Ushawahi kujichanganya kimapenzi mpaka ukawa unawaza hapo nyuma ulikosea wapi?

Ushawahi kujichanganya kimapenzi mpaka ukawa unawaza hapo nyuma ulikosea wapi?

Sasa unabidi kichwa Cha Uzi wetu badala ya kuwa

Ushawahi kujichanganya kimapenzi mpaka ukawa unawaza hapo nyuma ulikosea wapi?​

Iwe

Ushawahi kujichanganya kusoma story ambayo ajimaliziwa maana mwenye nayo bado anajichanganya na mahusiano mpaka anawaza hapo nyuma ulikosea wapi?​

 
S3 epi 8

Basi bana maisha yakaendelea hapo G tunawasiliana tu ila si kama mwanzo Kwa machale tu na huku kwangu wakawa wamekata mguu nadhani ni kwa maelekezo ya mama mkwe, nikiwa nataka kuwaona mi ndo nakua wa kwenda nawasalimu naondoka zangu..



Ikapita kama mwezi Kuna siku nipo kazini mama mkwe anapiga anasema nimtumie Hela ya nauli Kuna mahali amepata Binti wa kazi, basi nikatuma zikapita kama siku 2 Binti wa kazi akawa amekuja, hapo Sasa nawaza mama mkwe atakua kwenye mkakati wa kunipiga pini kabisa nisije nikapata nafasi ya kua na G tena huku kama ilivyokua awali, nikasema hapa hakijaharibika kitu....


Muda ukaenda yule dada kaanza kuzoeana na mtoto ikafika wakati G anaweza kupata muda anatoka tukaonana ila sikuwahi kumruhusu kabisa aje kwangu maana mama mkwe alikua anapajua nikasema hapa niwe makini huyu mama kashahisi kitu anaweza kuja kunipiga ambush....


Fast forward.....


Penzi na G likaendelea hivo hivo kiwizi wizi tu hatukupata changa moto yoyote hapo katikati, hapo naye Sasa kaanza kunizoea sio kama mwanzo mnaweza Sasa mkakaa mkaongea mkacheka yaani kashakua huru, na mi nishanasa hapo nawaza huyu simuachi hata kikitokea nini



Matokea ya form 4 yakaja kutoka bahati mbaya hayakua mazuri Kwa upande wa G,ila nikawa nae karibu namwambia asijali Kila mtu kapangiwa njia yake katika maisha, ukiona huku pamezibwa ujue Kuna mahali pengine unapaswa upite, basi nikawa namshauri atafute tu chuo achague kitu ambacho anataka kufanya aende kusomea, akaniambia sawa ache niwaze ntakujulisha, hapo mama mkwe Sasa tukawa tunaongea Sana kuhusu swala la G ukizingatia mama mkwe ni mtu hakua na exposure Sana hivo akawa ananitegemea mimi Sana Sana kwenye ushauri


Zimepita kama wiki 2 siku nipo na G ndo ananiambia kama utaweza nitafutie tu mimi kazi yoyote nijishikishe kwanza mi naona mambo ya shule ntaenda kupoteza tu pesa huko, basi nikawa namshauri pale maana Kuna chuo nilishaanza Anza kuulizia nikawa namwambia asikate tamaa Bado ni mdogo awaze kufanya shule kwanza, ikaenda hivo hivo nae mama yake sio mtu wa kujali Sana akawa ananiambia huyu kama utaweza mtafutie sehemu yoyote apate kazi tu maana naona mambo ya shule ni kama hataki tena


Nikashauri wee mpaka nikachoka, badae nikaja mtafutia kazi Kuna mdada mmoja nilikua nafanya nae kazi alikua na cash point mjini kama viwili baada ya kumuomba Sana badae akamchomeka sehemu Moja akaanza kufanya kazi Sasa huko, hapo mama yake ana furaha tu anaona Bora hata mwanangu amepata mahali akiamka anajua pa kwenda



Akili za kitoto Sasa, hapo G anaanza kunishawishi afanye kazi hata miezi minne Ili aje amuombe mama yake aende kupanga Ili tuwe free Sasa, nikamwambia hapana we endelea tu kukaa nyumbani kwanza mambo mengine tutapanga huko mbeleni, na mtoto ashakuzoea Bora hata hio jioni mnakua wote ukirudi, maana hapo Sasa nawaza haya mambo ya mapenzi tutakuja kujiachia Sana itakua rahisi mama mkwe ajue jambo.



Hivo Sasa mara nyingi G akitoka kazini maana wao wanachelewa lazima tutakutana tu ndo aende nyumbani, maisha yakaendelea ivo ivo pakawa hapana shida Kila mtu ana amani.


Shetani Sasa nae sio ndugu Yako


G mzunguko wake wa hedhi nilikua naujua vizuri na yeye nilim downlodia application kabisa iwe inampa alert, Sasa tukaanza ujinga mmoja, siku ambazo ni za hatari tukaanza kutumia withdrawal method, Ile nikitaka kumaliza namalizia pembeni, kumbe hii njia ni ya kijinga Sana, nilikuja kuelewa Kwa gharama kubwa Sana


Kuna siku nipo na G hapo yeye ana kama miezi 6 kazini, na mwanangu hapo kashaanza kwenda shule, Kuna shule ioo jirani basi wanampeleka kanacheza cheza saa 6 anamfata huyo dada wake wa kazi, Sasa hio siku nipo na G ndo ananiambia ni kama hajaona siku zake lastly, aisee sikujibu kwanza kitu chochote nilihisi kama nimepigwa shoti, tukajipa moyo pale kua Kuna circle inacheza ye atulie kwanza, nikawa Sasa Sina Raha nimekua mtu wa mawazo yaani Kila siku namuulizia vipi, umeingia period??? Jibu ni hapana.... Ikaenda mpaka siku namwambia tafuta mahali ukacheki, jibu likaja positive ana mimba



Maisha yangu yakawa magumu ghafla hapo Sasa Nina mawazo Sina Raha, tukaacha na mambo ya kusex hapo na yeye Kila siku ananiambia ananitegemea mimi nimwambie tunafanyaje, kiukweli mimi sipendi na sio muumini kabisa wa abortion ila hio siku Kila nikiangalia option nilizonazo, na madhara ya maamuzi yangu naona Sina namna hapa ni abortion tu,katika kitu kilichokua kinanipa mawazo nakumbuka kipindi tupo chuo Kwa kuskia au kuona kabisa, Kuna cases nyingi za wadada walifanya abortion zikaenda tofauti Sana,wengine waliumwa mpaka kupostpone( kuahirisha) mwaka wa chuo, chuo mimba zinatolewa Sana hivyo nilishapata story za madhara huko



Nikawa nawaza Sasa ikienda vibaya mtoto wa watu akapata shida, tofauti na kuogopa reaction za Rachel na mama mkwe ila hapo na mimi Nina feelings nae namuwazia tu basi namuonea huruma


Upande mwingine nawaza timbwili la Rachel, huyu mama mkwe ataniona mi ni kiumbe wa aina gani? Mama yangu Sasa na sister ndo balaa wakiskia ndo itakuaje Sasa, watu walinishauri nikate mizizi na hii familia, wakafurahi hata walivyoskia tumeachana na Rachel,wakanishauri kikubwa niangalia mwanangu, waje waskie tena nimejisimika kabisa kwenye hii familia dah itakuaje


Nikapima option zote nikaona abortion is the way to go, siku nikamuita G nikamtuliza kweli kiakili tukaongea mambo mengi badae ndo nikampa hili wazo, kwanza akaruka mita mia, akaanza kulia, mara Ina maana muda wote ulikua unanchezea tu, huwezi kuniambia unanipenda alafu uniambie nitoe mimba, hapo akaongea wee maneno mengi mi hapo sielewi kabisa, namuulizia Sasa mama dada wakijua, akasema potelea popote ndo ishatokea Sasa, ongea Sana pale wee ila mwisho wa siku tutakosa muafaka badae akaondoka tukasema tutaongea siku nyingine, hapo hakuna Cha sex Wala nini kwanza mi mood ilishakata kabisa



Sasa bana kashaondoka hapo nakaa kama nusu saa naona G kanitumia sms ambayo kwangu mimi nilitafsiri kama ni ya dharau kwanza maana tangu nijuane nae kwanza ananiheshimu na kuniogopa, pili ikiwa na vitisho ndani yake, kaandika


"Ni wakati Sasa sahihi wa kusimama kama mwanaume, mwanaume hukabili si kukimbia changamoto, tafuta namna ya kujua unafanyaje na ukiendelea kuniambia nitoe hii mimba hizi habari ntazifikisha Kwa mama mwenyewe maana naona kama we unamuogopa Sana"


Fu*ck, nikasema " heeee tena "
 
Back
Top Bottom