BIG DOGG
JF-Expert Member
- Sep 15, 2024
- 1,869
- 2,707
ongeza epsod na iwe imeshibaOfisini mnasoma wote au?😀😀 Pole na majukumu Bado sisi tunamalizia wiki ya mapumziko
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
ongeza epsod na iwe imeshibaOfisini mnasoma wote au?😀😀 Pole na majukumu Bado sisi tunamalizia wiki ya mapumziko
Nilikua nawasimulia baada ya kusoma episodes za leo na kuanza kucheka kwa nguvu. Baba ako mdogo ni comedy wallahOfisini mnasoma wote au?😀😀 Pole na majukumu Bado sisi tunamalizia wiki ya mapumziko
HatariiiiiS3 epi 10
Mama namjua akianza kuongea hamalizi Leo sikumjibu chochote nikampotezea, kesho yake Sasa nawasiliana na ba mdogo yaani tunapanga mbinu utasema tuko vitani, kwanza akaniambia amefanya mawasiliano Kuna mtu kampata mwanza Mzee mmoja wa kwenda nae, akaniambia yule Mzee wa kwanza tulieenda nae wakati wa kujitambulisha Kwa Rachel hafai, anadai yule ni mlaini Sana hii vita hatoiweza inahitaji makamanda kweli, hapo mimi simbishii kitu chochote nipo kimya maana nilishamuachia msala apambane nao....
Ba mdogo akaja Sasa na idea Moja, operation ya kuua ndege wawili Kwa jiwe Moja....
Akaniambia hapa inabidi tulipue mabomu kotekote ibaki tu kazi ya kukabiliana na madhara yatakayojitokeza, jumapili akienda Kwa mama mkwe na mimi huku nikae na mama nimuambie tu Kila kitu, maana hata nisiposema akasema mama mkwe ni lazima tu atampigia mama, hapo Sasa naona nimeruka nimejichanganya tu, mama yangu namjua ataongea mpaka nyumba ipate ufa, ila nikiwaza msala wa mama mkwe kule naona Bora nipambane tu huku kule ni kwa moto zaidi, hapo Rachel yeye Bado Sasa, nawaza huyu nae hawezi kuacha ipite hivi hivi lazima tu ataleta vita ya aina yake,
Hua sifanyi kitu bila ya kua na plan b, nawaza haya mambo yanaweza yakaenda tofauti kabisa na tunavyotarajia hivo plan b yangu ni kua nikiona mambo yameharibika Sana nifanye mpango mtoto nimlete huku Kwa mama maana nilihofia Rachel anaweza pata sababu ya kumchukua mtoto....... Nikishamleta huku mimi Sasa nibaki nipambane na lolote litalokuja
Usiku wa deni haukawi kufika, jumapili hio hapo, nipo busy na askari wangu( ba mdogo) tunapanga mipango wa mwisho, nikampa idea usiende mikono mitupu nunua zawadi za mama mkwe na mtoto kwanza mpate hata pa kuanzia mkienda, Sasa ba mdogo hii ishu yeye anachukulia simple tu yaani anasema " hii ya Leo Haina Cha zawadi Wala nini, Leo tunaenda uwanja wa vita zawadi za nini tena"
Mimi huku swala la kumuambia mama likanishinda, Kuna rafiki yake mmoja mama mtu mzima Sana tulikua tunatenganishwa na ukuta tu huyu mama alikua mcheshi na simple Sana, nikawa nimeshamuambia majanga yote nikamwambia jumapili we njoo umueleze tu huyu Mzee mwenzako akasema hakuna shaka.........
Hio siku yule mama kafika Sasa home, tumekaa Kaa pale ikabidi mi nizuge nikatoka zangu nimuache Sasa afikishe msala huku, nimetoka nimekaa bar Moja nampigia ba mdogo kujua kafikia wapi, anapokea anauliza vipi wewe uko wapi? Namuambia npo bar hapa natuliza kichwa kidogo, jamaa nae anacheka anasema na si tumepitia hapa tunapiga Moja Moja kwanza hii vita sio ya kwenda ivi ivi
G hapo tunawasiliana kawaida ila sijamwambia chochote asije akavujisha taarifa akaharibu, ikafika muda ba mdogo ananiambia wapo njiani wanakaribia kufika....
Mimi ni nani??
Nikachukua Simu yangu, mama mkwe nikamtupia kwenye blacklist, Rachel nae nikamuunga huko huko.... Hapa nasema mpaka nipate kwanza feedback kutoka Kwa ba mdogo ndo ntajua Cha kuongea nao....
Basi wao wakafika kule hapo tukaacha kuwasiliana, hapo Nina mawazo najiuliza mbona nimejiingiza kwenye matatizo kiasi hiki, upande wa mama Wala siwazi Sana najua tu atasema mpaka nikome, huku Sasa Kwa mama mkwe.... Nikakaa pale yaani navyosubiri Simu ya ba mdogo ni sawa na mtu ammepeleka mwenzie labor anasubiri ajifungue
Nikiwa nashusha bia taratibu pale, mama yangu akaanza kupiga nikawa kimya tu Wala simpokelei, akapiga kama mara tatu mie kimya tu.... Nakaa kama dakika 10 naona sms kutoka kwake
" Hivi wewe hizo akili zako umezitoa wapi , mbona baba Yako hakua na akili kama hizo"
Nikawaza hapa bomu la kwanza lishalipuka...
Sijapata hata muda wa kuwaza ba mdogo nae anatuma sms
" Mzee hii Ngoma nzito, tushachemka huku"
Obeja mayoHappy new year 🎆 too
Unatakiwa ujicontrol mwenyeweSiku Fanya Kwa kupenda ila kulikuwa na sababu zilizonisukuma kufanya hivyo.
Mbona hamkusubiri hata mimba ikue ndo msemeS3 epi 12
Mama namjua hata hanipi shida Sana, alivyosema hivyo yule mama jirani Sasa akaanza " na we muache kijana wangu bana ", akaniambia njoo tukae hapa, kufika akaanza Sasa kujisemesha.... " Ila sio mbaya kuliko kuja kurundika watoto Wana damu tofauti tofauti wanakua na tabia za ajabu ajabu tu, Bora hata Sasa tupate wajukuu wengine hapo hapo"
Is this supposed to make me feel better? Hapana!!! Bado Nina mawazo makali Sana hapo, kuja kumcheki maza nae anankata jicho tu, akaanza
"Uzuri mimi kipindi kile mlivyokua mnaenda kuoa na baba zako bila kunishirikisha nilikuambia kabisa yatayowapata msinihusishe, na wewe una baba wengi tu ila kutwa unafanya mambo Yako na hao ambao hawana akili maana mnajuana akili wenyewe"
Nikaona Hawa wananchanganya tu nikaaga nikaingia zangu ndani, kufika ba mdogo nae anapiga, ananiambia Kwa aina ya huu msala we rudi tu huku tuunganishe nguvu maana huku Kuna balaa, nikamwambia siwezi kurudi mwanza mpaka nipate plan kwanza, yeye aendelee kupambana tu huko, hapo naanza kumwambia mimi huku nimemaliza kazi yangu wewe kilichokushinda ni nini, ananiambia " we Mzee huku ni pa moto mpaka yule Mzee niliyeenda nae alitaka kukimbia" nikamwambia acha niwaze Sasa tutajua Cha kufanya....
Hapo Simu ya G haipatikani nikaamua nitulie tu Sasa nafanyaje, nikapata wazo la kumpigia yule dada wa kazi wa mtoto nikasema hapana hapa ntaharibu anaweza kua na mama mkwe acha kwanza nikae kimya
Zinapita dakika, Simu inaita, kuangalia anapiga yule dada ya mgahawa rafiki yake na Rachel wa kipindi kile, hapo tulikua tunaongea nae Kwa nadra Sana, nikasema eeheee hapa pamekucha, nikapokea pale tukaanza salimiana analeta story za hapa na pale hapo namsikilizia tu najua Hana jipya itakua ni mambo ya G tu, basi badae anaanza Shem uko wapi? Nikamwambia nimesafiri, anasema Sasa "Shem ndo umefanya nini tena huku? Rachel kanipigia analia anasema mama yake ana Hali mbaya naona umeamua kumuua mama yake Sasa" .... Hapo nashangaa tena, mimi tena namuua mama yake?? Tukaongea pale ananiambia Rachel kesho anakuja huku..... Nikamwambia sawa hebu niache nipumzike kesho nikipata wasaa ntakupigia tuongee tukiwa tumetulia
Hapo nawaza Sasa ndo nimefanya nini? Mbona Kila kitu kinaenda ovyo tu, nawaza huyu Rachel akija atamfanya nini G? Huyu si anaweza hata kumpiga mpaka mimba itoke, akili ya kurudi mwanza inanijia, ila Sasa naenda kufanya nini Sina hata plan kabisa.... Nikasema acha ntajua
Hio siku sikulala, umiza Sana akili, badae nikapata wazo, katika wale wazee tuliowakuta tulivyoenda kujitambulisha Kuna wawili tulibadilishana namba, mmoja hakuwahi kuntafuta ila Kuna mmoja ni Mzee wa makamo Sana aliniambia Rachel ananiita mimi Babu, Sasa huyo Mzee Kuna kipindi nipo kazini aliwahi kunipigia akaniambia mwanangu jino linanisumbua nisaidie Hela nikalitoe, nakumbuka nilimtumia pesa kiasi, hio siku jioni nikarudi nikamwambia Rachel, akachukia kweli akaniambia Hawa nawajua ukiwaendekeza shida zao zote utakua unapewa wewe, akachukua Simu akawablock wote wawili
Ambae hafai Leo, ipo siku atafaa tu, kesho yake ikabidi Sasa yule Mzee nimtoe kifungoni(blacklist) nikampigia nikamkumbusha pale akawa kanikumbuka, nae anasema alipoteza Simu nikasema afadhali asije kua alikua ananipigia Simu inadunda, basi sikumwambia chochote nikamwambia yule rafiki Yako( ba mdogo Sasa) yupo mwanza mimi nimesafiri alisema akuone akusalimu kabla hajaondoka akasema sawa, badae nikamtumia yule Mzee kama elf 50 hapo sijamwambia kwamba Nina msala mwingine na mabinti zake, nikasema huyu ngoja nimuweke karibu badae anaweza kua msaada kwangu
Ba mdogo nae namcheki, ndo Nampa plan b, akaonane na yule Mzee mahali, wapige zao vyombo badae tu ndo amueleze Sasa, maana swala la kurudi Kwa mama mkwe lishakua haliwezekani tena, huyo Mzee ndo ataenda kuongea nae Sasa, wakae kifamilia watupe jibu Sasa, ba mdogo akasema " sawa hakuna shida Bora hata maana na mimi nilikua nataka nikuambie Kwa yule mama nisingeenda tena wale majirani wakali kweli wasije wakanibadilikia"
Ba mdogo nae mission town hapo ananiambia " angalia Sasa uniongezee balance kidogo si unajua napambana" namwambia sawa kesho ntakutumia
Yule dada co worker nae badae ananipigia anauliza yule Binti(G) uliyeniletea mbona hajaingia kazini? Hapo namzuga hebu ngoja nijaribu kuwauliza Sasa, akaniambia unaona Sasa ndo shida ya kuleta watu Kwa kujuana, nikamwambia tulia ntakurudia nikipata jibu, akasema sawa
Sasa kesho ba mdogo akakutana na yule Mzee, hapo nimeweka Simu standby nasubiri wakimaliza kuongea ba mdogo aniambie mambo yameendaje, kabla hata hawajamaliza ba mdogo anatuma sms " we Mzee Fanya uje tu huku, hii kazi uliyonipa siyo ya kufanywa na mtu mmoja, hapa ndo tumejichanganya kabisa"
Ukisimama nchale ukiinuka nchale 🏹🏹Ugali moto mboga moto bakuli ya bati.....
Hakuna kitu sipendi kama " kuahirisha tatizo"Mbona hamkusubiri hata mimba ikue ndo mseme
Mbona hamkusubiri hata mimba ikue ndo mseme
🤣🤣🤣 aisee lakini si- changamoto Sana Hao !?King ujawai kukutana na pisi za uswazi wewe hatari, wana majina yao hayo utasikia baba tombombo.
Nafsi haizeeki That's why Tuna Tumia I'd fake humuMunaohangaika pat alete hii story nikiwacheki kwa makini munacheza na miaka kuanzia 20 had 40.
Ukivuka 41 mwanaume/ke huwezi ukambebeleza mtu akupe story ya namna alivyongegeda mbususu ya grace maana yake utakuwa umevuka enzi za nyenge kichaaa.