Ushawahi kujichanganya kimapenzi mpaka ukawa unawaza hapo nyuma ulikosea wapi?

Ushawahi kujichanganya kimapenzi mpaka ukawa unawaza hapo nyuma ulikosea wapi?

S2 episode 12


baada ya training kuisha nikarudi, nakumbuka kipindi hicho pesa ilikuepo si haba maana tulijibana na posho tulipewa nyingi ukizingatia maisha yetu ya kibongo, basi nakumbuka nikarudi nikaenda wasalimia na kupeleka zawadi nikaondoka zangu, Rachel akaanza nitafuta mme wangu nakuja tulee mtoto wetu na blah blah kibao nikamwambia we nipe muda ntakuambia, ikapita muda mi kimya tu naenda kuona mtoto naondoka zangu, hapo kuna muda simkuti maana mtoto alishaacha na kunyonya



katika hela nilizobakiwa nazo nikaenda site nikamwaga tofali za kutosha nikaanza kuinua boma taratibu, sasa kuna kipindi Rachel akawa anauliza vipi kuhusu zile m3 nilizokuomba za mtaji mi nikwambia kwa sasa sina pesa nina ujenzi, basi sijui ni hasira au kesho yake akaniambia " kuna mtu kanitafutia kazi geita najiandaa kuondoka na mwanangu"



nikawa nawaza huyu mwanamke mbona kila siku ana jambo tu, lengo lake nipate stress tu au nini, nikampigia namuuliza sawa umepata kazi huko ukienda na mtoto na maisha hata hujaanza huko mtaishi vipi na wapi? akajibu " tutaishi tu mbona mi nilikua bila baba"


basi nikaona huyu mtu ni kama anataka ligi, jioni nikaenda kwao nikamkuta yupo na mama mkwe na grace, yule mdogo wao mdogo wa mwisho wa kiume kuna kipindi baba yake mzazi alikuja kumchukua, basi baada ya salamu na nini mama mkwe nikamueleza kila kitu tukawa kama tupo kikao, nikawaambia mwanangu haendi popote kama wamemchoka nimchukue nimpeleke kwetu maana na kunyonya kashaacha, uzuri huyu mama mkwe nachompenda hakua kabisa upande wa binti yake kwenye mambo ya kipuuzi, mama mkwe akawa mkali sana akasema mtoto haondoki mahali akawa anamwambia mtoto wake kama umepata bwana huko we ondoka ila mjukuu wangu haendi popote, baadae huyu mama akaanza kulia anamuuliza rachel umesahau maisha tulioishi kwanini unajitafutia matatizo bure ni nini ambacho hupati



hapo na mi nina hasira nikamwambia yule mama mtoto wangu nafanya mpango wa kuja mchukue na kuanzia leo mi najitoa ule utambulisho hebu ufate siku huyu akileta mwanamme mwingine we mpokee tu na mahari chukua, mi nikaondoka zangu


kweli bana ikapita muda Rachel akaja kuondoka akaenda geita nilikuja kujua baada ya muda kua alipata mwanamme alikua ana maduara mgodini huko ndo alimtoa huku ila uzuri mtoto alimuacha kwao, Mungu nae ni mpaji mi nikabadilishwa kitengo nikaenda kitengo kingine tulikua tunapata pesa sana nyumba yangu inazidi kukimbia tu moyoni nina amani, kuhusu swala la mahusiano sikua na mahusiano rasmi tena ikawa ndo hivo tena tunatoka kazini tupo na co workers tunaenda viwanja tu, wadada wa kujiliwaza hapa na pale walikuwepo wengi tu hasa hasa wanafunzi wa saut pale



mawasiliano na rachel yatakataa rasmi, nikawa namuambia mama mkwe sasa nitafute mfanyakazi nianze tu kukaa na mwanangu, akawa anagoma ananiambia italeta picha mbaya ukizingatia upo mwenyewe hapo, kumbuka hapa huyu mama kashakua kama mama yangu mzazi haishi kunipigia simu, kila siku ananiambia mwanangu Mungu atakusaidia tu mtoto atakua


Grace nae akamaliza form 4 ndo ikawa muda wote yupo na mtoto maana mama mkwe alipata kibarua mahali, kwa hio muda mwingi ikawa ndo mtu ninayewasiliana nae sana kujua mahitaji na hali ya mtoto na nini japokua karibu kila baada ya siku 2 nilikua naenda kuwaona


sasa kuna kipindi mama mkwe akaanzisha utaratibu, siku za weekend anamtuma huyu Grace wanakuja kushinda huku kwangu ili nipate muda wa kukaa na mtoto, Grace nae atafanya usafi huku, kufua nguo , kupanga vitu na kupika n.k, ye akitoka kazini ndo hua anawapitia wanaenda nyumbani, ikafika mahali wakazoea nawaachia tu funguo hata siku npo kazini watakuja kukaa kwangu badae mama mkwe atawapitia waondoke



nakuja na season 3 sasa ambayo ndo itakua mwisho huku ndo kuna balaa zito, stay
S2 episode 12


baada ya training kuisha nikarudi, nakumbuka kipindi hicho pesa ilikuepo si haba maana tulijibana na posho tulipewa nyingi ukizingatia maisha yetu ya kibongo, basi nakumbuka nikarudi nikaenda wasalimia na kupeleka zawadi nikaondoka zangu, Rachel akaanza nitafuta mme wangu nakuja tulee mtoto wetu na blah blah kibao nikamwambia we nipe muda ntakuambia, ikapita muda mi kimya tu naenda kuona mtoto naondoka zangu, hapo kuna muda simkuti maana mtoto alishaacha na kunyonya



katika hela nilizobakiwa nazo nikaenda site nikamwaga tofali za kutosha nikaanza kuinua boma taratibu, sasa kuna kipindi Rachel akawa anauliza vipi kuhusu zile m3 nilizokuomba za mtaji mi nikwambia kwa sasa sina pesa nina ujenzi, basi sijui ni hasira au kesho yake akaniambia " kuna mtu kanitafutia kazi geita najiandaa kuondoka na mwanangu"



nikawa nawaza huyu mwanamke mbona kila siku ana jambo tu, lengo lake nipate stress tu au nini, nikampigia namuuliza sawa umepata kazi huko ukienda na mtoto na maisha hata hujaanza huko mtaishi vipi na wapi? akajibu " tutaishi tu mbona mi nilikua bila baba"


basi nikaona huyu mtu ni kama anataka ligi, jioni nikaenda kwao nikamkuta yupo na mama mkwe na grace, yule mdogo wao mdogo wa mwisho wa kiume kuna kipindi baba yake mzazi alikuja kumchukua, basi baada ya salamu na nini mama mkwe nikamueleza kila kitu tukawa kama tupo kikao, nikawaambia mwanangu haendi popote kama wamemchoka nimchukue nimpeleke kwetu maana na kunyonya kashaacha, uzuri huyu mama mkwe nachompenda hakua kabisa upande wa binti yake kwenye mambo ya kipuuzi, mama mkwe akawa mkali sana akasema mtoto haondoki mahali akawa anamwambia mtoto wake kama umepata bwana huko we ondoka ila mjukuu wangu haendi popote, baadae huyu mama akaanza kulia anamuuliza rachel umesahau maisha tulioishi kwanini unajitafutia matatizo bure ni nini ambacho hupati



hapo na mi nina hasira nikamwambia yule mama mtoto wangu nafanya mpango wa kuja mchukue na kuanzia leo mi najitoa ule utambulisho hebu ufate siku huyu akileta mwanamme mwingine we mpokee tu na mahari chukua, mi nikaondoka zangu


kweli bana ikapita muda Rachel akaja kuondoka akaenda geita nilikuja kujua baada ya muda kua alipata mwanamme alikua ana maduara mgodini huko ndo alimtoa huku ila uzuri mtoto alimuacha kwao, Mungu nae ni mpaji mi nikabadilishwa kitengo nikaenda kitengo kingine tulikua tunapata pesa sana nyumba yangu inazidi kukimbia tu moyoni nina amani, kuhusu swala la mahusiano sikua na mahusiano rasmi tena ikawa ndo hivo tena tunatoka kazini tupo na co workers tunaenda viwanja tu, wadada wa kujiliwaza hapa na pale walikuwepo wengi tu hasa hasa wanafunzi wa saut pale



mawasiliano na rachel yatakataa rasmi, nikawa namuambia mama mkwe sasa nitafute mfanyakazi nianze tu kukaa na mwanangu, akawa anagoma ananiambia italeta picha mbaya ukizingatia upo mwenyewe hapo, kumbuka hapa huyu mama kashakua kama mama yangu mzazi haishi kunipigia simu, kila siku ananiambia mwanangu Mungu atakusaidia tu mtoto atakua


Grace nae akamaliza form 4 ndo ikawa muda wote yupo na mtoto maana mama mkwe alipata kibarua mahali, kwa hio muda mwingi ikawa ndo mtu ninayewasiliana nae sana kujua mahitaji na hali ya mtoto na nini japokua karibu kila baada ya siku 2 nilikua naenda kuwaona


sasa kuna kipindi mama mkwe akaanzisha utaratibu, siku za weekend anamtuma huyu Grace wanakuja kushinda huku kwangu ili nipate muda wa kukaa na mtoto, Grace nae atafanya usafi huku, kufua nguo , kupanga vitu na kupika n.k, ye akitoka kazini ndo hua anawapitia wanaenda nyumbani, ikafika mahali wakazoea nawaachia tu funguo hata siku npo kazini watakuja kukaa kwangu badae mama mkwe atawapitia waondoke



nakuja na season 3 sasa ambayo ndo itakua mwisho huku ndo kuna balaa zito, stay tuned
Noma sana
 
disclaimer(tuanze tu s4 maana nimesahau hata kule nimeishia episode gani)

S4 epi 1




Katika kitu nilikuja sijui Sasa kumbe Rachel huku yaani ashakua na kinyongo Sana na mdogo wake, mimi hapo najifariji tu tu naona huyu ni mtu na mdogo wake hata kama wametofautiana ni mambo ya muda tu, hapo nawaza Hawa wameishi pamoja muda wote huo, waje wagombane tu kisa mimi, naona hapa hapana ni suala la muda tu mambo yatakaa sawa, I was wrong!!!



Sasa Rachel na yule dada wa mgahawa ni watu wamekaa sana pamoja, Kwa hio hata kwenye mambo ya kijinga inakua rahisi Sana mmoja kumshawishi mwenzake, Rachel kumbe muda wote huo alikua na mpango, mi nikawa navutwa tu sielewi chochote.....



Kuna kipindi Sasa Rachel kaniita tuongee, hapo mama mkwe mawasiliano na mimi yashakua hafifu Sana yaani ni mtu hatuongei kama zamani, huyu mama mkwe kule kwake akawa ndo anamalizia anafanya mipango ya kuhamia, Sasa hio siku Rachel kaniita tulikutana sehemu flani hapo nimetoka kazini nimeenda na jamaa yule niliyeenda nae polisi mara wa kwanza, jamaa hapo nae ananishangaa ananiuliza " huyu Sasa mna ishu gani nae? Usisahau na kituoni ashakulaza ujue" hapo mi najiamini tu Wala najua huyu(Rachel) hawezi hata kunizidi ujanja wacha nimsikize tu nione anasemaje...... Tumekaa hio siku Rachel kaja mpole kweli tu, tukaongea mambo mengi tu, ye anajikuta Sasa anajutia yote yaliotokea ananiambia " unaona Sasa mpaka Sasa sipo karibu na mdogo wangu(G) kisa mambo haya"



Hapo mi namsikiza tu, badae namwambia maisha lazima yaendelee haya yashatokea Wala huwezi rudisha muda nyuma ndo ishakua hivo tu, na mimi hapo Nina kama guilty flani inaniingia moyoni maana Kila nikikaa na G japo ataonesha yupo sawa ila nikawa nawaza kama mimi ndo nimemgombanisha na familia yake, maana kipindi hiko hata mama yake naona tu kabisa hawapo sawa....



Rachel Sasa pale ndo akawa anaongea mambo mengi tu kuhusu yaliotokea, nae anaonyesha kujuta ila Sasa sio kama anataka niwe nae tena hapo ananiambia anataka tu tuwe sawa wote Ili awe huru Sasa hata akitaka kwenda kumsalimia mtoto wake na mdogo wake Sasa(G).... Nikaanza Sasa kumuambia pale kua na ye anakosea, kama ye alishaamua kuanza maisha mapya tena na mwanaume wake kule geita iwaje tena anakuja huku Bado anakua na kinyongo na sisi, namwambia hata G huenda asingefanya haya yote kipindi tupo wote, labda alifanya haya yote akijua wewe(Rachel Sasa) ulishaenda kuolewa huko na usha move on na maisha Yako....




Yote Kwa yote katika hayo maongezi point yake kubwa ilikua kua mama yake anahamia kwake Sasa na yeye hataki kwenda kukaa na mama tena, anataka kuanza maisha yake mengine kabisa.... Hapo ananiambia Hana kinyongo tena na sisi na G anataka amani tu Kila mtu aendelee na maisha yake



Point kubwa Sasa, ye akawa anadai ana akiba zake anataka kwenda kupanga aanze maisha yake... Siku nikipata nafasi hata kama sio Kwa wakati huo nimuwezeshe na yeye afanye biashara zake, hapo ananiambia " ukweli utabaki pale pale, mi ndo mama yake na D, Leo na kesho hata kama ukiwa haupo hakuna atayekua na uchungu na D kama mimi, ukiniwezesha mimi hata kama sio Leo lakini unakua umewekeza Kwa mtoto wako tu, kwani mi naweza kumuona mtoto akiteseka na wakati mimi nipo? Na mi ndo mama yake?"




Nikawaza pale namuuliza Sasa unataka nini? Ananiambia niongezee tu pesa kidogo nianze kuishi kwangu alafu siku ukiwa na nafasi na nafsi Yako ikiona sawa unaweza niongezea mtaji kidogo na mimi nipambane na maisha huwezi Jua kesho nikawa msaada Kwa mtoto wetu



Nikamwambia acha niwaze ntakujibu, Ile siku hatukukaa Sana akawa ameondoka, nikamshirikisha mshkaji wangu Sasa tuliyeenda nae pale akawa kama ana wasiwasi anasita tu pale badae akaniambia " mwanangu Kwa uliyopitia yote haya, hakikisha tu humfichi mke wako(G Sasa) maana haya mambo hayaeleweki, unaweza kufanya kitu Kwa Nia njema badae kikakurudia wewe"



Tukaagana pale mi nikaondoka zangu, home na G maisha ni ya amani Sana analea tu watoto Wala hawezi wabagua maana hata D ndo kamzoea kama mama Sasa, kama unavyojua tamaduni zetu watoto wakiwa wadogo, tulikua tunalala wote chumba kimoja......



Sasa hapo mi sielewi kumbe Rachel ananivuta tu alikua mpango wake, zikakatika siku mama mkwe akahamia kwake(japokua hata hakuniambia) taarifa napata Kwa Rachel tu hapo, nikaja kumpa kiasi flani kidogo tu Sasa japo kumsupport ikafika muda na yeye akahama akaenda kupanga sehemu nyingine, ikafika mahali Sasa tukapanga kwenda kule ustawi tena tuwaambie kua tushaelewana tu mtoto atabaki kwangu, ila kabla ya hapo nilimpigia ba mdogo nikamshirikisha akanishauri kwanini msimshirikishe mwanasheria maana haya mambo ya kukubalia Kwa mdomo hayana guarantee itafika muda utageukwa tu



Rachel nikaja mwambia, hapo anajifanya kua yeye Hana shida niamue mimi tu, basi Kuna jamaa alikua lawyer wa kampuni pale( part time tu sio muajiriwa kamili) nikaja mtafuta siku tukakaa mahali nikamuelezea situation zangu zote akaniambia Hilo swala Halina shida, basi tukaweka pale makubaliano ya mtoto na Rachel kupitia huyo mwanasheria tukazipeleka ustawi pale, badae akazipitisha mahakamani tukawa Sasa na official agreement kuhusu mtoto, japokua vihela vilitoka kiasi ila nikawa Sasa Nina amani kua mambo Sasa yamekaa sawa....


Sasa katika hayo makubaliano nayeye aliomba awe anapata muda wa kumuona mtoto, wote hatukuona kama ni jambo baya maana ukizingatia na yote Bado yeye ndo mama yake



Muda ukaenda Sasa sijui Rachel akaanza kumuingia vipi mdogo wake(G) nashangaa wakaanza kuja pale home na yule rafiki yake wa mgahawa watakuja salimia pale, Rachel atamuona na mtoto wataondoka..... Kuna kipindi ntawakuta nyumbani nawaona wako sawa tu at least nikaanza kupata amani naona Sasa Bora hili jambo linaenda tu sawa....




Sasa sijui ikawaje hapo G nae akawa amejenga Sana ukaribu na yule rafiki yake Rachel wa mgahawa, hapo anamchukulia tu kama dada yake na nini atashauriwa mambo ya maisha,na hapo washarudisha ukaribu na Rachel kiasi utakuta Kuna muda wanapigiana Simu na nini, hapo mama mkwe yeye ataongea na G kwenye Simu tu muda mwingi si rahisi kumkuta kaja pale, na mi hapo mawasiliano ni kama yalianza kufa kabisa



Kuna kipindi Sasa mama yangu mzazi akaja mwanza, alikaa kama wiki mbili pale, Sasa damu za watu sijui zikoje, sijui ni upole na unyenyekevu wa G ikatokea tu mama wameelewana Sana na G, ukija home utawakuta wapo wote tu na watoto mara mama atamletea hiki na hiki, basi nikasema Sasa hapa maisha yashanyooka tu vizuri



Hapo Rachel na yule rafiki yake nao watakuja salimia siku moja Moja waondoke zao, Sasa siku mama kabla hajaondoka akaniita tukaongea mambo mengi Sana pale badae Kuna maneno nakumbuka aliongea Kwa hisia Sana akaniambia "mwanangu Sasa hapa naona ushaanzisha mji wako, mi siwezi kukuingilia ushakua mtu mzima wewe, Kaa na huyu Binti, makosa ya nyuma msiyawaze Sana hata huyu mwenzako(G) nishamueleza, ila sisi ni watu wazima Kuna mambo tunayajua nyinyi sio rahisi kuyaelewa Kwa Sasa, mshauri mwenzako awe makini Sana na Hawa(Rachel na rafiki yake Sasa), binadamu hua hatusahau Kwa haraka, unaweza kuona mtu anakuchekea kumbe moyo Bado mzito, mwambie mkamwana wangu awe makini Sana asiruhusu mazoea Sana na huyu dada yake na huyu rafiki yake"


Sasa hapo nikawa nawaza ni uoga tu wa mama maana naona hapo Kila kitu kipo sawa, basi tukaongea pale kabla hajaondoka Kuna siku mama akaenda kumsalimia mama mkwe kule kwake sijui waliongea nini ikafika siku mama akaondoka zake



Rachel akaja kufungua kiduka chake pale Kuna siku niliongea nae nikapita nikamsalimia ni nikaondoka zangu, Sasa hapo naanza kupata mawazo ntakuja nimuongezee ka mtaji kidogo maana nawaza Sasa Yale maneno kua Kuna kesho, yeye akiwa na msingi mzuri hata mwanangu atakuja kuishi tu maana binadamu maisha yetu tumepewa kama zawadi tu hakuna anayejua kesho.....



Ikafika kipindi Sasa Rachel atakuja mchukua mtoto wake pale siku haendi shule, nikitoka kazini ntampitia mtoto nirudi nae nyumbani.... MAKOSA!!!!!



Aisee mtu kama ulishatembea nae tena mmeishi wote kabisa ukitaka muachane Kwa amani kabisa Kaa nae mbali kabisa ... Hii kuonana onana na Rachel badae ikawa balaa tu yaani, Kuna kipindi utamkuta hayupo dukani na hapo ana mtoto itabidi umfate mtoto kwake Sasa, hapo utaambiwa subiri nimuandae, utapewa chakula na nini, yaani huo ukaribu Sasa.... Alafu Sasa huku nyumbani G Sasa Hana shida Kila kitu kinaenda sawa tu yaani Kuna kipindi ni kama wanaume hatupendi utulivu tunataka mikikimikiki tu yanii


Ukaribu Sasa na Rachel Kuna siku nakaa tu nawaza, kuna mambo ambayo mlikua mnafanya itafika mahali utakumbuka tu, akili ikawa inagoma ila mwili Sasa Kuna muda unawaza ujinga tu... Hapo nimesharelax sio kama kipindi kile ilikua Kila siku Kuna hili na lile


Sijui hata ilikuaje Kuna siku Rachel kanipigia mi hapo nimetoka kazini tumekaa tu mahali na washkaji wa kazini, nikamwambia nipo mahali flani akaja, tumekaa pale na pombe nazo hizi sijui hata nini kilinipata mara mimi hapo nipo tena Kwa Rachel alipopanga Sasa, hapo najikuta Sasa ndo nafanyiwa visa vyote, penzi la mtu anayetaka kukurudisha, ulikua usiku mrefu Sana yaani amri ya sita ikavunjwa, ..... Dah ndo nikawa Sasa nimerudi shimoni!!! Muda ya kama saa 10 nikaoga nikaondoka hapo naambiwa ulale tu Sasa, nimerudi home G hata kuuliza chochote hakuna, nikala, asubuhi kazini akili inawaza Sasa majanga yote niliyopitia, mwili nao unakataa unakumbuka mambo ya Jana hapo



Kakawa katabia Sasa, nikipata muda mi huyo Kwa Rachel( aisee maisha haya), hapo ndo utaongezewa utundu wote basi tu, Sasa kumbe bana mi hapo naingia kwenye mtego Wala hata sishtuki chochote, ndo maana nilisema Rachel alikua hatua Moja mbele yangu.....



Sasa yule rafiki yake Rachel wa mgahawa hapo ana ukaribu na G Sasa, Kuna siku kumbe alimfata akaongea nae Sana akawa anamuambia "ongea na mume wako Sasa maana naona wanakua na ukaribu na dada yako, hata kama ni swala la mtoto watu walishakuaga wapo wote huwezi Jua" wakaongea mambo mengi pale yeye anajifanya kama anamshauri kama mdogo wake



Ikafika siku G akaanza kuniambia Sasa mbona siku hizi upo karibu Sana na dada? Kua makini hata kama ni mambo ya mtoto huwezi Jua dada anawaza nini


Akili ikaanza kuclick Sasa hapo, nikamtuliza tu pale kua hakuna kitu akaelewa maisha yakaendelea, kumbe mpaka yule rafiki yake anaenda kwangu yote ilikua plan ya Rachel all along nilikuja kujua nishachelewa Sana.....



Sasa tukaja pata safari ya kikazi, nyumbani nishaaga, sema gari la kazini Kuna services dreva kaenda kufanya, sisi tunaondoka tupo hoteli Moja hapo tunapiga tu pombe pale tusubiri gari lije tuondoke, dreva badae anatuambia itabidi tuondoke jioni kabisa ndo itakua sawa, sisi hapo tunaendelea tu na mambo yetu pale... Akili ya kimwili nazo Sasa, nikamcheki Rachel, akaja.... Hatujakaa sawa tupo chumbani, Sasa Rachel nae sijui ndo alimpanga informer wake( yule rafiki yake wa mgahawa)....


Nakuja kutoka jioni tumeagana pale, tumepanda gari safari inaanza Sasa G huyo katuma sms " Mme wangu haya maisha utahangaika mpaka lini, yote uliyoyafanya Leo mbona nayajua"



tenaa????



nikampigia simu pale hapokei tu, tuma sms nauliza kwani kuna nini kimya.... basi tukasafiri tukafika mida ya kama saa 9 usiku, tukaenda mahali tukapumzika, piga sana simu hazipokelewi, piga simu ya mdada wa kazi nayo haipatkani



kesho mtindo ukawa ule ule, hapo Rachel nae hatutaftani, nikawaza nimtume mtu nyumbani au, ila kwasababu safari ilikua siku 2 tu nikasema ngoja



siku ya pili nayo ivoivo, badae nikamtumia G sms namuambia nishamaliza kazi kesho tunarudi kulikoni mbona hatuwasiliani mama


kimyaaa...



kesho yake sasa tupo njiani tunarudi mwanza , napata sms kutoka kwa mama yangu mzazi sasa ananiambia "mwanangu huko wameshakuchezea, sitaki kuja mwanza kubeba maiti ya mwanangu huko, kama pamekushinda tafuta kazi sehemu nyingine au urudi kwanza nyumbani"



nikazidi kuchanganyikiwa, nampigia mama simu nae hapokei, nikatuma sms " kuna nini kwani mama?" nae hajibu


nakuja fika mwanza nyumbani nakuta geti limefungwa gonga sana hamna kitu, piga simu mtindo ni ule ule mpaka nikajiridhisha hapa hakuna mtu



napata hofu na hasira pia sasa, badae nikamtumia G sms hapo nikawa mkali mbona simuelewi waache kunifanyia mambo ya kipuuzi.... kimyaaa....... nimekaa kidogo akajibu " funguo utazikuta hapo kwenye duka la flani baba D(jina la mwanangu wa kwanza)



hilo duka walikua wanaenda kununua mahitaji hapo lipo karibu, nikampigia G hapokei.... tuma sms kwani mpo wapi naona kimya tu....



nikatoka fasta mpaka hapo dukani, nakuta ana wateja ikabidi nisubiri kwanza watoke, kuja kuuliza sasa kulikoni ndo jamaa ananiambia funguo nimeachiwa kuna gari walipita nayo hapa imewabeba, naulizia nani na nani naambiwa wote, G watoto na dada yao...... aisee hapo sielewi jamaa namuuliza gari gani nae hajui hata aina akataja tu rangi na muonekano wake



piga simu sana kwa G hamna kitu hapokei, namuwaza nimpigie mama mkwe naona hapana hapo sijajua ni nini ntaharibu tu, nikatuma sms tena kwa G " sipendi upuuzi wanangu umewapeleka wapi, maana naona simu zangu hupokei"



nakaa kidogo napata ujumbe kutoka kwa mama yangu mzazi " sikutaka kujihusisha na mambo yako ila naona mwisho wake utakua mbaya sana,acha kumsumbua mtoto wa watu, ntakaa nae huku na wajukuu zangu mpaka siku ujinga wako utakapokuishia"
Kama ni story ya kweli wewe jamaa ni fala 😀😀😀😀😀
 
S4 epi 2



At least Sasa nikawa nimeshausoma mchezo mzima, Sasa sijui kwanini, badala ya kushtuka nikajikuta tu nimepata hasira Sana siku hio(ntalizungumzia huko mbele)..... Nikachukua zile funguo pale nikaondoka zangu maana hapo Sasa yule mtu wa dukani naona kabisa ashaanza kuniuliza maswali ya uchuro....



Nikafika nyumbani naona kama hapako kawaida, nishazoea kukuta watu na nini, nikaona tu pale nikatupia begi langu huyo nikatoka nikaondoka zangu..... Hapo move ni kama linaenda kimya kimya Rachel nae hajanitafuta Wala nini ila hapo mi nishamshtukia najua yeye ndo mastermind wa huu upuuzi wote....



Wakuambia Kuna mstari mwembamba Sana kati ya mapenzi na chuki, nikajikuta tu napata chuki flani Kwa Rachel tena, upande wa G Sasa Nakua na mixed emotions, unajua sisi wanaume unashajua mtu anakupenda 100% Hilo nalo ni tatizo, unakua unafamfanya kama mtu yeye Hana hisia, nikajikuta moyoni tu namlaumu G, kwanini aondoke bila kuniambia...... Basi tu nikawa na hasira pale.




Nini kilitokea?


Siku Kama nne zikapita hapo siwasiliana na Hawa wahusika wote(G,mama,mama mkwe, Rachel)..... Ndo nikaja Sasa kuanza kupata picha ya nini kilitokea Ile siku, kumbe yule rafiki yake na G Kwa kujifanya sijui anamuonea huruma ndo alimpenyezea G zile taarifa ya mimi kua na dada yake pale kabla sijaenda safari, G nae akamvaa dada yake kumuuliza huko napo akaambulia majibu ya dharau na kejeli.... Hili nilikuja kulijua Kuna siku G amenitumia screenshots za mawasiliano baina yake na dada yake na yule rafiki yake...... Hapo hatusemeshani mi hata sikumjibu.... Kuna sms Rachel akawa anamuambia Sasa mdogo wake " we ndo ulianzisha tabia ya kuiba vya watu, huyo sio wako nilikua nimekuazima tu" 😔😔



Nikawa at least nimejua nini kimetokea



Ikapita wiki, Hali ipo vile vile, Kuna siku nikampigia mama mzazi Sasa...



Mimi: mama shikamoo, vipi Hali Yako huko?


Mama: marhaba, unaendeleaje huko?


Mimi: nashukuru Mungu mama, vipi Sasa mlimtoa mtoto huku shule ndo itakuaje Sasa?


Mama: aliyekuambia huku hakuna shule ni nani?


Mimi: Sasa na huku ada nilishalipa mbona?



Mama: Kuna mtu amekupigia Simu akikuomba ada???


Dah, nikakata simu pale naona Sasa Hawa wamejipanga kivita ngoja na mimi niwaache tu, hapo sister akawa ananipigia nikaacha kupokea Simu zake, Rachel nae amepiga zake kimya ni kama alijua ashalipua bomu anasikilizia matokeo tu



Nikaanzisha tabia Sasa, tofauti na kazi nikawa sio mtu social kabisa.... Mpaka nahisi kama nimerogwa, nikitoka kazini ntarudi zangu tu home Moja Kwa Moja ntakaa zangu tu chumbani ntakunywa pombe pale, mpaka nipate usingizi kesho tena ratiba Ile Ile, nikishatoka kazini Simu nilikua naiset ukipiga Wala siskii, nikija kuingia kwenye calls Nakuta missed calls zote hapo nachagua wa kumpigia wengine nawapotezea....


Wazo hata la kumfata G Sina hapo, Nina hasira tu naona huyu nae kilichompeleka huko nini, mama nae Nina hasira nae kwanini anachukua familia yangu bila ridhaa yangu, Rachel ndo usiseme, kiufupi hapo najikuta karibu Kila mtu namchukia, nikawa na roho flani sitaki kukubali kua Nina makosa, nikawa ni mtu tu wa kumlaumu Kila mtu....





Muda ukaenda Sasa na wao wakaanza kunitafuta, ntapigiwa Simu na mama,G,sister,ba mdogo,Rachel mama yake Yaani Ile circle nzima hapo ni kama nimepata roho flani tu ya kishetani Wala siwezi pokea Simu zao hata siku moja, Wala kujibu sms, nakumbuka G akawa ananitega pokea basi ongea hata na mtoto mimi wapi kimya tu



Pombe nazo nikaona hazitoshi, nikaanza Sasa vilevi vingine, ntanunua stock kubwa ya pariki ndani, ntakua na tambuu za kutosha ndani..... Ikawa nawaza muda tu wa kutoka kazini ufike nawahi home hapo ndo naona kama ni sehemu ambapo akili yangu inakua Ina amani, ntakunywa pombe pale, ntatafuna hayo na tambuu ntakula pariki pale yaani napata amani ya moyo tu



Nikaanza kua addict Sasa wa hivi vitu, nikitumia naona nipo Dunia ya kwangu kabisa ambayo Haina kelele Wala nini, naskia amani kabisa ya moyo!!! Ujinga wa haya mavitu Sasa nikawa usingizi sipati, najiona tu nipo high muda mwingi naskia Raha.... Kuna kipindi sitalala kabisa asubuhi naamkia tu kazini, mpaka macho yakaanza kubadilika rangi.....



Weekend ndo naweza nisitoke hata ndani kabisa, na haya ma vitu yanaua appetite kabisa Wala Sina hamu ya kula, ikafika mahali weekend kuzima Simu kabisa naona ni kitu Cha kawaida tu, hapo nyumba inaanza kua chafu Sasa muda wa kufanya usafi Wala hata siwazi



Kuna jamaa yangu walikuaga wa kishua Sana nakumbuka kipindi tupo chuo Kuna pills flani jamaa alikua anatumia zipo kama drugs kabisa, nikaja kumcheki sijui ikawaje nikamtumia Hela akanitumia kikopo flani hivi, nikaanza kutumia na hivo vidonge,ukimeza kimoja aisee unahisi Dunia ni Mali Yako, dah nikawa sijui Nakua kama Teja Sasa



Nikaanza kutembea Sasa na zana zangu kwenye gari, tupo kazini nikiona stimu zinapingua ntaenda kwenye gari najitupia mzigo narudi kazini, aisee Ile kitu ikaanza kuniongezea confidence, nikawa mtu naongea karibu na Kila mtu yaani najiamini basi tu mpaka nahisi kazini wakawa kama wananishangaa....



Sasa hapo pombe nikinywa ni kama siskii chochote, ikafika mahali ni kama pombe niliacha tu naona hazina kitu, mirungi nilijaribu ikanishinda.... Mimi hapo ntakula zangu pariki, ntameza kidonge kimoja ntatulia naanza kutafuna tambuu pale..... Nikiskiza mziki yaani nahisi kama mimi ndo nimeimba hio nyimbo



Hapo sitaki kabisa mawasiliano na mtu ni kama nikawa nimejitenga kabisa na jamii, ndo maana unaona mateja wanaishi wao Kwa wao, wanahisi jamii haiwaelewi...... Yakawa ndo maisha yangu mapya mzigo ukikaribia kuisha ntatuma Hela jamaa dar atanitumia faster tu, hizi tambuu na pariki mzigo mpya ukifika lazima ntapigiwa maana nilikua nanunua mzigo mkubwa kama stock vile




Hapo G kashalalamika kwenye Simu mpaka basi, sms zinakua nyingi mpaka ye ndo anaanza kuniomba msamaha.. hapo hata wanangu mi siwawazi, nikawa mbinafsi Sana najiwazia mimi tu, Kuna siku mama mkwe Sasa aliwahi kunifata mpaka kazini nadhani mama ndo alimtuma nikamwambia nipo busy tu ntamtafuta, yaani hivo tu, nikaja kumpotezea..... Rachel nae Kuna kipindi akawa ananisumbua nikaja tu kumjibu siku tukikutana ama zako ama zangu




Majanga!!!


Nakumbuka Kuna siku jumapili hapo npo ndani tu kama kawaida, nimekunywa pombe kidogo Sana kipindi hicho hata siipendi kivile, nshajitupia mizigo yangu kama yote nipo stimu vibaya mno, Sasa hivi vitu tofauti na Bangi ni kua nikitumia Nakua active Sana, Kuna feeling flani ya Raha hivi tofauti na Bangi ambayo ni kama inakupooza(kusizi)..... Ghafla naanza kupata joto Kali Sana... Nikaingia bafuni nikajimwagia maji pale hapo sijavaa chochote nipo peku, Ile nitoke Sasa sijui nilikosea step vipi nikateleza nikaanguka, aisee sijui nini kilitokea nakuja zinduka ishakua usiku kichwa kizito hapo utasema nimebeba scania kichwani... Bado npo uchi aisee, nikajikongoja pale nikaenda kuvaa boxer nikawa nimekaa pale.... Hofu ikanitanda naona ningekuja kufa mimi Leo kifo Cha aibu namna hii, hapo nawaza sijilaumu mimi nawalaumu tu watu walionizunguka naona kama wao ndo wananifanyia makosa... Siku hio hio nikameza tena pills pale nikala mavitu yangu yaani Kwa hasira Sana, kesho nikazima Simu sikuenda kazini, jumatatu nayo ivo ivo nipo tu ndani maisha Yale Yale sikwenda kazini tena kesho yake, Simu nimezima hapo... Kula nakula mara Moja hapo utakuta nimekula kitu simple tu nakaanga ndo inakua imetoka, kazini sijatoa taarifa yoyote, hio jumatano hapo nipo stimu vibaya naskia geti linagongwa kumbe ni wafanyakaz wenzangu, jamaa wanaingia ndani wanashangaa huyu jamaa anaishi vipi... Wananiangalia pale hawanielewi.... Jamaa wanchek pale mezani Kuna vitu hawanielewi, mmoja akaviangalia pale ananiuliza mbona jamaa unatumia hivi vitu una shida gani aisee.....


Wakajadili pale naona wananipotezea muda tu natamani hata kuwafukuza ila kaheshima flani tu hapo, mmoja akasema huyu jamaa inabidi nimpeleke Kwa mtaalam wangu Fulani kashachezewa huyu.... Basi bana tukaongea pale wakaondoka....


Nikapitisha wiki sijaenda kazini bila taarifa yoyote Ile, hapa nimeelezea Kwa ufupi Sana ila Hali ilikua mbaya nilishaanza kua nusu Teja kabisa....



Basi tu Kuna siku flani namuwazia mama mzazi na maisha nayoishi,nawaza wanangu hapo,sijui ikawaje tu Nikapata msukumo flani nikampigia mama Sasa nikamueleza mambo mengi tu pale hapo najihisi Sina amani kabisa mama badae akaniambia "njoo tu huku utengenezwe huko washakuchezea"
Aiseee
 
Mwanetu asingekuwa na Umatemate angekuwa Mtaan anaokota makopo au Magereza kabisa japo nisingependa afike huko kabisa!

Champ najua ushatoka kabisa huko
Zamani mimi ni mtu mzima! Hila huyu jamaa ulimwengu anaoishi na aina ya wanawake anaowaoa mimi hapana kwakweli! Kwanza mimi sipendi familia ambazo hazijimudu na za kiswahili! Huyu jamaa amegharimika sana kwasababu kajiingiza familia choka mbaya! Eti watu wa vikoba wanakuja kusomba vitu kwasababu ya marejesho jamaa chapu anaokoa jahazi kwa 600k?? Sasa hiyo mimi ningewaambia nimetoa "mahari" msinidai tena! Sijui mambo ya tambiko lete ngombe watatu na hela juu, duuuh!
 
Back
Top Bottom