Ushawahi kuhisi upo single ndani ya ndoa?

Kichwa kinauma mamdogo, nikitulia tutaendelea na udadavuzi, btw amesema ameugua gafla masai dada, watu hawaoni kama huyu dada anahitaji msaada!
Ma mkubwa hali ni tete. Watu wakiamua kutoka ndoani tunawatukana na kuwaita majina mabaya na kuwaona ni wajinga na waliokosa uvumilivu. Sasa kwa hali kama hii jamani hadi mtu anaumwa mmmmmmmmmh
 
Hahhaaa pole sana..sio wote wako kama huyo wako
Mshauri tu vizuri huyu
 
Ma mkubwa hali ni tete. Watu wakiamua kutoka ndoani tunawatukana na kuwaita majina mabaya na kuwaona ni wajinga na waliokosa uvumilivu. Sasa kwa hali kama hii jamani hadi mtu anaumwa mmmmmmmmmh
Kwa hiyo hapa unaweza kupata justifications za kuvunja ndoa? Kwenda kinyume na maaandiko matakatifu.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo hapa unaweza kupata justifications za kuvunja ndoa? Kwenda kinyume na maaandiko matakatifu.



Sent using Jamii Forums mobile app
Niliongelea generally; nitakujibu specifially.

Ndoa ina msingi huu mkuu "mume mpende mke kama Kristo alivyolipenda kanisa; na mke mtii mumeo". Mahusiano yao hawa hayana upendo na sasa hivi na tendo la ndoa linasuasua. What do you call that kind of a relationship? Unaiita ndoa kwa misingi ya vyeti na pete + vows asizoziheshimu au? Ikifika stage ndoa inakuwa life-threatening; why not separating? The good thing is; masai still wants her marriage to work out

1 Wakorintho 7:4-5
4 Mke hana amri juu ya mwili wake, bali mumewe; vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake, bali mkewe.

5 Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, ili mpate faragha kwa kusali; mkajiane tena, Shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu.

Vipi hapo mume anaenda sawa na maandiko matakatifu?
 
Wiki 2 bila tendo la ndoa ni nyingi za kulalamika JF?
 
Wamama hawakosei kwenye ndoa huwa wanakosewa siku zote.
 
Ninachoona mwanamke anapambana na nguvu za giza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tafuta maana ya neno hili: "nymphomania".

ama pia hujasoma nilipomwambia HS ya kuwa inajulikana wanawake tunauwezo wa kusurvive muda mrefu bila kufanya mapenzi, na sifikirii ni sahihi wewe kudhani kudai haki ya kufanywa after two weeks ni ‘nymphomania’ na je ni dhambi kuwa na nymphomia?

hujajibu maswali yangu bado.
 
JF sio sehemu salama ya kuchukua ushauri unaoenda kuamua maisha tako. Huku ni sehemu salama ya kutua mizigo uliyoshindwa kuitua uraiani tu ila sio utatuzi wa matatizo kama haya.

-Humu utashauriwa na watu walio-single vijana wa kiume na wake ambao bado wanakula kwao.

-Huku utashauriwa na wanawake wasio ndani ya ndoa walioumizwa na wanaume kibao kilichobaki mioyoni mwao ni mwanaume nini bwana. Waogope saana hawa.

-Huku utashauriwa na wanaume walioshindwana na wake zao kwasababu zao wazijuayo wenyewe.

-Huku utashauriwa na single parents hasa wanawake.. hawa kamwe hawawezi kukupa ushauri wa kukujenga..hawaamini katika ndoa wengi wao.

Tafuta watu walioishi kwenye ndoa miaka na miaka na wanaojiheshimu kwenye jamii yako wapo wengi tu. Waeleze A- Z ya mkasa wako au kama wamekuwa wakiyashuhudia utapata mawili matatu ya kuchukua. Wao wanamjua mmeo ni mtu wa namna gani na wanakujua wewe ni mwanamke wa namna gani.

Ila hapa unatuomba ushauri kuntu kama huu tusiokujua tutasema nini? Hatumjui mmeo tutasema nini? Hili suala yapaswa uwajue wote kwa undani ndipo utie neno. Ndiyo maana nikauliza kwanini unahisi mmeo alianza kubadilika???
 
Kama huyo mumeo hajakutundika watoto wengi achana naye tu!!
Struggle For Success!
Hapa Kazi tu.
 

Wewe jamaa agiza kinywaji chochote ntalipa. Kuna kipindi alisema kwamba mume wake kampata humu humu, itakuaje kama jamaa atasoma hizi threads? Si ndio itakuwa kamwaga petrol kwenye moto!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…