Ushawahi kujichanganya kimapenzi mpaka ukawa unawaza hapo nyuma ulikosea wapi?

Ushawahi kujichanganya kimapenzi mpaka ukawa unawaza hapo nyuma ulikosea wapi?

Episode 11


maisha yakaendelea hapo nishabadili na namba za simu nikarudi kazini ila nikawa mlevi sana, kuna siku mpaka director alikua mmama mmoja hivi alinifukuza ofisini akaniambia we nenda kwanza mpaka kesho, barua za onyo nikawa nakutana nazo karibu kila wiki, Maisha yakaendelea nikaja kuona nikiendelea kufanya kazi dar sitapata amani ya moyo, nikaanza mipango ya kutafuta kazi sehemu nyingine kimya kimya nikaja kupata kazi mwanza ila nilitakiwa nisubiri kama miezi miwili ndo niripoti , sasa kuna siku nimekaa Mary akanipigia sijui hata namba zangu alipewa na nani, akanisihi sana tuonane nikamuambia sawa, basi badae tumeonana yupo smart kweli na kazini alirudishwa pale pale, akawa ananiambia twende ukachukue vitu vyako vilivyobaki, tukaenda home tukaishia kusex tu, mazoea yakaanza taratibu nikaona no this is not right nikamwambia tuache tutarudisha matatizo tu, nikaja kuamugaza naenda mwanza nahama huku, akakubali hivo hivo mpaka siku naondoka tulilala wote asubuhi niliondokea kwake



Mary kwa sasa ameshaolewa na ana mtoto mmoja, hua tunawasiliana sana yaani sana ila hatujawahi kuonana tangia hio siku naenda mwanza yaani hata nikiwa dar tulishakubaliana tusije onana kabisa, kuna siku nipo dar ananiita mikocheni huwez kuamini nilienda ila njiani roho iligoma nikarudi, hata leo hii nimetoka kuongea nae tunashauriana mambo mengi ya kimaisha



samirah ye bado hajaolewa na nina mawasiliano yake hua tunaishia kutaniana hapa na pale tu japokua nae sijawahi kumuona toka ile siku tunaachana akiwa bado chuo, 6 years ago!!!


Mimi sasa, mwanza ndo nikakutana na machizi wenzangu kwenye mapenzi nikapigwa matukio mpaka akili ikakaa sawa, ndo lengo la kuleta huu uzi ila muone kua niliacha wanawake wa aina gani na nikaja kutumbukia na kupigwa matukio na wanawake wa aina ipi, wanakuambia mkataa pema pabaya pamuita, hapa ndo sasa story inaanza rasmi wadau
Dah mapenzi kmmk
 
Hahah mwamba inaonekana wewe elimu imepita kushoto. Sasa suala la muda ambalo dunia imejiwekea mfumo ili tuelewane kwa pamoja ni suala la kulalamika kweli? Umeiona tu hiyo 1:42 ila hiyo aliyoandika 23:10 umeielewa. Nyie ndo mnaanza kulalamika kwanini hatua 75 za miguu zinakuwaje ekari moja 😂😂😂
Kula chuma 🏃
 
Hahah mwamba inaonekana wewe elimu imepita kushoto. Sasa suala la muda ambalo dunia imejiwekea mfumo ili tuelewane kwa pamoja ni suala la kulalamika kweli? Umeiona tu hiyo 1:42 ila hiyo aliyoandika 23:10 umeielewa. Nyie ndo mnaanza kulalamika kwanini hatua 75 za miguu zinakuwaje ekari moja 😂😂😂
Nadhani sijalalamika,ni kuelewasha Tu kiswahili cheti tukipe hadhi,huwezi kuandika saa 6:50 katika lugha ya kiswahili eti unamaanisha ni saa 12!

Tunachanganya mambo sana.

Ni sawa na siku hizi,watu wanatumia maneno ya kikenya bila kujua.
 
Back
Top Bottom