[emoji1787][emoji1787][emoji1787] mission town karudisha mpira Kwa kipa, mama mkwe anakabia kwajuuhahaha ukiona dili limemshinda mission town kakurudishia mwenyew bas jua kazi ipo
FactNi bora kuweka wazi mapema kuliko kuwachia wenyewe waijadili mimba G angeweza kumezeshwa maneno kwa vitisho akubali kua alibakwa wakati wanaenda kulala kule na mtoto, familia zetu za ki africa unazijua, bora hivyo kuliko kupewa kesi ya kubaka
Huo mstari wa mwisho nimecheka sanaS3 epi 10
Mama namjua akianza kuongea hamalizi Leo sikumjibu chochote nikampotezea, kesho yake Sasa nawasiliana na ba mdogo yaani tunapanga mbinu utasema tuko vitani, kwanza akaniambia amefanya mawasiliano Kuna mtu kampata mwanza Mzee mmoja wa kwenda nae, akaniambia yule Mzee wa kwanza tulieenda nae wakati wa kujitambulisha Kwa Rachel hafai, anadai yule ni mlaini Sana hii vita hatoiweza inahitaji makamanda kweli, hapo mimi simbishii kitu chochote nipo kimya maana nilishamuachia msala apambane nao....
Ba mdogo akaja Sasa na idea Moja, operation ya kuua ndege wawili Kwa jiwe Moja....
Akaniambia hapa inabidi tulipue mabomu kotekote ibaki tu kazi ya kukabiliana na madhara yatakayojitokeza, jumapili akienda Kwa mama mkwe na mimi huku nikae na mama nimuambie tu Kila kitu, maana hata nisiposema akasema mama mkwe ni lazima tu atampigia mama, hapo Sasa naona nimeruka nimejichanganya tu, mama yangu namjua ataongea mpaka nyumba ipate ufa, ila nikiwaza msala wa mama mkwe kule naona Bora nipambane tu huku kule ni kwa moto zaidi, hapo Rachel yeye Bado Sasa, nawaza huyu nae hawezi kuacha ipite hivi hivi lazima tu ataleta vita ya aina yake,
Hua sifanyi kitu bila ya kua na plan b, nawaza haya mambo yanaweza yakaenda tofauti kabisa na tunavyotarajia hivo plan b yangu ni kua nikiona mambo yameharibika Sana nifanye mpango mtoto nimlete huku Kwa mama maana nilihofia Rachel anaweza pata sababu ya kumchukua mtoto....... Nikishamleta huku mimi Sasa nibaki nipambane na lolote litalokuja
Usiku wa deni haukawi kufika, jumapili hio hapo, nipo busy na askari wangu( ba mdogo) tunapanga mipango wa mwisho, nikampa idea usiende mikono mitupu nunua zawadi za mama mkwe na mtoto kwanza mpate hata pa kuanzia mkienda, Sasa ba mdogo hii ishu yeye anachukulia simple tu yaani anasema " hii ya Leo Haina Cha zawadi Wala nini, Leo tunaenda uwanja wa vita zawadi za nini tena"
Mimi huku swala la kumuambia mama likanishinda, Kuna rafiki yake mmoja mama mtu mzima Sana tulikua tunatenganishwa na ukuta tu huyu mama alikua mcheshi na simple Sana, nikawa nimeshamuambia majanga yote nikamwambia jumapili we njoo umueleze tu huyu Mzee mwenzako akasema hakuna shaka.........
Hio siku yule mama kafika Sasa home, tumekaa Kaa pale ikabidi mi nizuge nikatoka zangu nimuache Sasa afikishe msala huku, nimetoka nimekaa bar Moja nampigia ba mdogo kujua kafikia wapi, anapokea anauliza vipi wewe uko wapi? Namuambia npo bar hapa natuliza kichwa kidogo, jamaa nae anacheka anasema na si tumepitia hapa tunapiga Moja Moja kwanza hii vita sio ya kwenda ivi ivi
G hapo tunawasiliana kawaida ila sijamwambia chochote asije akavujisha taarifa akaharibu, ikafika muda ba mdogo ananiambia wapo njiani wanakaribia kufika....
Mimi ni nani??
Nikachukua Simu yangu, mama mkwe nikamtupia kwenye blacklist, Rachel nae nikamuunga huko huko.... Hapa nasema mpaka nipate kwanza feedback kutoka Kwa ba mdogo ndo ntajua Cha kuongea nao....
Basi wao wakafika kule hapo tukaacha kuwasiliana, hapo Nina mawazo najiuliza mbona nimejiingiza kwenye matatizo kiasi hiki, upande wa mama Wala siwazi Sana najua tu atasema mpaka nikome, huku Sasa Kwa mama mkwe.... Nikakaa pale yaani navyosubiri Simu ya ba mdogo ni sawa na mtu ammepeleka mwenzie labor anasubiri ajifungue
Nikiwa nashusha bia taratibu pale, mama yangu akaanza kupiga nikawa kimya tu Wala simpokelei, akapiga kama mara tatu mie kimya tu.... Nakaa kama dakika 10 naona sms kutoka kwake
" Hivi wewe hizo akili zako umezitoa wapi , mbona baba Yako hakua na akili kama hizo"
Nikawaza hapa bomu la kwanza lishalipuka...
Sijapata hata muda wa kuwaza ba mdogo nae anatuma sms
" Mzee hii Ngoma nzito, tushachemka huku"
Bila shaka wewe huwa ni mtaalam wa kuangalia zile muvi ngumu ambazo wengi huwa hatuzielew,yaan ni mpaka utulie au uwe na akili ya kujiongeza ndo unaielewaNi bora kuweka wazi mapema kuliko kuwachia wenyewe waijadili mimba G angeweza kumezeshwa maneno kwa vitisho akubali kua alibakwa wakati wanaenda kulala kule na mtoto, familia zetu za ki africa unazijua, bora hivyo kuliko kupewa kesi ya kubaka
Patrick utskapo fika mwisho mwa kisa hiki please weka contact zako mkuu, February nakuja meanza likizo, tuonane walau tupate bia aiseMna catch Sana ma feelings ila uzuri mnarudi tu, siku ya kujitambulisha tulikutana na wazee kama 6, Rachel ndo overall akaniambia " sijui hata mama kawatoa wapi"... Huyu Mzee katika kubadilishana namba ndo akaniambia mimi Rachel ananiita Babu!!!
Na kuhusu kutuma hio Hela ndo Rachel akaniambia Hawa sio wa kuwaendekeza watahamisha shida zao kwako,
Sasa ni kipi ambacho hakieleweki hapo?
🤣🤣Kanyaga Twende Baba Grace, Tumechelewa sana
Hata mimi natabiri hivoMimi siyo nabii, ila Grace naye atagawa utamu
Kumbe ni threadWakuu natumaini wote mpo salama na mnaendelea vyema kusherekea sikukuu hizi
Dah, kwa upande wangu mimi sipo sawa kabisa hapa najiona mkosefu sana na sijui hata jamii itanielewa vipi, nimekuja huku naamini kuna wakubwa na watu wenye busara naweza pata ushauri.. Nayopitia kwa sasa na jinsi nilivyokua na mahusiano imara huko nyuma ni mbingu na ardhi. Kisa ni kirefu kiasi chake hivyo naomba muwe wavumilivu
Mikosi ilianza kama miaka 7 iliyopita nikiwa nimemaliza chuo, nilikua na maisha bora sana yasiyo na misukosuko yoyote, nilianza mahusiano na mrembo mmoja tukiwa form four wote sema shule tofauti, yeye akisoma shule ya bweni ya wasichana pekee na mimi kipindi icho niko boarding school boys tupu, huyu binti mpaka kumpata nilitumia sana nguvu acha tu hua sitaki hata kukumbuka, ni binti ameshika sana maadili sidhani kama kuna binti wa namna hiyo endelea kufatilia huu mkasa utaelewa kwanini nakuambia hivo....ili iwe rahisi acha tumuite mary japo sio jina halisi ntajitahidi kuficha codes kadhaa
Mary alikua ametoka familia yenye uwezo mkubwa tu sana na yenye maadili mema, mama yake akiwa na wadhifa mkubwa tu serikalini na mzee wake akiwa mfanyabiashara, hatukua majirani bali nilikutana nae shuleni kwao nikiwa nimeenda kuhudhuria mahafali ya dada yangu mkubwa, bado hio siku naikumbuka kama jana kweli mapenzi yana nguvu unaweza kumuona mtu ukakaa wiki nzima bila kumtoa akilini kwako, sikufanikiwa hata kumsemesha hio siku nikawa nimeondoka na mawazo kibao tu huku namuwaza mtu ambae nilikua na imani sitokaa nije nimuone tena maishani..
Basi bana maisha yakaendelea mpaka siku nakumbuka nipo naangalia cd ya graduation ya sister kuna kipande walikua wanaimba madarasa ya chini ndipo nikamuona Mary bana, hapo nilikua nishaanza kusahau kuhusu yeye, nikamuita sister nijajikaza tu nikamuuliza unamjua huyu binti? Akamuangalia akajibu " vipi unamjua kwanini unaniuliza?" Nikamuambia hapana simfahamu ila nakumbuka nilimuona nilivyokuja shuleni kwenu kipindi kile, sister akaniambia anha huyo anaitwa Mary(disguise name) ni mdogo wake na fulani.... Akaniuliza vipi kuna nini...? Nikajibu hakuna kitu kwani wao wanakaa mkoa gani, uzuri akaniambia wanakaa mkoa mmoja na sisi tulipo, hapo mapigo ya moyo yanaenda kasi sana
Basi kila nikipata muda nikawa namdadisi sister kuhusiana na yule binti mpaka kuna siku sister akaniambia na wewe nimechoka na maswali yako ngoja ntakuombea namba kwa dada yake, baada ya kama siku mbili sister akaja akanipa ile namba hapo nimechanganyikiwa nashindwa hata nianzie wapi,nikaja mtafuta kwa njia ya sms akanijibu nikatumia nguvu sana kujitambulisha uzuri alikua anamjua sister, akawa anakomaa tu anauliza unataka nini toka kwangu nikamuambia tukiwa marafiki itapendeza akanijibu hakuna shaka....
Nikaja kumuomba nimuone kabla shule hazijafunguliwa tukaja kuonana sehemu moja alikuja na mdogo wake ila hatukukaa sana wao wakaondoka,mawasiliano yakaendelea kwa njia ya barua kipindi hicho kishule shule sasa, kufika form 4 ndo nikaja kumfungukia hisia zangu kwake nakumbuka alikua mkali mpaka nusu urafiki ufe, lakini sikukata tamaa mpaka akaja kunikubalia tukawa wapenzi rasmi
Huyu binti alikua na msimamo sana maana hatukufanya chochote mpaka tukaja kumaliza six nakumbuka kwa mbinde nilimvunja usichana hio siku alilia sana akaniomba nisije kuacha kumuoa, kwa uzuri na tabia zake hakika nilishajihakikishia hapa mke nimepata, tukachaguliwa wote udsm hakika nilifurahi sana nikapanga ghetto huko ndo mapenzi yakawa rasmi sasa, jumatatu naenda nae chuo jioni namuacha anakaa hostel za chuo mpaka ijumaa tukitoka tunaenda wote ghetto mpaka jumatatu tena, hakika Mary alikua mzuri sana ndani ya muda watu wengi sana wakawa wanamjua, nakumbuka kuna siku nipo hall kwao tupo room wakaja wadada flani nilikua nasoma nao kozi moja Mary kuwaambia kua mi ni boyfriend wake wale wadada kila tukikutana nae lecture hall wakawa wananiambia we kaka ulimpata wapi binti mrembo vile
To cut the story short, Mary hakuwahi kuniletea mauza uza yoyote kipindi tupo chuo, na ujinga sikufanya mwingi maana hakuna weekend yoyote ambayo sikua nae, maisha yakaendelea mpaka tukamaliza chuo mi nikapata kazi mwenye government institution moja ofisi zake zipo posta yeye akapata kazi kwenye private firm, after a while tukahamia kwenye nyumba nzima Mungu akajalia tukanunua na usafiri, asubuhi nampeleka job namuacha jioni anatoka anakuja ofisini kwangu ananisubiri mpaka natoka tunaenda wote home maana mi nilikua nachelewa kutoka, sikua na wasiwasi na Mary maana kuanzia chuo alishatongozwa sana na alikua akiniambia tu naomba uniamini siwezi kufanya ujinga
Basi tukaanza kuishi maisha ya Mume na mke rasmi, uzuri kwao wote kasoro wazazi tu ndo walikua hawanijui, na kwetu ivo ivo, tukaanza kabisa na kupanga mipango ya kutambulishana makwetu, dah kumbe bana ukipanga hivi shetani nae anapanga vile, nakumbuka kuna birthday moja nilihudhuria nikakutana na msichana mmoja wa kisomali mixture kidigo alikua anasoma chuo cha uhasibu TIA aisee najuta sana hio siku maana nahisi masaibu yangu yote mpaka leo hii nakula christmas kinyonge ivi yalianzia hapa...
Endelea kunifatilia naandika leo leo hii mpaka iishe hata kama ni saa 7 usiku
Elewa story acha kukurupukaSio kusubiri mimba ikue ilitakiwa wapige kimya tu,angemuachia G ndo ajue atamwambia vp mama ake kuhusiana na huo ujauzito,sjaona umuhimu wa kwenda kujisema ni kama walikuwa wanaenda kujigamba kwa mama mkwe kwamba sie ni kiboko wa kuto mb
hAta hvyo hii ni hadithi tu kwasasa,(mwanzo tuliambiwa Recho alikuwa hawajui wale wazee,leo tunaambiwa mzee mmoja Recho alikuwa anamuita babu na Pati aliwah msaidia hela ya kung'oa jino Recho akasema huwajui hawa watahamishia shida zao zote kwako)
Leta Uzi utuambie wameru walikufanyaje😂😂Ingia kwenye 18 mmachame au mmeru
Ah ha apo Baba mdogo ameta tahadhali maana mnaweza chapwa viboko 70 ili kuondoa mikosiS3 epi 12
Nikawaza nikasema ba mdogo nae Sasa mbona namuamini ila Kila anapogusa anapigwa za uso, huyu Mzee kamshindwa tena? Mbona balaa Sasa hapa.... Anyway nikasema ngoja amalizane nae atanambia imekuaje tena
Hapo mawasiliano Sasa yashakua magumu, mama mkwe ndo kabisa siwezi hata kumgusa, ikabidi nimpigie dada wa kazi wa mtoto, huyu nilikua naongea nae mara chache Sana , akanisalimu pale naulizia Hali ya mtoto akasema yupo sawa, nikamwambia hebu Kaa sehemu mwenyewe alafu unitafute, akaniambia usikate Simu ngoja nitoke nje, alivyofika nje ndo namuambia hebu Sasa niambie nini kinaendelea huko
Ndo ananiambia mama anaumwa, yupo Kwa jirani hapo rafiki yake ndo wanamuuguzia huko, haya, namuulizia G, huyu dada nae anasema G kuanzia asubuhi aliondoka pale hajarudi mpaka Sasa... Kwa Io ye amebaki mwenyewe na mtoto tu ndani, Sasa mama mkwe hua Nampa Hela ya matumizi ya Kila mwezi nikawaza huyu nae ndo anaumwa unaweza Kuta hawapati Kila kitu mtoto ataanza kuteseka Bure
Basi yule dada hata alikua hajui password ya m pesa yake, nikamuelekeza dukani akapewa namba ya wakala nikatoa pesa kidogo nikamwambia mtoto akihitaji kitu uwe unamchukulia Sasa, akasema sawa, nikadadisi nikajua Rachel hajafika Bado ila aliskia wanasema Binti Yake mkubwa yupo njiani.... Nikajua atakua Rachel huyo
Badae Sasa namcheki ba mdogo, Sasa kumbe yule Mzee bana baada ya kumchukua maelezo kidogo Mzee akawa mbogo, vita yake kwanza anasema tuna dharau Sana, kwamba hatukupeleka mahari ya Rachel kwanza hio ni dharau kubwa, alafu Kwa kua tumeshawaona wao ni wajinga Sana tumeamua kuzalisha tena hapo hapo maana tumezoea vya Bure( aisee Kuna wazee Wana midomo)
Ba mdogo akajaribu kuleta Sasa pale Mzee haelewi Wala nini ikabidi kikao kife, Sasa kumbe bana kipele kikapata mkunaji( hIi nilikuja kujua badae).... Yule Mzee akamuambia Mzee mmoja kati ya wale tuliowakuta( Hawa wazee walikua kwenye ukoo wa kina Rachel upande wa mama huko maana walikua bila baba)... Ila inaonekana hawakua na ukaribu hata na mama Yao kivile, Sasa bana siku hio hio wakashikana mguu Kwa mguu mpaka Kwa kina Rachel, kufika kule wakamuanzishia varangati tena mama mkwe, kwamba ukoo unadhalilishwa yeye anakaa kimya anashindwa hata kutoa taarifa Kwa wazee, Sasa wakasema wao ndo watashughulikia hilo jambo mpaka mwisho wake ujulikane
Ba mdogo hapo kaniambia we subiri tu kwanza huyu Mzee alisema atashauriana na mwenzake alafu atampa jibu, kweli walivyotoka Kwa kina Rachel wale wazee wakampigia ba mdogo wakawa tena wamekutana nae mjini, mimi hapo naskilizia tu, baada ya kuanza kufanya mazungumzo Kuna mda ba mdogo akanipigia, Ile kuongea nae akaniambia bwana mdogo nipo na wazee hapa ngoja nikupe tu baadhi ya utaratibu wakiwa na wao wanaskia
Sasa walee wazee wakamwambia ba mdogo hapa kwanza kabla ya yote inabidi tambiko lifanyike, mambo ya kuondoa mikosi maana wanasema ishakua mkosi kwenye ukoo wao, Kwa Io wakamuelekeza vitu vyote vinavyotakiwa na inabidi tuvinunue sisi, wao wakadai hawawezi kufanya Hilo tambiko, Kuna wazee ambao ni wakubwa kwao na wamewahi kufanya tambiko kama hili ndo wanaruhusiwa, inabidi wakawatafute, wakaombe na ruhusa kutoka Kwa mkuu wao wa ukoo.... Basi wakasema inahitajika ngombe mmoja na mbuzi dume wawili, Kuna aina ya nguo za kimila za wale wazee wa tambiko na makorokoro kibao wakasema wakishajua tarehe ya tambiko itabidi tulipe hivo vitu kwanza, alafu tambiko likiisha ndo tukae Sasa kikao....
Basi ikabidi niseme tu nimeelewa, ba mdogo akakata akaniambia ngoja tuendelee ntakujulisha nikamwambia sawa, narudi Sasa Kwa dada wa kazi ananiambia G hajarudi Bado, ila Kuna mdada mwingine kaja nikajua atakua Rachel huyo
Hapo nawaza huyu G nae kaenda wapi, na mbona hapatikani, na kama Rachel karudi G ataweza kweli kurudi nyumbani, nikasema Cha msingi awe salama tu hayo mengine tutajua
Sa ba mdogo amekata Simu akaanza kutuma sms " mwanangu Hawa wazee tusikubali watupelekeshe, Hawa tukiwasikiliza Kila kitu watakuja kutufilisi"
Sasa hapo mi namshangaa maana ye ndo Yuko nao huko, anashindwa nini kuongea nao, nikamjibu Mzee we pambana huko mi Niko mbali ntafanya nini Sasa akaniambia sawa hakuna shida
Nimekaa tena kidogo sms tena ya ba mdogo " Hawa wazee wanasema siku ya tambiko lazima tuwepo hasahasa wewe, tuwe makini Mzee Hawa watu huku ni wajinga Sana tunaweza kwenda kichwa kichwa tukaishia kuchapwa viboko na uzee huu"
Nikabaki nashangaa
shusha nyingne mkuu..S3 epi 12
Nikawaza nikasema ba mdogo nae Sasa mbona namuamini ila Kila anapogusa anapigwa za uso, huyu Mzee kamshindwa tena? Mbona balaa Sasa hapa.... Anyway nikasema ngoja amalizane nae atanambia imekuaje tena
Hapo mawasiliano Sasa yashakua magumu, mama mkwe ndo kabisa siwezi hata kumgusa, ikabidi nimpigie dada wa kazi wa mtoto, huyu nilikua naongea nae mara chache Sana , akanisalimu pale naulizia Hali ya mtoto akasema yupo sawa, nikamwambia hebu Kaa sehemu mwenyewe alafu unitafute, akaniambia usikate Simu ngoja nitoke nje, alivyofika nje ndo namuambia hebu Sasa niambie nini kinaendelea huko
Ndo ananiambia mama anaumwa, yupo Kwa jirani hapo rafiki yake ndo wanamuuguzia huko, haya, namuulizia G, huyu dada nae anasema G kuanzia asubuhi aliondoka pale hajarudi mpaka Sasa... Kwa Io ye amebaki mwenyewe na mtoto tu ndani, Sasa mama mkwe hua Nampa Hela ya matumizi ya Kila mwezi nikawaza huyu nae ndo anaumwa unaweza Kuta hawapati Kila kitu mtoto ataanza kuteseka Bure
Basi yule dada hata alikua hajui password ya m pesa yake, nikamuelekeza dukani akapewa namba ya wakala nikatoa pesa kidogo nikamwambia mtoto akihitaji kitu uwe unamchukulia Sasa, akasema sawa, nikadadisi nikajua Rachel hajafika Bado ila aliskia wanasema Binti Yake mkubwa yupo njiani.... Nikajua atakua Rachel huyo
Badae Sasa namcheki ba mdogo, Sasa kumbe yule Mzee bana baada ya kumchukua maelezo ba mdogo,Mzee akawa mbogo, vita yake kwanza anasema tuna dharau Sana, kwamba hatukupeleka mahari ya Rachel kwanza hio ni dharau kubwa, alafu Kwa kua tumeshawaona wao ni wajinga Sana tumeamua kuzalisha tena hapo hapo maana tumezoea vya Bure( aisee Kuna wazee Wana midomo)
Ba mdogo akajaribu kuleta Siasa pale Mzee haelewi Wala nini ikabidi kikao kife, Sasa kumbe bana kipele kikapata mkunaji( hIi nilikuja kujua badae).... Yule Mzee akamuambia Mzee mmoja kati ya wale tuliowakuta( Hawa wazee walikua kwenye ukoo wa kina Rachel upande wa mama huko maana walikua bila baba)... Ila inaonekana hawakua na ukaribu hata na mama Yao kivile, Sasa bana siku hio hio wakashikana mguu Kwa mguu mpaka Kwa kina Rachel, kufika kule wakamuanzishia varangati tena mama mkwe, kwamba ukoo unadhalilishwa yeye anakaa kimya anashindwa hata kutoa taarifa Kwa wazee, Sasa wakasema wao ndo watashughulikia hilo jambo mpaka mwisho wake ujulikane