Naenda zangu dar mida saa 3 ivi kutoka dodoma, nimekurupushwa tu kwa ofis nikaona sio mbaya nikapita zangu pale stend ya cbe kwa mama bwashee hua ana supu nzuri gari niliacha inaoshwa kona pale, basi wakat naingia pale nikakuta wadada wanne pisi haswa na mshkaji moja nao wanaingia na mabegi yao nikawasalimia kwa mbwembwe sana mi ni mtu utani sana, duh nilipandishwa na kushushwa aisee, binti mmoja tu ndo alipokea salam wengine hata habar na mimi hawana.
sijakoma nikaendelea kuwachangamkia jamani mnaenda dar nina usafiri? wakaniangalia tena juu mpaka chini nimevaa simpo sana kipensi na sendoz, yule yule dada aliyenipokelea salam ndo akajibu ndio boss, nikamwambia mbele yao we unaonekana mstaarabu sana hutolipa nauli, ajabu hata mwanaume mwenzangu eti kama hanioni....
basi tumekula pale nikainuka nikamuaga yule mrembo nakuja nafata gari sogea pale pemben ya barabara akacheka akasema sawa bos, nikafata chuma nafika pale nawaona wanajivuta lakin wadada wa3, mdada mmoja na mshkaji wamekaa zao hawana hata habari...