Ushawahi kujichanganya kimapenzi mpaka ukawa unawaza hapo nyuma ulikosea wapi?

Ushawahi kujichanganya kimapenzi mpaka ukawa unawaza hapo nyuma ulikosea wapi?

S2 episode 2


Sijakaa sawa dada wa mgahawa anapiga tena, " Shem upo wapi?" Nashangaa huu ushem wa lini tena, nikamuelekeza nilipo akaniambia tunakuja akakata simu. Baada ya muda kweli nawaona huyu hapo na rachel, Rachel amevaa kigauni flani ivi amejibeba kweli kweli, yule dada wa mgahawa alikua mcheshi sana akafika akaniambia " haya mtu wako huyo hapa mbembeleze mwenyewe mi nimechoka"... Nikamvuta rachel namuuliza kuna shida gani akaniambia tu we futa hio picha ndo tutaelewana, basi bana wakala pale na vinywaji kidogo yule dada wa mgahawa nikamuambia tafuta usafiri wako mapema sisi leo hatujamaliza kubembelezana... Rachel ni kama alianza kusita ila badae akakubali tukaenda kulala wote kwangu hio siku safari mpya ya mapenzi ikaanza


Kuhusu rachel sasa, ye aliishia la saba, kalelewa familia duni na mama tu na ana wadogo zake wawili mmoja wa kike alikua form 1 bado mwingine wa kiume mdogo yupo la pili, mama yake nae kazi haieleweki yani ni kujishkiza hapa na pale tu, basi tukaanza penzi la rachel sijui hata niliwaza nini miezi mitatu tu ya kwanza mimba tayari, hapo nimemchunguza kidogo sana ila nikasema sawa tu, akawa anakuja kwangu anapika, anafanya usafi kuna muda ni kama alihamia tu kwangu kabisa



Tofauti sasa nikaanza kuiona rachel kwao ndo tegemezi kwa hiyo bills zote nikawa nalipa mimi kupitia yeye, mara sijui ana michezo anadaiwa, yaani vitu ambavyo sikuzoea kutoka relationships za nyuma, ila nikawa siwazi kwani financially nilikua sipo vibaya na nawaza huyu anabeba mtoto wangu sitaki apate stress, sasa kuna siku nipo kazini, ikaingia sms namba mpya "mwanangu mna mpango gani na mwenzako na hio hali yake mtakuja lini kujitambulisha?"


Nikawa kama sielewi elewi hivi, jioni nikamuuliza rachel hii namba ya nani akaangalia akasema hii ya mama nilimpa namba yako, nikabaki nashangaa, nikaanza kuona red flags, mbona kama uswahili sasa huu, mama mkwe anaanza kuntafuta mimi alafu tena kwa sms, nikasema something is not right hizi familia nazoingia huku nitanyooshwa tu
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] eti nisije kunyooshwa
 
Mkuu umeliwa na usipoangalia hicho kibarua kitaota nyasi
Haha uzuri wake wengi wameshamuelewa ila ndio hivyo ataondoka kwa hizi kero na hili naliweka wazi kabisa. How will I be happy with all these disappointing thing in entire of my life.? The wedding lock bado sana kwangu labda kwenye 40's huko
 
Episode 6


Hapo akili ikaanza kuwaza kwa kasi, nikakumbuka kuanzia Mary namuona kule shuleni kwao, that innocent girl leo hii anakua hivi kwasababu yangu, nikajikuta chozi linatoka,nikamtumia sms, nakuja mke wangu nakupenda, sikuaga hata mtu nikaondoka zangu ofisini kwenda nyumbani, hapo samira nae anapiga simu sipokei, sms sijibu, ikaingia roho nikaanza kama kumchukia tena samira, ila nikawaza she is just another innocent girl mimi ndo mwenye makosa, hakuna namna ya kurekebisha hapa....huyu nae akijua, amejitunza kote huko leo hii ajue nilimtoa usichana kumbe nina mke, nikasema hapa there is no winning nimejichanganya tu tena sana



Nafika home nakuta Mary ashalewa tena, analia tu, dah nikasema ndo maisha gani haya tena, ikawa hakuna namna nambembeleza tu ikabidi pombe zote nitoe ndani nikazifungia kwenye gari, imefika muda nikatoka kwenda kumtafutia chakula nae katoka kuna grocery pembeni kaenda kanunua wine tena, narud hayupo kumkuta ndo huko tena analia tu watu wanamshangaa nikajiskia vibaya sana, sikuwahi kumuona hata amelewa tangu nimjue, nikambembeleza tukaenda home, yule dada wa grocery akaniambia mdogo wangu badae uje


Nikarudi home Mary kula akagoma nikambembeleza akawa amelala, nikatoka mpaka grocery hapo kichwa kina moto nikabugia konyagi ndogo kwanza bila hata kupumzika, yule sister wa grocery alikua mshkaji wangu kiaina ila Mary hakua na mazoea kabisa na majirani, ananiuliza kulikoni wifi kafanyaje ikabidi nimueleze tu ilivyokua, nae akaanza kunchamba na mwenzake "kaka una mke mzuri hivo anafanya kazi nzuri unataka nini tena"



Akili ikaruka, kazini sijaaga, kuna Mary hapa sijui nadeal nae vipi, Kuna samira hapa nae namfanyaje, aisee sikuwahi kua na siku nzito kiasi hiko
Maisha bana, jamaa ana kistori flan hivi Kama movie, Kisha Kisha nyingii? Anyway mim naomba MUNGU nipate mwanamke mwema, awe mzuri, asiwe mzuri, awe mweupe, awe mweusi, awe bikra asiwe bikra vyovyote vile naomba mwanamke mwema I'll be loyal to her.

Nimeshatrooomba sana, nataka kutulia Sasa.
 
S2 episode 8


Basi baada ya kutuma hio sms Rachel akajibu
" Yaani sipendi mwanaume asiyejiamini, marafiki zangu kuja imekua shida ulitaka nani aje kunitembelea, mbona wa kwenu wameshindwa kuja, kama ni mtoto unasema sio wako sawa tu ntamlea mwenyewe wala siwezi kushindwa, siku ya kwanza tu mtoto tumeanza na kugombana, hivi Patrick unajua nimekuheshimu kiasi gani mpaka nimeamua kukuzalia, unajua wangapi walikua wanalilia hio nafasi? Sawa niache tu basi mi ntakaa na mwanangu"


Sasa hapo ndo nikazidi kupata hasira, yaani huyu binti anaona kama ananisaidia kua nae, nikawa nawaza yanii hata sikustahili kua na huyu binti

Sasa hapa nizungumze jambo moja ila sio kwa ubaya msije kusema mi ni mbaguzi, Rachel kama nilivyosema shule ilikua hamna, yanii nikitoka kazini kuna mambo mengi siwezi zungumza nae tofauti nilivyozoea na Mary, siwezi muelezea mambo yangu ya kazini, ye pia hana cha kunielezea, yaani career wise niliingia kwenye maisha mengine kabisa, kuna muda unaandikiwa sms naomba hera badala ya hela, ni vitu nilivyokua naona kabisa nimeji downgrade lakini nikawa naamini familia haijengwi kwa elimu tu bali upendo na nidhamu, sasa mtu kama huyu tena anaona kama ananisaidia tena mimi, hapo ndo nikazidi kuchoka kabisa



Nikapiga zangu mtungi ikafika mida kama ya saa 4 usiku nikamtumia tu sms ya jina la mtoto maana alikua wa kiume mi huyo nikaenda zangu nyumbani sikurudi tena hospitali, nafika home mama mkwe na ananipigia anaongea kwa furaha ananiambia mwanangu naskia mjukuu wangu anaitwa fulani bora sasa na mimi niitwe bibi fulani, nikaongea nae tu kawaida tukatakiana usiku mwema pale, huyu mama alikua mtu mmoja mwenye hekima sana sikuwahi kugombana nae, mpaka nikawa najiuliza huyu Rachel hizi tabia ametoa wapi


Kesho asubuhi nikaamka nikaenda hospitali nikakuta mdogo wake Rachel(tumuite Gracy) katoka kuwaletea supu pale, nafika mama mkwe akanivuta chemba, akaanza "mwanangu kama ntakukwaza nisamehe kwani jana mmegombana nini na Rachel mbona alikua analia usiku na sasa anasema anataka kwenda kukaa nyumbani kwangu hataki muende kwenu"?


Nikawaza pale nikaona huyu binti ni mpuuzi sana nikamuambia mama mkwe usijali wala sijagombana nae chochote kama anataka hivyo we nenda nae tu mbona kote ni nyumbani tu na sio mbali ntakua nakuja tu, basi bana hapo nina hasira nikaenda nikalipa bills zote pale hospitali, nikawaitia taxi sikutaka hata kuwapeleka nikasema nawahi kazini, basi walivyotoka kuingia kwenye taxi nikatoa laki moja nikampa mama mkwe nikamwambia mama hii ya tahadhari, akashtuka kabla hajapokea akaniambia "mwanangu kwanini asikae nazo mama fulani(jina nililompa mtoto sasa) nikamuambia hapana kaa nazo wewe tu huyo ana uchovu, nikampa zile pesa mi nikaondoka zangu


Nikafika kazini kuna mbuzi nilikua nimeagiza nikamtuma kijana mmoja nikamuambia akifika huko kwao amchinje kabisa awaandalie awape kwa ajili ya mzazi( kimila sisi lazima mzazi achinjiwe, hata kama ni kuku)... Nikiwa kazini nikawa maendeleo namuulizia mama mkwe Rachel hata nikawa sihangaiki nae mpaka kuna muda akanitumia sms " mme wangu nisamehe kama nimekukwaza, naona hauko sawa na mimi naomba tuwe sawa kwa ajili ya mtoto wetu"
Nikamjibu hisia zako tu mi npo sawa!!! Hapo nina mixed emotions, moja nina furaha kupata mtoto wa kwanza huku kwingine nakwazika na tabia za Rachel na mashaka juu ya mtoto pia.....


Basi tumetoka kazini nikapita kwa kina Rachel na wafanyakazi kama wawili wenzangu tukakaa pale kwa muda, piga supu nini badae sana tukaaga kwenda bar kidogo kupiga gambe, haikupita muda mama mzazi ananitumia sms "hongera zako,huyo mme wangu anaitwa nani?"



Nabaki nashangaa nani tena kamuambia
 
Back
Top Bottom