR akinuka asee "amejitakia" tena mtu akiwaga karibu yangu halafu anaharufu ya ajabu simkwepeshi,namchana LIVE maana hamna sehemu ina manukato bei rahisi kama DAR.
Kupendeza you dont need designer brands...Unaweza ingia maduka tu ya pembezoni mwa mji ukapata nguo safi tu kama Kariakoo unaona tabu kwenda.
Kwa staff anaepata 2M+ inakuwaje ngumu kufanya shopping ya 200k tu kila mwezi which is basically enough.

Suruali na mashati mazuri unayapata kwa 25k or less. Viatu ndio itategemea maana viko juu sana in cost. Kama utanunua pair moja moja sio mbaya atleast kila baada ya mwezi.
 
Swala la kutokidhi vigezo ni sawa...ila kama uliumia nakukataliwa pia.
Hapana binafsi kwenye kazi huwa sina mapenzi haijalishi nani wala nini hata awe Mama yangu au Baba yangu sina mzaha katika kazi
Nilimkata kwasababu hakukidhi vigezo
 
Kwangu mimi ni viceversa. Nifikapo mahali ambapo hawanifahamu watu hunipa heshima na wengine hata kujifikiria sana kabla ya kuchukua uamuzi wa kuja ongea na mimi. Hii ni kutokana na mwonekano wangu tu ila with time huwa wanaanza onyesha tudharau flani na wengine kunichana kabisa kwa msokwa1 kwa mara ya kwanza nakuona nilidhani wewe ni mtu wa aina flani ivi
 
sisi wengine baada ya hapo ndio huwa tunafunga vioo mazima,yaani fanya kama hatujawahi kukutana.

mimi jamaa alinisimulia hii tabia ya kudharau mikakati ya mtu katika maisha yake, usione mtu kazini yupo yupo tu miaka inaenda ukamdharau kwamba hana mipango, utajichanganya.

jamaa anasema wameanza kazi mwaka mmoja na huyo mshikaji wake, yeye akawa amepanga nyumba ya gharama kama 250k,usafiri wa kusumbulia watumjini nk. mwenzake yupo yupo tu. nyumba katafuta ya 120k, gari hakununua nk.

wamefanya kazi kama miaka 8 hivi. baadae siku moja wanapiga story jamaa yangu sasa akaanza maneno ya kumsimanga jamaa, oooh we vipi bana hela hatuoni wapi unapeleka, upo upo tu kama mshamba.jamaa akakereka ikabidi amuonyeshe salio bank, akasoma kwa utulivu ilikuwa ni 68mil, kwenye simu kuna 7mil.

baada ya pale jamaa siku yake iliharibika sana.
Aisee
 
Back
Top Bottom