Ushawahi kulala njaa kwa kukosa pesa ya kula? Ulifanyaje?

Ushawahi kulala njaa kwa kukosa pesa ya kula? Ulifanyaje?

daxy Jr

Member
Joined
Apr 15, 2020
Posts
88
Reaction score
307
Hii ilinitokea kati ya mwaka wangu wa 2 na wa 3 wa chuo kikuu. Nilifanya kibarua cha kuhudumu kwenye mgahawa kila nikitoka chuo ili kujikimu na mahitaji yangu ya chuo, Pesa ilikua ngumu sana.

Nilijiskia aibu ila ilibidi nifanye kile nilichokifanya ili niweze kuishi. Kuna muda nilikua nakusanya chakula cha wateja walichobakiza kisha ningekila bila watu kuniona. Boss hakua rafiki sana hivyo alinipatia msosi mara mojamoja sana akijiskia - hizo zilikua siku nzuri

Sijawahi kuwa maskini kiasi kile tena!
 
Aisee mara nyingi tu, nilichojifunza ni kuwa njaa haizoeleki !
 
Nachojua huwezi kufa njaa katika taifa lisilo na janga la njaa, ila kula deshi kawaida tu.
 
Back
Top Bottom