Ushawahi kuhisi upo single ndani ya ndoa?

Kuna kitu ngoja nikufundishe, kamwe usizamishe moyo wako.kwa mwanadamu hata umpendeje, manake wanadamu huwa wanabadilika wakati wowote. Penda mtu atkeast 50 percent hata awe mumeo.manake wanadam wana asili ya kuwa washenzi tu kuna siku atakuzingua, 50.percent unajibakishia mwenyewe siku akizingua unakua stable.

Lakini hata usiogope, kwa kuwa sa hv huna kitu we kuwa mpolee huku ukingoja uchumi wako ukae sawa, tena mpende huyo mumeo keshakuambia ukweli kuliko angekwambia ushajizeekea huna namna. Cha msingi kwa sasa msikilize akitoa hoja yoyote kuhusu mwanae au hapo ndani ili upunguze kumkwaza, huku we unamark time mambo yako yatengemae,..mbona utakuja kwenda nae sawa tu. Kuwa mpole sana na usioneshe kama unajali maneno yake we kuwa bwege huku ukitulia we ukae sawa manake hapo kama huna kipato usijemzingua akakufukuza ikawa majanga.@masai dada

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole Sana kwa unanyoyapitia! Baaba ya kusoma kinachokusibu nikavaa kiatu chako! Aisee kichwa kiliniuma hafla! Pole ndugu yangu...pole kipenzi! Jua kwamba kila linalokutokea linasababu! Hataivo every thing will be alright!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapana usiseme hivyo, Mungu hajapanga hivyo ni changamkto za kawaida mbona, u atakiwa uwe strong ukabili hizo changamoto na mpatane vitu kwa amani manake huwezi mfosi mtu anayekulisha.
Mkuu nilishasaligi huko nyuma mpaka nikaona acha nikae tu labda uenda ndo Mungu kapanga hivi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kung'ang'ania ndoa kama mtu hakuelewi ni bora uende utafute maisha yako utakufa kabla ya wakati kwa ujinga wako trust mi huyo sio mana wala baba y'ako
Omba divorce hiyo mahari itagawanjwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeoongea Point sana kunywa fanta nakuja kulipa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole kwa hili kasheshe linalokukuta Mrembo.

Wanaume wengi ni wabinafsi sana na wengi ndo wanafanyaga mioyo ya wanawake kuwa migumu.Tulia uzuri unamjua mume wako ndoa ni kupambana usirudishe mpira kwa kipa, bado mapema mno!jifunze kumpuuza kipindi hichi fanya vile vitu unavyovipenda.

Kumbuka wewe ndo chanzo cha furaha yako.Kingine tafuta biashara au mradi wowote utakaokufanya uwe busy na uweze kutengeneza kipato chako.Mbona utatoboa kimya kimya pasipo kuwa na majibizano ndani.Mungu akusaidie kweli kweli maana si rahisi.Happy New year.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Samahani Dada. Je huyo mzazi mwenzie walioana??? Je mahusiano yao yalikuwaje Mpaka wakapata Mtoto??? Huyo Mzazi mwenzake ana hali gani huko aliko???
 
Ushauri huu hapa masai dada huitaji kuongeza hata nukta

Hongera Mkuu Daby kwa busara hizi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nakushauri maisha popote. Amsha mapema. Hapo huna mume. Kwa sababu umewekeza hela hapo kwenye nyumba ili kuondoka kwanza na huo mkopo,nenda ustawi wa jamii. Hapo omba mambo mawili,la kwanza kuachana,waambie madhira yote unayopitia. La pili huo mkopo wa nyumba,wamshurutishe akurudidishie,ksbb nimekuona wewe ni mpambanaji,hiyo ukaanzie mbele. Ila hakikisha umeachana na huyo mume

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Agree
 
Pole saana mdada, si mtaalamu wa mambo hayo lakini common sense unanipa haya ya kusema.

1. Naona kuna kama hali ya mashindano, hata kama siyo moja Kwa moja basi hata hiyo ya wewe kudai fair treatment mwenzako analiona kama unashindana, sasa anakukomoa.

2. Huenda mama wa mtoto wa zamani ana mkono wake, au kuna mwanamke mwingine nje anamfanya asijisahau na akutreat vibaya, labda utaondoka mwenyewe. Inaweza ikawa hivi hivi tuu ujinga wake au hata kimazingara pia.

3. Ama kuna uwezekano ndugu zake flan hawakukubali, sasa nayeye amekuwa jinga jinga anayekosa ku analyse mambo.

4. He is short sighted, yaan ukute hapo umechangia ujenzi, na sasa huna hela huna ujanja, anajiona amefiiika, hajui kuwa hiyo nyumba siyo yake pekee.

Nini cha kufanya??

1. Huyo ni mumeo never give up on him, yaani weka akilini kwako kuwa kitakacho kutoa hapo labda roho itoke. Wewe ndo mtu wa kurekebisha yoote hayo. Hilo uwe nalo akilini.

2. Analyse Mali zote mlizochuma pamoja, ikiwepo na hiyo nyumba, register malalamiko official, iwe ustawi wa jamii, kikao cha ukoo, popote pale tafuta ushauri, yaani ijulikane kuwa mmejenga pamoja na kuwa mkopo wa mshahara wako unakatwa Kwa sababu ya Hilo, wazazi wako waliokusomesha wajue Hilo, mshenga ajue Hilo, yaani Kwa vyovyote vile ajue kabisa hicho anachojiaminisha ni ndoto. Mtoe upepo.
Usiogope vita kuongezeka lakin nakwambia akijua yote hayo atapunguza speed.

3. Ishi kwako bila kujali upendo wake, pika chakula, fanya majukumu yoote ya mke, omba hela za matumizi, ukinyimwa basi. Ila jishushe, usijinyenyekeze kiviile, itafika mpaka watoto wataona unanyanyaswa ila utafanyaje ndo zamu yako ya ups.

4. Punguza matumizi binafsi ili usiteseke Sana, kama unaweza kuishi na nywele fupi kata Tu, kwenye vikoba sijui kitchen party unaweza kujitoa au kujipunguza saaana, dunia haitakuelewa kirahisi lakn kwakuwa unajijua utakuwa na amani moyoni.


Ukiweza hayo japo for 4months utaona anajirudi mwenyewe. Ila ukiishi kama vile hayo anayokufanyia siyo kweli basi utateseka kisiri Siri Hadi utajikuta ume give up kirahisi.

Pole , nitaendelea hapa ama inbox

Note: hao watoto wote wanakutegemea uyakavyosimama wewe, bila wewe wanapotea wote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CHUKUA HUU USHAURI
 
Kwenye ule uzi...kuna mtu aliniambia WEWE NDO UNAMPENDA NA SIO YEYE yaani tunaishi kwa amani kwakua nampenda so vitu anavyofanya nina ignore
Kwa Hilo utakuja kulia zaidi
 
Ningekua nimesimama kiuchumi hata kesho ningeanza upya.
Inaumiza sana kuishi na mtu asiekupenda ila wewe unampenda ni bora na wewe mapenzi yawe yameshaisha
Sijui umri wako ila naisi wewe ndyo unajitesa sana kama bado una miaka 20 kazi mbele kama ni ya serikali wala usiwe na hofu just chill ila kama ni kampuni binafsi na una mkataba wa miaka 3 bado kwenye mkataba anza kujiwekeza polepole na kwenye ndoa yako usiexpect makubwa kama anakutia na unagurahi basi amini ilo ni jambo la muhimu mengine potezea jifurahie mwenyewe toka out na mwanao, au na marafiki zako jitafutie furaha ww usingoje yeye akupe ili ufurahi mmeo anajua unampenda ndyo maana anajibu vile ajisikiavyo acha kulilia penzi acha kuulizia Mali kikubwa tayari una kzi unaweza kujiwekeza mwenyewe uku anajua na usijichanganye tena kufanya kitu cha pamoja maana madhara ushayaona akikuuliza mwambie ni cha mwanao kama ni kiwanja weka jina la mwanao nyumba jina la mwanao kuepuka mogogoro mbeleni kumbuka furaha inaanza na wewe mwingine anaongezea tu kwaiyo itafute kwanza wewe ndyo mwingine akupe worry not about wealth kama una nia ya dhati utatafuta na kupata.
.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…