Pole saana mdada, si mtaalamu wa mambo hayo lakini common sense unanipa haya ya kusema.
1. Naona kuna kama hali ya mashindano, hata kama siyo moja Kwa moja basi hata hiyo ya wewe kudai fair treatment mwenzako analiona kama unashindana, sasa anakukomoa.
2. Huenda mama wa mtoto wa zamani ana mkono wake, au kuna mwanamke mwingine nje anamfanya asijisahau na akutreat vibaya, labda utaondoka mwenyewe. Inaweza ikawa hivi hivi tuu ujinga wake au hata kimazingara pia.
3. Ama kuna uwezekano ndugu zake flan hawakukubali, sasa nayeye amekuwa jinga jinga anayekosa ku analyse mambo.
4. He is short sighted, yaan ukute hapo umechangia ujenzi, na sasa huna hela huna ujanja, anajiona amefiiika, hajui kuwa hiyo nyumba siyo yake pekee.
Nini cha kufanya??
1. Huyo ni mumeo never give up on him, yaani weka akilini kwako kuwa kitakacho kutoa hapo labda roho itoke. Wewe ndo mtu wa kurekebisha yoote hayo. Hilo uwe nalo akilini.
2. Analyse Mali zote mlizochuma pamoja, ikiwepo na hiyo nyumba, register malalamiko official, iwe ustawi wa jamii, kikao cha ukoo, popote pale tafuta ushauri, yaani ijulikane kuwa mmejenga pamoja na kuwa mkopo wa mshahara wako unakatwa Kwa sababu ya Hilo, wazazi wako waliokusomesha wajue Hilo, mshenga ajue Hilo, yaani Kwa vyovyote vile ajue kabisa hicho anachojiaminisha ni ndoto. Mtoe upepo.
Usiogope vita kuongezeka lakin nakwambia akijua yote hayo atapunguza speed.
3. Ishi kwako bila kujali upendo wake, pika chakula, fanya majukumu yoote ya mke, omba hela za matumizi, ukinyimwa basi. Ila jishushe, usijinyenyekeze kiviile, itafika mpaka watoto wataona unanyanyaswa ila utafanyaje ndo zamu yako ya ups.
4. Punguza matumizi binafsi ili usiteseke Sana, kama unaweza kuishi na nywele fupi kata Tu, kwenye vikoba sijui kitchen party unaweza kujitoa au kujipunguza saaana, dunia haitakuelewa kirahisi lakn kwakuwa unajijua utakuwa na amani moyoni.
Ukiweza hayo japo for 4months utaona anajirudi mwenyewe. Ila ukiishi kama vile hayo anayokufanyia siyo kweli basi utateseka kisiri Siri Hadi utajikuta ume give up kirahisi.
Pole , nitaendelea hapa ama inbox
Note: hao watoto wote wanakutegemea uyakavyosimama wewe, bila wewe wanapotea wote.
Sent using
Jamii Forums mobile app