Mpaji Mungu
JF-Expert Member
- Apr 24, 2023
- 13,544
- 43,537
Kikubwa scene za Rachel & G sitadanganyaIli unilishe matango pori😀😀
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kikubwa scene za Rachel & G sitadanganyaIli unilishe matango pori😀😀
Yaan anasifia uharamia. Angeanza kuna tatzo limetokea nahisi kuna jambo haliko sawa kwa racheli na mwenzake pat afu ndio aanze. Sema mwamba nae hakumoanga babake mapema ili waende na script imekamilikaHuyo baba yako mdogo jau gambe limemkolea hafati script inavyotaka anajitungia mwenyewe eti “Kijana wetu naona ameamua kuunganisha undugu” 😹😹😹
Hawa wajinga walipita bar kwanza ndo wakaenda hukoYaan anasifia uharamia. Angeanza kuna tatzo limetokea nahisi kuna jambo haliko sawa kwa racheli na mwenzake pat afu ndio aanze. Sema mwamba nae hakumoanga babake mapema ili waende na script imekamilika
Mkuu unachoandika sio jambo geni kwenye jamii zetu dada kamkataa mtu wake mdgo mtu kachukua uskukan yapo sisi wabantu au unatwanga wote hata zaidi ya 2 wa familia mojaVyovyote watakavyoona tu mi sipo kumfurahisha mtu hapa, naamini kuna watu wanaweza kujifunza kitu Kwa niliyopitia mimi
Hapo waliznguaHawa wajinga walipita bar kwanza ndo wakaenda huko
Ashukuru alikunywa balimi, angejichanganya kunywa pingu au chipapa ba mdogo angeomba naye akazie undugu kwa mama mkwe ili walee wajukuu 😹Yaan anasifia uharamia. Angeanza kuna tatzo limetokea nahisi kuna jambo haliko sawa kwa racheli na mwenzake pat afu ndio aanze. Sema mwamba nae hakumoanga babake mapema ili waende na script imekamilika
Jamaa mpaka Leo ni msanii msanii tu anajiita " Mzee wa kazi chafu" 😀Ba mdogooooooooo 😂😂😂😂😂
Bila picha ya ba mdogo huu Uzi ni batili mana ametisha sana.
Hahaha na huo ukaribu bamdogo anaweza mtaka mama rachelAshukuru alikunywa balimi, angejichanganya kunywa pingu au chipapa ba mdogo angeomba naye akazie undugu kwa mama mkwe ili walee wajukuu 😹
🤣🤣🤣🤣🤣Hawa wazee wanasema siku ya tambiko lazima tuwepo hasahasa wewe, tuwe makini Mzee Hawa watu huku ni wajinga Sana tunaweza kwenda kichwa kichwa tukaishia kuchapwa viboko na uzee huu"
Si ndo mambo Yako unayopenda hayo 😀Kikubwa scene za Rachel & G sitadanganya
Kesho kabla sijamaliza siku zangu za holiday ntakua na ba mdogo, sema yeye sio mtu mtandaoni, Ntampa salamu za Wana jfStory nzuri sana aisee
Mpe salamu nyingi tumempenda sanaKesho kabla sijamaliza siku zangu za holiday ntakua na ba mdogo, sema yeye sio mtu mtandaoni, Ntampa salamu za Wana jf
Ila Baba mdogo ni Comedian kabisaS3 epi 13
Sasa mimi nakuaga na maamuzi yangu nikashafanya hata iweje siwezi kubadili, nikapiga mahesabu story za Kanda hizo kweli nazijua, katika kukaa mwanza Kuna msiba ulitokea wa rafiki yangu alifiwa kwao nikamsindikiza, Ile kufika center akukutana na wajomba zake pale tukaanza kupiga bia kwanza kabla hatujafika msibani, mmoja wao akazidiwa akashindwa kwenda kuzika, kesho wamekaa kikao mjomba anaambiwa lala chini apigwe viboko mjomba kagoma hapo na watoto wake wapo kabisa, badae wakatumwa vijana waende bomani kwake wachukue ngombe watatu kama faini, Mzee kuskia ivo akashuka tu chini wakamlamba viboko, hivyo kwanza nikasema hata mbingu ishuke swala la mimi kwenda kwenye Hilo tambiko siwezi kujaribu, Hawa watu swala la viboko hua ni la kufikia tu
Muda ukaenda Sasa mawazo yamehamia Kwa G, najiuliza huyu mtu yupo wapi? Hapo imefika usiku ulizia naambiwa hajaja, kazini najua hakufika maana yule dada bosi wake alinitumia sms " naona huyu Binti ni kama hataki kazi, na Leo hajaja".... Nikawaza pale nifanye nini Sina Cha kufanya, nikiwaza misala inayonisubiri mwanza nachoka kabisa
Sasa Kuna muda naona namba mpya inapiga, kabla sijapokea nawaza hapa inawezekana ni G huyu, au ukute mama mkwe au Rachel maana hao wapo blacklisted, au ni mtu mwingine tu, nikaona ngoja nipokee, nikawa naskilizia sauti kwanza mbinu za kibaharia, nikaja kujua ni Rachel... Nikakata simu
Nakaa kidogo zikaanza mvua za sms Sasa.... Lawama kama zote, mara nataka kumuua mama Yao, yaani maneno kama yote naonekana mimi ndo Malaya Dunia nzima, ila Sasa paliponichosa zaidi akaniambia kuanzia Leo hesabu huna mtoto tena na mimi, D naondoka nae na hutokaa uje umuone tena labda nikiwa nimekufa, ukitaka hata mahakamani tutaenda..... Nikasema mbona hili balaa Sasa, hapo nikapigwa na biti akaniambia " yaani we dawa Yako Iko jikoni ni swala la muda tu utanitambua vizuri"
.
Nikawaza sasa huku nafanya nini, mbona kule mambo ndo yanazidi kuharibika, G nae yupo wapi? Nawaza mtoto kweli akiondoka huyu Rachel naanza kumtafutia wapi, nikakata shauri hapa inabidi nirudi mwanza tu nikapambane na hizi ishu maana kukimbia sio suluhisho kabisa
Nikatoka zangu pale Kuna bar nikaenda piga piga gambe pale, narudi Nina mawazo Sana... Navuta hisia za nyuma naona kama nimeharibu maisha yangu mwenyewe, sijui nikapata hisia gani bana, nikachukua Simu nampigia Mary mara upande wa pili inapokelewa naskia sauti ya kiume, naambiwa huyu kapumzika mpigie kesho!!! Basi tu Kuna ka roho flani ivi kakaingia nikajiskia vibaya nikasema maisha ndo hivo lazima yaendelee
Kesho yake napiga plan jinsi ya kumuaga mama Sasa, nikaita fundi pale nikapiga nae hesabu arudishie rangi ukuta wa fence ulianza kupauka nikampa Hela za material pale, hua tuna utaratibu Kila tukirudi nyumbani na sister ni kujaribu kurekebisha chochote pale nyumbani, badae mama namuaga namwambia kesho narudi mwanza.... Akaanza kucheka, namuuliza unacheka nini we Mzee, ananiambia " hivi Kwa akili zako ulitegemea flani(ba mdogo Sasa) ndo ataenda kurekebisha ujinga uliofanya? Naona umeamua kwenda mwenyewe"
Hapo kumbuka simuambii chochote kinachoendelea, nikampotezea tu, badae akaniita akanipa zawadi za mjukuu wake tukakaa Sasa akaanza kunipa ushauri, kaniambia kua makini Sana mwanangu huko upo ugenini watu wanaweza kukufanyia Hila usichukulie mambo kirahisi nikamwambia sawa....
Kesho mimi huyo safarini narudi mwanza, njiani kuulizia si kazini Wala nyumbani G haonekani, nikasema nikifika ntajua.... Nikafika salama Sasa hapo tupo na ba mdogo tukaanza kupanga mbinu pamoja, jioni tunatoka nampeleka mahali anakataa ananiambia twende sehemu flani ndo Kuna watoto kule, nikamuambia naona ushakua mwenyeji, wewe ndo maana kazi ilikushinda unawaza watoto tu....
Sasa nafika mwanza G nae kimya tu sijui hata yupo wapi, ila nikawa najipa moyo huyu kwao watakua wanajua yupo wapi la sivyo wangenisumbua Sana.....
Wale wazee wakaja kumpigia ba mdogo hesabu pale tukakamuliwa pesa sijui ndo na Hilo tambiko, hapo namwambia ba mdogo we tutoe tu tutaona mwisho wake ni nini, akasema sawa tukapanga siku wakaja kuzichukua, Sasa kama bahati yule dada wa kazi wa mtoto nae sio mjinga alishakuja kujua nini kinaendelea pale, akaja akapata taarifa Kwa kuskia skia kumbe G alienda Kwa shangazi yake mmoja akawa amekaa huko, nikasema afadhali Sasa najua mtu yupo salama na nini
Hapo karata iliyobaki tuwasubiri hao wazee wafanye Hilo tambiko lao, wakae Sasa na mama mkwe kifamilia wao ndo watatupa jibu nini Sasa kifanyike pakawa hakuna ujanja zaidi ya kusubiri, hapo na mimi siku zinaenda nawaza hii ishu inatakiwa iishe kabla likizo haijakata...
Hapo siwezi hata kwenda kumuona mtoto yaani ni vurugu mechi tu
Zikapita kama siku 2 nipo na ba mdogo home mara G huyo kaja na mama Fulani nilikua simjui, tukawakaribisha pale ndo akajitambulisha kua ni shangazi yake( upande wa baba Sasa).... Yaani mama mkwe wanaitana wifi, Sasa tumeongea pale mimi nipo kimya hapo baba mdogo nae anajikuta ana busara muda wote yeye ndo anaongea pale wanamskiliza, Sasa sijui ndo ma wifi hawapatani au yule shangazi ni kama alikua mtulivu Sana, anamwambia ba mdogo Hawa ni watoto wetu haya yashatokea Sasa tufanyaje, ni kwenda nayo tu hivo hivo, nikasema afadhali Sasa hata na huyu
Siku ya kufa nyani Sasa.....
Tumekaa pale geti linagongwa, ba mdogo alikua karibu na mlango wa kutokea mara kainuka kaenda kufungua, badae sijui ni kama nilipatwa na wazo gani nikasogeza pazia nijue ni nani anagonga, geti kufunguliwa namuona Rachel na yule rafiki yake wa mgahawa, ba mdogo akasalimiana nao pale sijui aliwaambia nini yeye akawa anakuja wao wamebaki tu pale karibu na geti ila washaingia, jamaa kuingia ndani hakujali hata kama tuna wageni ni kama alipata wenge ivi ananiambia "mzee mwaka huu wa kwetu"
Kila mtu anapenda sema mwingine yupo huru kueleza mwingine kama ndo Ile kimya kimya, eb fikiria maisha bila hayo maniaje😁Si ndo mambo Yako unayopenda hayo 😀
Umenikumbusha story ya dj ally b anasema akilewa anajionaga mtu flani Mkubwa,Ashukuru alikunywa balimi, angejichanganya kunywa pingu au chipapa ba mdogo angeomba naye akazie undugu kwa mama mkwe ili walee wajukuu 😹
Shusha epsod ingine au mpaka kesho mkuu.Kesho kabla sijamaliza siku zangu za holiday ntakua na ba mdogo, sema yeye sio mtu mtandaoni, Ntampa salamu za Wana jf