Aisee pole sana kwa yanayokusibu. Binafsi nimejifunza jambo moja kubwa, katika haya maisha ili uweze kukabiliana na changamoto,unahitaji kujijengea 'a supreme sense of self-confidence and self-trust'. self-confidence ni kutokuwa na hofu kabisa na self-trust: ni kujua nini unatakiwa ufanye kwa wakati ambao jambo husika linatakiwa lifanyike, na kisha unalifanya bila kusitasita. Kusitasita kunazaa hofu na self-doubt. Kiwango cha selfdoubt ulichonacho kinalingana sawa na kiwango cha hofu, wasiwasi na mkanganyiko unaoupata.
Kwa hiyo, mimi nashauri ukae chini upembue mambo kwa uhalisia wake, moja baada ya jingine, kisha uamue nini cha kufanya next kulingana na majibu utakayojipa na hatimaye utekeleze utachoamua. Kwa mfano; wewe unadhani chanzo ni nini? Je, unaweza kufanya lolote kushughulikia hicho chanzo ili mambo yakae sawa? Kama huwezi, nini mbadala wake? Zipi faida na hasara za kubaki katika hayo mahusiano? Na nini faida na hasara za kujiondoa? Kipi kinakupa hofu zaidi na kwanini? Je, unaweza kukabiliana na kinachokupa hofu? Kipi kibaya zaidi (The worst thing possible) kinachoweza kutokea kama ukibaki kwenye mahusiano hayo au ukiondoka? Je, upo tayari kukabiliana nacho? endelea kujiuliza maswali kama hayo na ujipe majibu halisi (real answers)... kisha chukua hatua bila kusita.
Kwasababu kuna mawili yanaweza kutokea, aidha uwe proactive uchukue hatua mapema au uwe reactive usubiri mpaka utakapolazimika kuchukua hatua (when you will be forced to act bcoz you'll 've no choice). Na historia inaonesha watu wengi huwa wanalazimika kuchukua hatua wakati wameshachelewa, wakati wameshapoteza kila kitu, wakati hawana tena cha kupoteza... na ambacho huwalizimisha kuchukua hatua ni MAUMIVU MAKALI.
You either decide or the nature decides for you.
Nawasilisha.