Ushawahi kujichanganya kimapenzi mpaka ukawa unawaza hapo nyuma ulikosea wapi?

Wazee wa kukodi kwa Majadiliano [emoji23]
 
Kazi ipo
 
S2 episode 4


Basi bana tukakaribishwa na wale wazee wakaanza kujitambulisha mwingine mjomba mwingine sijui nani basi tu balaa tupu, hapo ba mdogo na yule mshenga nao hawaelewi niliwaambia tutawakuta tu Rachel na mama yake kazi itakua nyepesi...


Yule mzee mshenga akajieleza weee, kua kijana wetu amefanya uharibifu hapa bomani kwenu tumekuja kujisalimisha na kama mila zinazosema tulipie fidia/faini kwanza alafu tujipange siku nyingine tuje kwa ajili ya mahari sasa maana hatuwezi kujadili yote kwa pamoja


Kuna mzee mmoja akisimama kwa hasira akasema " nyie mnaongea nini?, Yaani mshamuharibu binti yetu alafu mnaongelea mambo ya faini kwanza tena, hapa tunamaliza mpaka na mahari kama hamtaki msitupotezee muda hapa msilete utoto wenu hapa"
Mzee mwingine nae akawa anatishia kuondoka kama hatutajadili na mahari kabisa, yaani kiufupi wale wazee walikua wakali wakatutreat kama watoto kabisa hakuna ustaarabu wala nini, nikaanza kuwaza Patrick mimi nimeingia kuna balaa gani mbona hawa watu hatuwezi hata kukaa tukaongea vizuri tu wanafoka kila mda



Uzuri yule mzee mshenga alikua mstaarabu sana wala hakupanic akazidi kuwaelewesha tu ila hawataki kuelewa, mwisho akaomba sisi wageni tutoke tujadiliane nje kwanza, tukatoka sisi watatu, yule mzee mshenga akaanza

"kijana wangu, kama unavyoona hii ngoma ishakua ngumu sasa tunafanyaje?

Kabla sijamjibu ba mdogo akadakia

"Hawa wasituone sisi wajinga, hatuwezi kubadili lengo la kuja huku wasipokua makini tutaondoka zetu tuwaache hapa"

Na mi hapo nishachukia tu sana nipo kimya tu, yule mzee mshenga ndo akawa anatutuliza, nikapata wazo nikampigia Rachel mara ya kwanza hakupokea, mara ya pili ndo akapokea

Nikamuuliza upo wapi mbona hata sikuoni na bado mmebadilisha utaratibu wote

Rachel: " mi npo huku ndani kwa jirani tumeambiwa tusitoke mpaka kikao kiishe, nisamehe mme wangu hata mi sikujua wangepanga hivi'

Mimi: " sasa mi siwaelewi wazee wako hawataki tuongee mi naondoka zangu zawadi za mama tumeziacha ndani huko"

Rachel: " usifanye hivo jamani, kwanini unataka kunitia ai.. "


Kabla hajamaliza nikakata simu, ba mdogo nae mi mzee mmoja mishen town mjanja mjanja sana akamwambia yule mshenga twende wakigoma maongezi tuwaambie tutakuja siku nyingine tuondoke zetu


Tukarudi ndani bado wale wazee hawataki maongezi ya faini wao ni vyote kwa pamoja na mahari, yule mshenga akaomba radhi akaomba tukajipange tuje siku nyingine, ni kama machale yaliwacheza wakajua hawa tunaweza tusiwaone tena wakajifanya kuzuga pale kua tuongee kuhusu faini kwanza alafu mahari ije iongelewe na iletwe kabla ya mtoto hajazaliwa


Basi wakaanza sasa faini, zawadi sijui za mama,babu makokoro mengine na ngombe 6😀, dah pale yule mshenga akaguna akasema ni faini wazee wangu au mahari kabisa, wakasema hio ni faini tu na hapo tumewaonea huruma maana mmekuja wenyewe, basi wakaanza kubishana pale mpaka wakaishia ngombe wanne kila ngombe waka mu valuate kwa laki 3 ikawa milioni laki 2, ukiweka na yale makorokoro ikaja kama milioni laki 6, hapo mi nina hasira nataka tu tumalize tuondoke, nilikua na kama milion laki 3 nikawapa tukasema hio laki 3 iletwe baada ya wiki moja, dah hio laki 3 wakatuandikisha maelezo kabisa na kusign nikapata hasira namuambia mshenga au niende watolea akawa ananiambia acha tu hakuna shaka


Baada ya wao kuvuta mpunga sasa ndo kidogo naona wakaanza kutuchangamkia sasa, kina Rachel na mama yake ndo wakaja wakaleta chakula kinywaji pale tukajumuika tukaaga tukaondoka, stop ya kwanza atm nikatoa pesa kidogo maana nilishapukutishwa kule tukapita bar kula kinywaji kwanza, yule mshenga akaniambia kijana hawa wazee sidhani kama kwenye mahari tutafika muafaka
 
Kazi ilikwepo hapa asee
 
S2 episode 5


Hilo sakata likaisha bana, Rachel jioni karudi namuuliza hao wazee ni kina nani, ye anacheka tu anasema sijui hata mama kawatoa wapi, dah moyoni nikawa nasema tu mbona hawa watu kama hawapo serious nikaanza kujuta sasa naona mbona kama nakosea, hapo mama sijamuambia anaishia kuskia tu maneno juu juu kwa watu


Baada ya kama siku 2 hivi, Rachel kuna simu yake ya zamani ilikua samsung sijui toleo gani ila zile za nyuma kidogo akawa kaniomba nimbadilishie kioo kilikua kimevunjika ili aje ampe mdogo wake wa kike yule alikua yupo form 2, sasa nikaja kutoka nayo siku naenda kazini nikaacha kwa fundi jioni nikaipitia, katika kukagua kioo kama kipo sawa nikawa nimeingia sasa kwenye simu haikua na password wala nini dah huko sasa ndo nilikutana na balaa ambalo siwezi lisahau



Nikaingia kwenye sms za kawaida aisee nilichoka, zilikua na span ya kama mwaka, ni kama sms za mwaka mzima hajikufutwa, huko nilikutana na sms za wapenzi kama wote yani, madereva wa malori, wame za watu, ma dj wa club, wafanyabiashara, vijana wa mtaani tu yaani vurugu tupu, nikapanic sana nikapita mahali nikaanza ichunguza simu taratibu, sms zile ambazo zilikua wazi kabisa kwamba ametembea nao maana unakuta wanakumbushiana kabisa waliyofanya zilikua za wanaume kama 8 ivi



Kuna kama watu 6 hizi hazina ushahidi wa moja kwa moja kama walifanya au, hapo ni sms za kawaida, nikazama whatsapp sasa... Uwiiii.... Huyu binti ni malaya sijapata kuona huko napo watu washamla sana, unakuta sms anaelekezwa njoo guest flani, mara namtuma boda akufate alafu watu tofauti, kuna moja jamaa anamuambia nakufata unipe binti anadai siwezi tumejuana leo tu mara subiri nikuandalie siku nyingine ili nikupe vizuri, jamaa akakomaa demu badae akamwabia haya nifate, ni hio namba haijaseviwa hata😔, hapo na mimi binti nishaanza kumpenda nilijikuta natetemeka tu sijawahi kuumia vile


Nikaja gallery sasa, kuna video mbaba mtu mzima wapo chumbani anampiga romance huku anamnywesha savannah, yaani kwenye hio simu nikisema nieleze mambo yote niliokuta naweza andika mpaka nikachoka maana ni mengi mno hayaelezeki,


Kuna chat nikakuta anachat na yule dada wa mgahawa yaani hapo ndo kila akienda kuliwa ndo hua anamuambia shoga yake, mpaka kuna siku yule dada wa mgahawa akamwambia "shoga yangu na we sasa punguza umalaya"
 
Du pole sana boss sio poa
 
recho ni kama Elineva tu, pumbavu sana elineva
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…