Ushawahi kuhisi upo single ndani ya ndoa?

Yote yatapita,huwezi kubaki katika hali hiyo milele. Ni sualala muda tu,piga moyo konde,tambua hitaji la moyo wako then tekeleza hitaji hilo.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna watu na comments zao eti “endelea kumpenda huyo ni mumeo” am being like WTF! Hivi mnajua hata mliletwa ulimwenguni kufanya nini nyie watu? Mnaijua thamani yenu kweli?! Is it necessary kuji attach kwa mtu ndio ukamilike? Can’t you guys stand on your own!? Yaani mtu unavumilia ujinga wiki ya kwanza, ya pili, mwezi, mwaka, mwaka wa pili, wa tano!!!!!!! Wait hebu tuambie labda kuna taji huko mbeleni mtavikwa au?

Kwanini mnamshauri mwenzenu aendelee kuvumilia mateso, kuna guarantee ipi kuwa mumewe atabadilika anytime soon, na akichelewa kubadilika damage inayotokea kwa huyu dada mtai repair ninyi? Jitahidi basi kuwa serious, ifike muda watu tufundishwe ndoa ninini na kila mtu awe na mipaka yake. Tatizo Africa hakuna genuine reasons za watu kuoana, sababu za ajabu kabisa hupelekea watu kujikuta wameoana. Ndoa nyingi zipo juu ya mawe hawasemi tu, wapo kimya kama hamna kinachotokea.

Watu yapaswa waoane kwasababu tu wanapendana na siku upendo ukiisha ni ruhusa na busara kutengana kuliko kuchapana matukio mwisho muuane!

Ndoa ni nzuri, kutokuwa ndoani pia ni kuzuri , its all about peace and being happy. Dear young girls stick on your standards, don't lower your standars, wait for the right time with right man its real worth it and while your waiting invest on yourself. Wasichana msiyumbishwe na makelele ya patriarchal societies ohh mara unazeeka mara atakuoa nani ohh mara utaishia kuwa single mother na blah blah zingine, learn to think independently, jichagulieni aina ya maisha mngependa muishi, binafsi nilishamwambia tena na tena akijaribu kufanya ujinga My happiness can’t be compromised, najua nini nataka katika haya maisha kama hawezi nipa/ nisaidia nipate i’m better off!

Nimesoma comments nikagundua wengi wamezoea manyanyaso na wengine wamezoea kunyanyasa, laiti mngejua maisha yalivyo matamu na mafupi nyie watu msingekubali kabisa mtu akuchukulie muda wako autumie kwa mambo yakipuuzi!
 
Binti Kiziwi nakuelewa sana ulichokiandika lakini practically hatuendi hivyo! Ndoa ni ngumu na huo uzungu wako kwenye ndoa wengi hawaufuati usimshauri mwenzio hilo. Do you know how difficulty to get divorce paper in Tanzania? Without it will you be free and happy!? tatizo la ndoa la huyu mdada ni dogo sana, ameolewa na mtu mbinafsi na ninahisi mumewe bado ajaacha ujana ndo maana anam treat unfairly mkewe! Baadhi ya wanaume wakipendwa wanakuona mjinga that’s maturity, as time goes on huyo mwanaume ataelewa thamani ya mkewe! Mimi simshauri aachane na mumewe!
 
Natamani nijue kitu, una age gani, najua una mtoto mmj naye? Hili ni swali la msingi sana. Moja, pili...tatizo ni hisia au hakupendi(kwamba labda ni periodical love) sometimes anaupendo sometimes hana). Je yeye ni age gani unaweza uka estimate tu.
 
Tafuta Wakili akusimamie, muandikiane huku alionyesha umechangia. Jisimamie anakuchezea tu, utakuta labda bado analala na mama wa mwanae. Ndio sababu kubwa ukionyesha haupo nae karibu. Tafuta wakili pata chako, hata mkiuza hiyo naomba potelea mbali. Kwake ni umemjengea yeye na wale sio nyie ( wewe na mwanao). Utaanza maisha mapya kivyovyote, anakutesa ukifa nani atamlea mwanao? Huyo mume hakupendi, anakuchezea. Jiongeze ujijali wewe na afya yako kwanza. Acha kumtegemea, anajua hivyo na hashtuki. Wakili kwanza jipatie haki yako, usimuonee huruma kashaamua iwe alivyo.
 
Acha tu.
Mwenzetu yamemkuta kaanza vibaya hana sh mia na anadaiwa rejesho la riba, dudu pia hapati na mume anamsakama tunamsaidiaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
Nianzie hapa hapa kukujibu. Mm kama mwanaume matured. Mwenye matatizo ni Masai Dada. Ana wivu, ni mchoyo, ila sio mbinafsi, hayuko serious, hayuko focused hapa bila kuambiana ukweli haitasaidia.

Katika haki ya kawaida, nyumba ni yake hapaswi kuanza kumsikiliza drunken man kuwa nyumba ya flani.

Sisi wanaume hamjawahi kutuelewa, tumeunbwa na extra mile japo tumeaswa tuishi nanyi kwa uangalifu, na hapo ndipo Masai alipokuwa blind.

Mapenz yao ni deaf blind. Mume anaendelea kutumia Male intelligence ambayo wamama hamna hii kitu.

Na Masai atakufa kwa kihoro. Wanawake wengi wanapoteza Maisha yao kwa kihoro, masai sio gangwe, sii muhuni, sii mlevi ni mtu wa Mungu japo ni mwanamke mjinga anapigana na adau asiyemjua, nilichoona mume anampenda Masai lkn masai anaketa kujua tabia kama za Lilith first adam wife.

Mwanamke asiyemnyenyekea mumewe nankuoenda ndg wa mumewe kama alivyoolewa huko hiyo ndoa itazama kina kirefu ardhini. Epuka ndoa kama hauko tayari kukubali sauti ya mume.

Swala la huruma kwa msichana wa kazi halikupaswa kuvuruga ndoa, swala la mdogo wa mumeo aka wifi halikupaswa kuwa kero kwako, katika hali ya kawaida nani anaharibikiwa?! anayelala na kufuliwa hadi chupi au anayefanyakazi na kutumikishwa?? Nyie ndiyo mnaofikiri kumpa mtoto good time ni kumsaidia. No nd never.

Kuifanya stori iwe fupi. Masai anamachaguo mawili. Kutii mume, abaki na ndoa, au abaki ndani akiwa na ananyanyasika asubiri afie ndani. Achague kuondoka atafute maisha mengine. Jibu analo
 
Mawazo yangu sasa, nayajua mwenyewe. Kwanza Mimi sijaolewa, ila akili yangu ingenituma yafuatayo:
1. Nyumba ina hati? Itafute uangalie imeandikwaje, kama kaandika jina lake mmeo, toa copy, then vibebe ukafanye certification, then certified copy tunza unakojua wewe. Maana ukigeukwa usishangae wakabadili umiliki ukashangaa hati inajina LA mama ake.
2. Kuanzia sasa, jihesabu hauna ndoa. Chochote unacho kifanya, waza furaha yako na future yako, fikiria hata kibiashara kidogo ufanya, huku unapanga majeshi yako. Najua mkopo una mwisho, hata mishahara huwa inapanda (thou yataka uvumilivu) yatakwisha. Muda huo usiwe boya tena kutumwa kukopa.
3.Ikitokea amekuagiza chochote cha thamani kununua (najua huna hela mpaka utumwe) make sure unapata risiti yenye jina lako. Tunza risiti.
4. With time utakuwa unaangalia hali ya mgonjwa inaendeleaje (mumeo anavyo kutreate namaanisha) ukiona ahueni ishi kwa tahadhari, kama ni mahututi hesabu muda wako wa kuwa stable kiuchumi ufanye yako.
 
Pole sana Masai Dada!
Kwa kina kabisa nimeelewa na kuguswa sana na tatizo lako. Kubwa babisa ni ni ule ukweli kuwa wewe ni mke halali wa ndoa na ndicho kimepelekea wewe kujitoa kwa moyo wako wote kuihudumia nyumba yako na kudumisha upendo ndani ya ndoa yako. Ni una ndoto na malengo makubwa juu ya familia yako.....mume, mtoto na wewe mwenyewe..... na ndiyo maana umetafuta hata mikopo kusaidia ujenzi wa nyumba.
Sina hakika sana japo natamani kusikia historia yako na mwenza wako namna mlivyoanza mahusiano na hatimaye kuingia kwenye hiyo ndoa. Hili kama nikilifahamu linaweza kunipa picha pana ya aina ya mahusiano yenu na nini kilipelekea hadi kuingia kwenye hiyo ndoa. Ninachotaka maanisha hapa si kwa nia mbaya bali kutengeneza njia ya namna gani kugundua tatizo lilipoanzia na hapo unaweza kupata chanzo sahihi cha kuanza kulitibu.
Nashawishika kusema huenda kuna maqmbo yako nyuma ya panzia na hivyo kuzuia hata watoa ushauri wakatoa ushauri wa kuweza kutibu hili tataizo. Mambo yanayoweza kuwa nyuma ya panzia ni mf uwiano wenu ki haiba......mnafananaje urembo wako na utanashati wake...... Mali anazomiliki yeye na zile unazomiliki wewe...... viwango vya elimu zenu nk. Haya ni mambo muhimu sana japo unaweze kuyaona si yamsingi kwa kudhani tu mwanaume vile alisha kubali kufunga ndoa na wewe haya si muhimu.
Wanaume tunatofautiana mambo mengi sana. kuna mwanaume anaethamini mahusiano yake yaliyo halali mbele za mungu bila kujali aliingia mahusiano hayo na mtu mwenye viwango gani kwa chochote kile katika uumbwaji wake huyo mwenza na vile avimilikivyo. Lakini pia uwezo wa kujitambua kwamba umekuwa nani baada ya kuingia kwenye ndoa na ni kwa jinsi gani kuchukuliana na mke wako kwa nyakati zote. Nachelea kusema wapo wengi tu wenye utambuzi mdogo kabisa kwenye haya mambo. Sitaki kumshutumu mumeo moja kwa moja lakini inaelekea kwa maelezo yako mume ni tatatizo/cahanzo cha hili tatizo maana wewe umekuwa ukumshauri mambo mengi kwa busara kubwa lkn yeye anabisha tu sababu ni mwanaume au sababu ya hadhi yako kama nilivyoeleza awali hawezi kukusikiliza.

Kwa uchache tu niseme wewe ni mke halali wa hiyo ndoa.....japo sina hakika ya imani gani.....lkn inatosha tu kwa mujibu wa sheria za nchi ambazo ni supreme mbele ya imani ninyi ndiyo wamiliki wa hizo mali hususani nyumba japokuwa huyo mtoto wake anaweza kuwa na sehemu na si umiliki wote kama anavyotaka kukutisha. Labda awe alijenga hiyo nyumba na huyo mwanamke mwingine kabla ya kukuoa japo pia si kweli kwa mujibu wa maelezo yako. Mumeo atakuwa na hulka ya kuongea na kuropoka aidha akikwazwa au kwa nia ya kutaka kukutocha tu ......sadist.... japokuwa ayaongeayo yanakuumiza. ushauri wangu tumia busara zako japo ziwe na kiasi kwa kutoruhusu maneno yake kutengeneza kidonda moyoni mwako. Jaribu kutafuta furaha itakayokufanya uwe huru hata pale anapotafuta kukuumiza. Atakapokuona umejawa amani na huumizwi na makwazo yake ndipo atagundua kuwa kumbe kazi aifanyayo ni bure na hakika atatafuta namna ya kurudi kwako na kukupigia magoti.

Utanisamehe nimeandika kwa haraka sana maana watu wamejaa mlangoni pa ofisi yangu wakihitaji niwahudumie kwa sasa. Nikipata muda nitakushauri vizuri zaidi na hakika faraja itakurudia tena. Pole sana na Mungu akupiganie.
 
Yaani shida iliyopo hapo ni kubwa sana dada yangu ndiyo maana anakupa majibun hayo ya kijeuri. Kuna kitu nyuma ya panzia ambacho wewe unajua au hujui. na kubwa katika yote ni mahusiano ya pembeni na mwanamke mwingine au mama mtoto waki na hiyo ndiyo sababau ya kuku ignore wewe na kukupa majibu makavu hivyo
 
Ulishawahi msaliti huko nyuma? Ulimfanyia au ulimuonyesha dharau au kiburi Maana wanaume tunatunza kumbukumbu hata miaka hamsini ya usaliti.
 
Pole kwa matatizo ya ndoa. Raha ya ndoa, hata kama ni mtafutaji wa familia, kile unachokipata ukione kama ni chako, mkeo na watoto. Lakini pia umenifungua macho. Kumbe kuna wanawake wiki 2 ni nyingi sana kwao! Namshukuru Mungu kwa kunipa mwanamke tunayeendena. Hata mwezi unapita, kutegemeana na mazingira, bila madhara yoyote.
 
Poole sana, ila nahisi kuna kitu ulishamkosea. Naye angepata fursa ya kuandika hapa makosa yako lazima tungejua nani mbaya.

Ila nachojua mwanaume mpaka kadiriki kufunga ndoa na wewe na akakuweka ndani, ujue alikupenda kwa dhati, ila kuna mahali pengine ulimkosea, kama sio wewe basi itakuwa mama mkwe wako anahusika, na kama si hivo basi kuna nguvu za giza.

Ila mi nilimpenda saana mke wangu nikamfungulia kila aina ya biashara zinafirisika tu, nikampa mtaji unakwisha tu, na mbaya zaidi hajawahi kuonyesha upendo wa dhati kwangu (hajawahi kuwa romantic), na mpaka sasa nampenda. Nimezaa naye watoto watatu wote wanasoma private schools.

Ki ukweli ananitesa saana, namvumilia tu kwa kuwa wanangu sipendi waje walelewe na mama wa kambo kwani wanaweza athirika kisaikolojia.

Nimetokea kuwachukia sana wanawake, siwezi kuwatetea hata kidogo, mke wangu anatumia fursa ya mimi kuwajali wanangu kunitesa na kuishi anavyotaka. Hivi naandika ujumbe huu nikiwa nimejilaza kitandani asbh hii nina mawazo sana huku nimenyimwa unyumba, nikaona bora niingie Jf kuperuzi nakutana tena na hii mada.

Siku nikimaliza majukum kwa wanangu na ishu zingine ndgndg hapa hom hakika naye atajuta. Atakuja kuandika hapa Jf kutaka huruma ya wanazego. Wanawake mnakera sana bhaana, siku janaume likifanya maamuzi magumu mnakimbilia jamii forum kutafuta huruma.

Pambaneni na madhambi yenu, ila samahani kama wee hauko hivo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Stockholm syndrome dear..wengi wanaumwa.
 
Mmhhh,mi mwanaume,lakini hii ni kumfanya mwingine mtumwa.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…