Ushawahi kujichanganya kimapenzi mpaka ukawa unawaza hapo nyuma ulikosea wapi?

Ushawahi kujichanganya kimapenzi mpaka ukawa unawaza hapo nyuma ulikosea wapi?

S2 episode 9


Mama namjua ni mtu wa maneno mengi nikawa nimempotezea tu mpaka kesho yake nikampigia tukaongea nakamuambia jipangane tu mje mumuone mjukuu sasa akasema hakuna shaka

Baada ya Rachel kujifungua imepita kama wiki 2 ivi kuna siku mama mkwe ananipigia anauliza baba upo wapi namuambia npo najiandaa kutoka kazini hapa akaniambia njoo mara moja kuna shida nyumbani, basi nikatoka haraka nikaenda kufika pale nakuta kama kuna hali ambayo siielewi kama kuna watu watu wengi, nafika nikamvuta mama mkwe pembeni namuuliza nini tena hapa ndo ananiambia kua Rachel anadaiwa na wanakikundi wenzake sijui wameenda dukani kwake wamesafisha kila kitu hapa wapo kwangu wanataka kuchukua tv yangu kwa nguvu, nikachoka kwanza nikauliza kikundi gani hiki, na dukani wamechukuaje vitu mbona pamefungwa yeye mwenyewe ni kama haelewi


Basi nikamuita sijui ndo mkubwa wa kikundi naona wanakuja kama wote nikawapiga biti pale nataka kuongea na mmoja tu, akaja namuuliza mnadai bei gani anadai bado kama laki 6, kutokana na ile hali ya aibu pale nikaingia kwenye gari nikatoa laki 3 nikampa na namba zangu nikamuambia hio nyingine ntakupa kesho, ni kama alitaka kugoma ila kuna jicho fulani nilimkata akapokea hio pesa



Mama mkwe nae akaanza kuniomba msamaha pale ananiambia mwenzako sijui ana shida gani mbona mambo ya aibu haya mwanangu, sikumjibu kitu mi nikaondoka zangu, nikawa nawaza hapa sichezewi michezo ya kiswahili kweli? Hivi kweli ndo nimekuja tengeneza familia na watu kama hawa kweli? Hio siku yalinishinda kuna rafiki yangu mmoja nilimpigia nikamuelezea situation zote aisee mpaka akashangaa, mwishowe akanionea huruma akaniambia tu we angalia jinsi utavyokuja kumpata mwanao basi



Huku maisha yakasonga mi nikawa naenda tu wasalimia pale kwa kina Rachel nawapelekea mahitaji na nini, sasa ikapita zaidi ya mwezi mama na sister wakawa wanakuja mwanza, hapa katikati mahusiano na Rachel ndo yapo ivo ivo sema moyoni nilikua nishamtoa namuwaza mwanangu tu, nikampa taarifa mama mkwe kua amuandae binti aje huku kwangu ila akifika mama amkute nipo nae huku


Sasa sijui ni kiburi au ujinga wa huyu binti, akagoma kutoka kwao akasema watakuja kumsalimia huko huko, hapa nadhani alikua ananikomoa maana baada ya kumlipia lile deni na kuona ameua biashara niliacha kumpa financial favour yoyote, nikawa mme kwa kipemba kila kitu nanunua au namtuma boda, maisha ya kuniomba mara laki laki 2 nikapiga full stop, kwanza nikawa nawaza huyu sina hata malengo nae, hio siku nilichukia nikaenda kwao kufika baada ya maongezi ndo nikawaambia mama na dada wanakuja inabidi mje kwangu sasa, rachel anadai mi siendi kama kunisalimia watakuja huku huku, nikawa nimechukia nikawaambia basi nipeni mtoto wamkute kwangu kama we hutaki kuja baki



Rachel nae sijui ni wehu au nini akaropoka " mtoto mwenyewe hata mahari hujamlipia unaongelea mtoto gani? "

Sijakaa sawa mama yake akanyanyuka akaanza kumpiga huku analia "mwanangu mbona unanitia aibu kiasi hiki una shida gani mbona huniheshimu au mimi sio mama yako, unajua nimehangaika na wewe vipi?"


Nikaona huu ujinga sasa mimi huyo nikaondoka zangu, nikaanza utaratibu mpya, situmi matumizi wala simu zao nikawa sipokei, haikupita siku mama na sister wakaja tukafanya mpango tukaenda wasalimia, sasa sijui kina mama wanakua na nini naona mama akawa busy tu anamkagua mtoto muda tunaondoka akaniambia huyu ni wa kwetu kuna kishimo nimekiona sikioni wanangu wote niliwazaa mkiwa nacho, nikapata faraja kidogo ila hapo bado machale yanacheza tu


Basi kina mama wakawa wanaenda kusalimia huko wanashinda jioni wanarudi kwangu, sister sasa ndo akaanza kunchamba ananiambia mdogo wangu kweli ulimuacha Mary ndo umeanguka huku..... Nakuonea huruma...... Walikaa kama siku 4 wakaaga wakaondoka wakiwa njiani naona sms ya mama "mwanangu asante kwa mjukuu, anza sasa kutafuta mke hapo hamna mke"
Yaani "MKUU" ndio tumeishia hapa kweeli,,, umesababsha nichelewe bas la kwenda Mwz zen unaishia hapa,!!?

Mwisho wa Mary tumeuona ila wa Samira naona km Kuna kitu umeficha tusikijue kuhusu yy maana Kwa Akili za kawaida baada ya kukutana na yote hayo Opportunity cost baada ya kuforgone Mary na Recho tulijua ungekua na akili ya kumrudia Samira ili kuondokana na uswahili usio na na chembe ya ustaarab
Nilichikiona kingne wee ulikua mchanga sana wa mapenzi, nginjangija umekuja kutana nazo kwenye kuoa badala ya uteenager,,
Pia amini usiamini after a long run kwenye Maisha ya ndoa either na Samira/Mary uliowatoba wangekuja kuchepuka tu kutaman kulonja zingine maana ndio kitu hawakua wamefanya ktk ujana wao, yaani ingefka time wangetaka kufanya "ujana"
 
Yaani "MKUU" ndio tumeishia hapa kweeli,,, umesababsha nichelewe bas la kwenda Mwz zen unaishia hapa,!!?

Mwisho wa Mary tumeuona ila wa Samira naona km Kuna kitu umeficha tusikijue kuhusu yy maana Kwa Akili za kawaida baada ya kukutana na yote hayo Opportunity cost baada ya kuforgone Mary na Recho tulijua ungekua na akili ya kumrudia Samira ili kuondokana na uswahili usio na na chembe ya ustaarab
Nilichikiona kingne wee ulikua mchanga sana wa mapenzi, nginjangija umekuja kutana nazo kwenye kuoa badala ya uteenager,,
Pia amini usiamini after a long run kwenye Maisha ya ndoa either na Samira/Mary uliowatoba wangekuja kuchepuka tu kutaman kulonja zingine maana ndio kitu hawakua wamefanya ktk ujana wao, yaani ingefka time wangetaka kufanya "ujana"
Bro, You're a great Thinker. Ndo maana me sipendi kujilaumu kwa yaliyokwisha tokea, huwezi kuikimbia hatima. Huenda angebaki na huyo marry/samira still kuna wakati ambao angejutia kuwaamini. Angeanzisha tena uzi wa kwanini asingechepuka mapema. Marry na samira hawajapitia hekaheka za ujana wangekuja kumsumbua sana

"Normal is boring"
 
Nafikiri ilibidi iwe hivyo ilivyo 😂 HAKUNA kosa lolote zaidi ya matokeo ya machaguo😄😄😄

Maisha yana ladha zote (chungu,tamu,furaha,majonzi) yote hayo nimatokeo ya chaguzi HAKUNA chaguzi yenye furaha pekeee...ila akili inaturejesha kwenye hadidu za ulinganifu nakuona kuna kosa😂😂😂enewei

Ukimchagua mwanamke kadiri ya maandiko ametokana na ubavu bas jua umechagua kilicho dhaifu kadhalika ukimchagua mwanaume tambua Hana mbavu moja🤣😂 NI dhaifu pia....😄😂😂😂
 
S2 episode 10


Mama namjua nikampotezea tu japo nafsi yangu ilikua inaniambia kile kile ambacho kilikua kipo moyoni mwangu, lakini kitendo cha kuendelea kufanyiwa kiburi na Rachel ch kugoma kuja nyumbani hata wageni walipokuwepo nikasema hakitapita hivi hivi, nikasema ni muda muafaka sasa wa kuacha kujifanya kijana mwema sana, mimi huyo sasa nikakata mawasiliano na Rachel pamoja na mama yake, yaani hivo tu, simu sipokei, sms sijibu, hakuna cha matumizi wala nini, kitu pekee nachokumbuka kutuma tena namtuma mtu ilikua pampers za mtoto, sabuni za kufulia, mafuta ya mgando ya mtoto na wipes!! Nikitoka kazini nachelewa kurudi nyumbani basi tu nikaanza ratiba mpya nazojua mimi



Wakalalamika sana kwa sms lakini wapi mi npo kimya tu, wanakuambia dawa ya jeuri ni kiburi, imepita kama mwezi siku natoka zangu kazini nafika nyumbani namkuta Rachel yupo na mtoto, mama mkwe na mdogo wake(Grace) wananisubiri, nikajifanya kama sijashtuka wala nini nikafungua nikawakaribisha ndani, basi na wao wakazuga kama hakuna tofauti yoyote tukawa tunapiga story kawaida badae nikamwagiza boda akaleta mahitaji pale wakawa wanapika mi nikatoka nikawaacha pale, nimerudi badae mama mkwe kashaondoka yupo Rachel na mdogo wake



Rachel ndo akawa karudi sasa kwa style hio maisha yakaendelea badae tukawa sawa tu ila ndo hivyo ukishakosa imani na mtu mnaishi kwa machale tu sana, kufupisha sana mambo japo katikati hapo ugomvi haukosekani, mtoto ndo ana kama miezi 9 ivi, ikatokea nafasi kazini za kwenda training nje, mwanzo sikutaka kwenda ila kuna bosi wangu akanishauri niende nikirudi anaweza nibadilisha kitengo chenye maslahi zaidi, nika apply zile nafasi nikakaa kimya kusikilizia majibu maana waliokua wanataka walizidi nafasi zilizotolewa



Baada ya kama mwezi majibu yakatoka nimepata nafasi ila kuondoka ilikua kama baada ya miezi miwili, na kule ni kwenda kukaa wiki 8, nilivyoona posho ambayo tutakua tunalipwa kule nikaona si haba nikapata msukumo nitafute eneo ninunue nijenge hata msingi kabla sijaondoka, nilikua na akiba yangu fulani kweli nikafanya mpango nikapata kiwanja kikubwa tu pembezoni kidogo ya jiji nikaanza kujenga msingi kimya kimya hapo sijamwambia mtu wala hata sikuona sababu....



Hapo swala la safari wanalijua sema muda bado ulikua haujafika, sasa kuna notebook moja nilikua naandika mahesabu ya site ili co monitor cost Rachel akaja kuiona akawa ananiuliza hayo mahesabu ya nini, nikamwambia kuna mahali nimenunua najenga msingi huko, akakaa kimya ni kama mtu ambae hakufurahishwa maana hata hakuniuliza ni wapi, mchana npo kazini napata ujumbe toka kwake nae kaandika business proposal yake sijui biashara gani anataka milion 3 kabla sijaondoka ya biashara yake, nikamjibu tu plain sina pesa kwa sasa huoni kama najenga



Aisee ni kama nilipalilia moto, huyu binti kumbe alikua na mdomo sana nilikua simjui vizuri
 
Back
Top Bottom