S3 epi 19
Tukatoka pale nikapata muda kidogo wa kukaa na mwanangu pale, badae tukaaga tukawa tumeondoka, hapo ba mdogo ananiuliza wale wazee mmeishia wapi, hapo mi hata sikutaka kumjibu, akawa ananiambia wale ungeniachia mimi ndo kiboko Yao, nikawa namshangaa tu Sasa maana ye aliwakimbia akaniachia mimi msala.....
Muda unaenda likizo ikafa, nikaanza kwenda kazini kama kawaida, haikupita muda Sana nikaja kupata mkopo kazini, nikamalizia kibanda changu kule Kuna mtu akawa anakaa sikuhamia Bado, sister akanishauri nifungue mini supermarket, nikawa nawaza makorokoro yote Yale siku ya kupiga hesabu si ntakua mwehu mimi nikaachana na Hilo wazo, nikatafuta mahali nikafungua duka la kuuza electronics na accessories zake maana hivi vitu tangia chuo nilishafanya Sana hizi biashara, nikajichanganya mbele nikaweka kibanda Cha miamala ya Simu.... Hii ilikufa mapema tu kuna kipindi huyu dada niliyemueka walikuja wakamtapeli zaidi ya million 2, nikawaza na hizi commission hazifiki hata milioni hapa ntakua nafanyia kazi wajanja nikaachana na hio biashara, G hapo Bado yupo Kwa shangazi yake Wala sikutaka kupeleka mambo Kwa papara, ba mdogo Bado nipo nae town tu.....
Ikaenda mpaka siku Sasa tukahama pale tukahamia nilipojenga Sasa, nikanunua vitu vya ndani ambavyo havipo mpaka kiasi pakaonekana ni nyumba Sasa, kuratibu mawasiliano pale nakumbuka siku wanamleta G Sasa pale alikuja na shangazi yake, yule mama mwenye nyumba kule kwao, mtoto wangu na dada wake wa kazi, mama mkwe alikataa kuja, yule mama mwingine akawa tu ananiambia usijali mwanangu Bado huyu mama hajakaa sawa ila mtakaa sawa tu Wala usiwe na mawazo
Hio siku kwakweli ni kama nikaanza Sasa kupata amani, hatimae naanza kuishi na mwanangu, G nae huyu hapa, nikiangalia hata kama Bado Kuna vinyongo ila Kwa mama yake na wale wazee wake Kwa upande wangu naona nimeshamalizana nao, basi tukala pale ikawa kama kasherehe flani pale
Yule mama na shangazi yake G badae wakampa pale ushauri, wakawa wanamwambia usijione mdogo ndo Sasa ushakua na mji Sasa hivi...badae nikatoka nikawaacha wanashauriana pale sijui waliishia wapi badae wageni wakaaga wakaondoka
Tumebaki Sasa wenyewe, ba mdogo hapo hio siku ana Raha yeye anapiga zake mitungi tu mimi npo kimya ila moyoni Nina amani Kwa kiasi chake, ba mdogo nae sijui ndo kulewa akaanza kujisifu pale mbele ya G, " mimi sijawahi kushindwa jambo, umeona Sasa hili jambo jinsi lilivyokuja kuisha kitaalam" hapo namcheki tu G anacheka zake tu.....
Basi tumekaa pale mpaka muda wa kulala, ba mdogo tumemuacha, dada alikua kashalala, sisi hao na mtoto mpaka chumbani, G anafika kanilalia anacheka tu namuuliza vipi na wewe, akaanza yani tulianza kama matani tu Leo siamini tumefikia hapa..... Nikawa namwambia ndo utulie Sasa ukiniletea ujinga narudi kwenu natafuta mdogo wako hata Kwa ndugu zako naoa huko siwezi kutoa mahari mara mbilimbili kwanza kwenu wamenisumbua Sana, akawa anacheka tu
Kuna kulala Sasa hio siku? Sex kiasi maana tulikua na muda Sana na muda mwingi ni kama tulikesha tu tunaongea mipango ya hapa na pale na Sana Sana kukumbushiana mabalaa yetu, haipiti muda atanitania " kaka unakumbuka ulinibaka?".....
Fast forward.....
Ba mdogo akaja kuondoka, Huku G nae tumbo linazidi kukua tu, maisha yashakua ya amani Sana, tofauti na Rachel G alikua na heshima flani Sana kwangu, zile heshima za kuniheshimu kama kaka kuanzia kipindi kile hazikuwahi kumtoka, mambo yanaenda vizuri tu Sana japokua mama mkwe hakuwahi kuja pale ila tulikua tunaenda kumsalimia na kwenye Simu pia sio kama zamani ila mawasiliano yapo...
Muda ukaenda Sasa G anakaribia kujifungua, mama yangu mzazi mada za G ni kama alikua anazikwepa Sana ikafika muda nikawa nimemsoma na mimi nikaacha kumwambia mambo yake, Sasa Kila kitu hapo tunaona kinaenda sawa, balaa likaja kutokea, Rachel kule sijui alitibua nini, akarudi rasmi mwanza, yule rafiki yake mwenye mgahawa hapo nae kashavutwa sogea tukae na mshkaji mmoja, ikabidi afikie Kwa mama yake, kumbuka hapa mama yake Bado wamepanga pale hajahamia kwake.....
Sasa huyu Binti(Rachel) kumbe kichwa chake kina wadudu, nilikua simjui vizuri