Wengi sana mko ivo,
Mfano kuna wadada wa3 wanafanya kazi duka la jirani na kabiashara kangu sasa ofisi yao ilihamia siku za karibuni mwezi wa 5, yaani walikua na dharau hata salamu hawatoi sa ingine, ukiangalia wanavyovaa vizuri utasema ndio wenye duka..... Kumbe wanalipwa ela ndogo sanaa hata kula yenyewe wanajibana wakati mwingine wanajichanga wanakula miogo na maji
Sasa walivyojua kabiashara ni kangu basi kila mmoja kwa wakati wake anajipendekeza kiaina mi wala sina noma nimechangamka tu
Sasa mmoja kaja tu anajichekesha na utani nimnunulie saa, nkatafuta ya mda mrefu ishachoka kiaina nkampa.
Ila nilishakaa nao nkawasema kuhusu hiyo tabia yao, nkawaambia unawejikuta unamletea nyodo boss wako wa kesho au mmeo bila kujua, wananiheshimu sana sa hivi
Kuna wanawake wanaringa jamani acheni tu. Hata wanaume pia wapo.